UTANGULIZI WA FASIHI YA KISWAHILI KF 102 Prof

  • Slides: 72
Download presentation
UTANGULIZI WA FASIHI YA KISWAHILI KF 102 Prof. Aldin K. Mutembei (Ph. D) Ofisi

UTANGULIZI WA FASIHI YA KISWAHILI KF 102 Prof. Aldin K. Mutembei (Ph. D) Ofisi # 317 Jengo la Kiswahili Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, CKD

LENGO KUU na MUHIMU Kuhusu Usomaji katika CKD Kuwajibika na Kuondoa woga

LENGO KUU na MUHIMU Kuhusu Usomaji katika CKD Kuwajibika na Kuondoa woga

Mambo ya Jumla kuhusu Maisha ya Chuo Kikuu • Wajibu wako kama Mwanafunzi •

Mambo ya Jumla kuhusu Maisha ya Chuo Kikuu • Wajibu wako kama Mwanafunzi • KUSOMA: →Usomaji wa binafsi; →Nguvu ya Makundi; →Kujisomea Maktaba (Majengo); →Maktaba za Mkondoni.

Maisha ya Chuo… • ZINGATIA UMUHIMU HUU: ØAndika vizuri, kwa uwazi, na moja kwa

Maisha ya Chuo… • ZINGATIA UMUHIMU HUU: ØAndika vizuri, kwa uwazi, na moja kwa moja ØUwe na mwonekano tofauti kama Mwanachuo ØKuna Mtu wa Mitaani (lugha, mavazi, ujengaji hoja), na Mwana CKD • Huwezi kusoma kwa makini hadi Ujisake: Wewe ni Nani?

Maisha…MTU MWENYEWE • Falsafa ya Sufi Bayazid • Kujitambua, Kujithamini, Kujipenda (LUGHA, mavazi na

Maisha…MTU MWENYEWE • Falsafa ya Sufi Bayazid • Kujitambua, Kujithamini, Kujipenda (LUGHA, mavazi na FIKRA) • Unajitambua? Unaweza kumtambua mwingine. • Unajithamini? Unaweza kumthamini mwingine. • Unajipenda? Unaweza kumpenda mwingine

Maisha…TUNAVYOKUTARAJIA UWE • Umekuja kusoma na Kuelimika. ØTunataka hatimaye kuona matunda ya Elimu Yako

Maisha…TUNAVYOKUTARAJIA UWE • Umekuja kusoma na Kuelimika. ØTunataka hatimaye kuona matunda ya Elimu Yako • Umekuja kuhesabika kuwa miongoni mwa wachache wenye bahati ØTunataka kuiona bahati hiyo • Itumie bahati hiyo bila kuichezea • Umekuja Kusoma na Kufaulu

Maisha…CKD Kikujengee UZALENDO: • Uzalendo na Kupenda nchi yako. Kuwa tayari kuipigania na Kuitetea

Maisha…CKD Kikujengee UZALENDO: • Uzalendo na Kupenda nchi yako. Kuwa tayari kuipigania na Kuitetea • Uzalendo wa Kupenda yaliyomo katika nchi yako, kuyatangaza na kuyasimamia. • Uzalendo wa kupenda lugha yako: kuitumia na kuieneza. • Ikiwa huwezi kujipenda, na kuwapenda wengine, ni vigumu kupenda nchi yako.

Mihadhara ya Chuo na Usomaji • Hujengwa kwa KUSIKILIZA na kuandika kilichozungumzwa • Sio

Mihadhara ya Chuo na Usomaji • Hujengwa kwa KUSIKILIZA na kuandika kilichozungumzwa • Sio kunakili tu yaliyoandikwa (notes) • Sio kutoa tu nakala (photocopy) • Jenga, uwezo wa – kusikiliza, kutambua kilichosemwa – Kuchukua unachoona kinafaa – Kuandika yale yatakayokukumbusha kilichosemwa • Kamwe usikariri. Ni makosa makubwa sana kukariri, bila kuelewa inachosemwa. Hakikisha hutoki nje ya darasa bila kuelewa kilichosemwa.

UHURU WA MAWAZO Jenga hali ya kujiamini. Jenga uwezo wa kutoa hoja. Anza taratibu,

UHURU WA MAWAZO Jenga hali ya kujiamini. Jenga uwezo wa kutoa hoja. Anza taratibu, na jizoeze kutoa hoja. Usijitetee kama huna cha kujitetea, ila Usinyamaze ikiwa unalo la kusema. Kupinga kwa hoja kwa nia ya kukuza maarifa ni tabia inayotarajiwa kwa msomi. • Msomi mzuri hutoa mawazo yake bila woga na kuwa tayari kukosolewa au kukosoa wenzake. • • •

Uhuru wa Mawazo… • Mwalimu si adui, ni rafiki anayetaka kupitia kwake upande ngazi,

Uhuru wa Mawazo… • Mwalimu si adui, ni rafiki anayetaka kupitia kwake upande ngazi, ufike juu. Juu sana. • Walimu wazuri huwaruhusu wanafunzi kuwapita, na hujivuna pale wanapowaona wanafunzi wao wakiwa katika nafasi mbali za juu: Kimasomo, Kimapato, Kimaisha n. k • Ninawatia moyo na kuwakaribisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. • Mmekuja kusoma, kuelewa na kufaulu!

Kazi ya Nyumbani • Kila mtu asome na kutafakari Makala ya mwaka 1971: Matumizi

Kazi ya Nyumbani • Kila mtu asome na kutafakari Makala ya mwaka 1971: Matumizi ya Kiswahili Nchini, Shuleni na Vyuoni (J. K. Kiimbila) Katika Kichocheo cha Uchunguzi wa Kiswahili, uk. 60 -69. Makavazi. • Linganisha mawazo hayo ya zaidi ya miaka 40 na mawazo ya sasa. Je kuna kipi kipya? – Novemba 21, 2018

Mihadhara: UTANGULIZI… • Tunajifunza somo hili tugundue nini? • Sanaa ni njia ya mwanadamu

Mihadhara: UTANGULIZI… • Tunajifunza somo hili tugundue nini? • Sanaa ni njia ya mwanadamu kujieleza • Fasihi kama kioo cha jamii – kinaioneshaje jamii? • Lugha kama kioo cha fikra – kinazionesha fikra zipi • Lugha kama kichukuzi cha mila – inachukua mila zipi

MIHADHARA • Fasihi ni Nini? • 1. HISI: Sio tu suala la hisia, bali

MIHADHARA • Fasihi ni Nini? • 1. HISI: Sio tu suala la hisia, bali ni uoneshaji wa mahusiano baina ya watu; na watu na dunia yao katika jamii kwa njia ya kisanaa. • 2. KIOO CHA JAMII: Ni zaidi ya Kioo. Haituoneshi tu, bali ni mjadala wa harakati za mwanadamu katika kuyaingia maisha, kuyatengeneza, kuyabadilisha, kuyaishi na hatimaye kuachana na maisha.

Mihadhara… • Fasihi ni Nini? • 3. MAJADILIANO: Hujadili maisha kwa kipindi fulani cha

Mihadhara… • Fasihi ni Nini? • 3. MAJADILIANO: Hujadili maisha kwa kipindi fulani cha historia, historia yenyewe, chimbuko la jambo na mustakabali wake. • 4. ZAO LA HISTORIA, huiitika historia, na huchongwa na historia. • 5. NI SANAA ambayo hutengenezwa kutokana na mchakato wa kihistoria na kiharakatika maisha ya jamii.

Chimbuko la Fasihi • Hivi Fasihi ilitoka wapi? Na Je kila Jamii ina Fasihi

Chimbuko la Fasihi • Hivi Fasihi ilitoka wapi? Na Je kila Jamii ina Fasihi au Fasihi ni kwa wachache? • Kuna Nadharia au Mitazamo 4 • 1. Chimbuko lake ni Mungu/Miungu (dhanifu) – Imekuwapo duniani kama zawadi toka kwa mungu kwa wateule wachache – Mungu mwenyewe ni msanii Mkuu – Nyimbo mf. Ooh Lulu

Chimbuko …/ • 2. Chimbuko lake ni nguvu ya miujiza au sihiri – Kujaribu

Chimbuko …/ • 2. Chimbuko lake ni nguvu ya miujiza au sihiri – Kujaribu kukabiliana na kuyashinda mazingira. – Kuchora, Kuchonga, Kujenga vijumba na kunuizia – (SIKU HIZI) Kuombea vitambaa au Kifaa n. k • 3. Chimbuko ni Mwigo – Kuiga mazingira, sauti, mwonekano, wanyama, ndege, nk – Kubuni hali ya ufanano – Ushairi ulichimbuka kutoka ktk kuiga – Mwanadamu ni kiumbe wa uigaji, tokea mtoto – Ni mwigo ukimaanisha uwakilishi wa jambo kwa jingine. Ni taswira inayolenga kuonesha jambo

Chimbuko …/b • 4. Chimbuko ni Mabadiliko ya Mwanadamu (Yakinifu) katika kuyadhibiti mazingira •

Chimbuko …/b • 4. Chimbuko ni Mabadiliko ya Mwanadamu (Yakinifu) katika kuyadhibiti mazingira • Marx na Engels wanaingalia Fasihi kama zao la mabadiliko katika maisha ya mwanadamu ambayo hutawaliwa na – Mfumo wa uzalishaji mali – Uhusiano katika uzalishaji mali – Mfumo na Uhusiano hutokeza MATABAKA • Fasihi ni zao la Matabaka na Uhusiano katika uzalishaji mali • Katika uhusiano mwanadamu alihitaji lugha

Dhima ya fasihi • Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea mwulizaji anatoka katika

Dhima ya fasihi • Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea mwulizaji anatoka katika tabaka lipi na kwake fasihi ni nini. • Kuburudisha • Kuhimiza Kazi na Kujenga moyo wa kazi • Kujenga tabia: Kuonya, Kuasa, Kufunza • Kuelimisha • Kuhifadhi kurithisha amali za Jamii (mila, desturi, thamani n. k) • Kukuza na Kuhifadhi lugha

Dhima…/ • Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea mwulizaji anatoka katika tabaka lipi

Dhima…/ • Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea mwulizaji anatoka katika tabaka lipi na kwake Fasihi ni nini. • Kuendeleza harakati fulani katika Jamii • Ujenzi wa Utaifa • Kuleta Ukombozi: Hasa wa kifikra, kisiasa, kiuchumi, kitabaka, kijinsia, n. k • Fasihi ni zao la Kitabaka. Tabaka husaidiwa na itikadi katika Kujiimarisha • Itikadi: Mfumo wa mawazo, imani kuhusu mahusiano na maongozi ya watu ktk Jamii

Dhima za Fashi ktk maisha • • • UCHUMI ITIKADI SIASA UTAMADUNI FALSAFA UJUMI

Dhima za Fashi ktk maisha • • • UCHUMI ITIKADI SIASA UTAMADUNI FALSAFA UJUMI

Dhana ya fasihi ya Kiswahili • Waswahili wenye hii Fasihi ni kina nani? •

Dhana ya fasihi ya Kiswahili • Waswahili wenye hii Fasihi ni kina nani? • Fasihi hutambulishwa kwa Lugha: Kiswahili • Wenyeji wazungumzao Kiswahili katika Afrika Mashariki na Kati na Visiwa vya Bahari ya Hindi katika Mwambao wa Afrika mashariki • Inayoeleza utamaduni na maisha ya Waswahili • Rej. Mulokozi, 2017: Sura 3. Fasihi ya Waswahili, Fasihi ya Kiswahili na Fasihi kwa Kiswahili (30 -33). • Je Fasihi ya Kiswahili na Fasihi ya Kitaifa ni Dhana ile? (Mutembei, 2004: Mulika No. 26).

Maendeleo ya Fasihi Katika Mifumo Mbalimbali ya Maendeleo ya Binadamu • Kwakuwa tumezungumza kuwa

Maendeleo ya Fasihi Katika Mifumo Mbalimbali ya Maendeleo ya Binadamu • Kwakuwa tumezungumza kuwa Fasihi ni chombo cha mabadiliko ya Mwanadamu, tuyaangalie mabadiliko hayo, tukijikita katika ufafanuzi wa Karl Marx na Friedrisch Engels. • Kuna Ujima • Utumwa • Umwinyi na Ukabaila • Ubepari • Ujamaa • Uliberali

Sanaa, lugha na fasihi Wakati wa Ujima • • Kuwaunganisha watu Umoja na Ushirikiano

Sanaa, lugha na fasihi Wakati wa Ujima • • Kuwaunganisha watu Umoja na Ushirikiano vilisisitizwa Lugha ilikuwa si changamani Fasihi – hasa simulizi ikihusisha maudhui yasiyo changamani. – Wema dhidi ya Ubaya – Wahusika wanaowakilisha watu halisi – Wahusika na uhusika wao katika jamii: miti, wanyama ndege nk

Kipindi cha Utumwa • Mabwana dhidi ya watumwa • Kupumbaza watumwa na wao kuonekana

Kipindi cha Utumwa • Mabwana dhidi ya watumwa • Kupumbaza watumwa na wao kuonekana kuwa hiyo ni majaaliwa yao • Watumwa kudai ukombozi • Udhibiti wa kazi za kifasihi • Matokeo ya udhibiti: – Lugha ya mafumbo – Wahusika changamani

Kipindi cha Umwinyi na Ukabaila • Mamwinyi dhidi ya watwana • Kupumbaza watwana na

Kipindi cha Umwinyi na Ukabaila • Mamwinyi dhidi ya watwana • Kupumbaza watwana na wao kuonekana kuwa hiyo ni majaaliwa yao • Kustarehesha mamwinyi na makabaila • Udhibiti wa kazi za kifasihi • Harakati za ukombozi – Wahusika changamani

Kipindi cha Ubepari ni nini Matabaka Migogoro ya wafanyakazi dhidi ya Mabepari Migogoro viwandani

Kipindi cha Ubepari ni nini Matabaka Migogoro ya wafanyakazi dhidi ya Mabepari Migogoro viwandani na mashambani Migomo Ukombozi Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui hayo • Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo • Ni nini wajibu wako kama mhakiki • •

Kipindi cha Ujamaa ni Nini Ujenzi wa Taifa Jipya Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa

Kipindi cha Ujamaa ni Nini Ujenzi wa Taifa Jipya Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa Ujenzi wa Sera Mpya Usawa na Ushirikiano Vita dhidi ya Makabaila na Mamwinyi Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui hayo • Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo • Ni nini wajibu wako kama mhakiki • •

Kipindi cha Mfumo wa Uliberali • Maana • Ni mambo gani mapya yanayojitokeza katika

Kipindi cha Mfumo wa Uliberali • Maana • Ni mambo gani mapya yanayojitokeza katika kipindi hiki • Soko huria ni nini na maudhui yake ni yepi? • Utandawazi au Utandawizi • Unajitokezaje katika fasihi • Uhuru wa uandishi na athari za uhuru huo • Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui hayo • Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo • Ni nini wajibu wako kama mhakiki

Tanzu za Fasihi • 3: 1. Fasihi simulizi • 3: 2. Fasihi andishi •

Tanzu za Fasihi • 3: 1. Fasihi simulizi • 3: 2. Fasihi andishi • 3: 3. Kufanana na kutofautiana kwa fasihi simulizi na andishi • 3: 4. Fani na Maudhui katika fasihi simulizi na andishi

3. 1 Fasihi Simulizi • Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na kubuniwa kichwani na

3. 1 Fasihi Simulizi • Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi (Mulokozi, 2017: 38). • Ni tukio linalofungamana na muktadha Fulani wa kijamii. • Mulokozi anatofautisha kati ya fasihi ganizi na fasihi simulizi. • Hakikisha unajua tofauti za dhana hizo kwa usahihi

Changamoto katika Maana ya Fasihi Simulizi • Jina: Simulizi (kusimulia: Oral) – Ganizi (inayoganiwa-

Changamoto katika Maana ya Fasihi Simulizi • Jina: Simulizi (kusimulia: Oral) – Ganizi (inayoganiwa- narrative) • Ufafanuzi: – Kutungwa kichwani – Kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na matendo – Hakuna maandishi • Ufafanuzi huu katika ulimwengu wa sasa • Usimulizi katika Radio na TV

3. 2 Fasihi Andishi • Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na kuwasilishwa kwa hadhira

3. 2 Fasihi Andishi • Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya maandishi (Mulokozi, 2017: 40). • Hutegemea vipengele vitatu: mtunzi, msomaji na mdhamini. • Suala la udhamini hutofautiana kutegemea utanzu wa fasihi andishi unaohusika • Katika maandishi kunajitokeza changamoto ya udhibiti – Ni muhimu jamii ijihakikishie kushikiliwa kwa maadii ambayo yameijenga jamii hiyo.

3. 3 Kufanana na Kutofautiana • Je fasihi andishi hufananaje na fasihi simulizi? –

3. 3 Kufanana na Kutofautiana • Je fasihi andishi hufananaje na fasihi simulizi? – Matumizi ya mbinu za usimulizi katika uandishi – Matumizi ya wahusika na lugha za usimulizi • Ni wapi zinakutana na wapi zinaachana? – Zote ni sanaa za lugha – Zote hujadili migogoro, matatizo na changamoto za mwanadamu katika kuyakabili mazingira yake – Hujadili maana ya kuwako, na mahusiano baina ya mwandamu – Huonesha masuala yahusuyo hisi na Imani – Uchangamani wake hutofautiana

3. 3 Kufanana na Kutofautiana/… • Mabadiliko makuu kutoka katika kusikia – Macho na

3. 3 Kufanana na Kutofautiana/… • Mabadiliko makuu kutoka katika kusikia – Macho na Masikio ni viungo vikuu • Kuingia katika kuona – Macho yakawa kiungo kikuu • Mabadiliko kutoka “neno” sauti, kuwa “kitu”alama ya maandishi. Alfabeti ikasimama kuwa kiwakilishi cha sauti • Neno lilisikika tu, alama sasa inaonekana na kuweza kushikika (karatasi/Kitabu)

 • • • Fasihi Simulizi Chimbuko la fasihi simulizi Tuliangalia chimbuko la Fasihi

• • • Fasihi Simulizi Chimbuko la fasihi simulizi Tuliangalia chimbuko la Fasihi kwa ujumla. Je unadhani ni nini chimbuko la fasihi simulizi? Je fasihi hii ilianzaje? Je ilikuwapo lini?

4: 2. Maudhui na dhima ya fasihi simulizi Tofauti kati ya maudhui na dhima

4: 2. Maudhui na dhima ya fasihi simulizi Tofauti kati ya maudhui na dhima ni nini? Tuliangalia dhima ya Fasihi kwa ujumla. Je unadhani ni nini dhima ya fasihi simulizi? Ufafanuzi wako uendane na vipindi katika mabadiliko ya maendeleo ya mwandamu • Je dhima hubaki ile au hubadilika? Kwa vipi? Kwanini? • •

4: 3. Fani na muktadha wa utendaji katika fasihi simulizi • • Ifafanue dhana

4: 3. Fani na muktadha wa utendaji katika fasihi simulizi • • Ifafanue dhana ya utendaji katika fasihi simulizi. Uainishaji wa fasihi simulizi bado ni changamoto. Je, igawanywe kwa kufuata: Uainishaji wa Balisidya, Uainishaji wa Taasisi ya Elimu, Uainishaji wa awali wa Mulokozi, 1996. Uainishaji wa Kobia, Uainishaji mpya wa Mulokozi, 2017: 51 - 62)

4: 4. Uchambuzi wa tanzu na changamoto zake • Kutokana na Uainishaji, ni dhahiri

4: 4. Uchambuzi wa tanzu na changamoto zake • Kutokana na Uainishaji, ni dhahiri kuwa uchambuzi wa tanzu za fasihi simulizi una changamoto kadha. • Ni muhimu kuzifahamu changamoto hizo. • Ni muhimu zaidi kuwa na msimamo unaoweza kuutetea ni kwanini unapendelea uchambuzi mmoja wa tanzu dhidi ya mwingine.

Moduli ya 5: Fasihi Andishi • 5: 1. Fasili mbali za fasihi andishi •

Moduli ya 5: Fasihi Andishi • 5: 1. Fasili mbali za fasihi andishi • 5: 2. Chimbuko na maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili • 5: 3. Tanzu na kumbo za fasihi andishi ya Kiswahili • 5: 4. Fani na maudhui katika fasihi andishi

5. 1. Fasili mbali za fasihi andishi • Litteratura: Kitu kilichonukuliwa kwa maandishi. •

5. 1. Fasili mbali za fasihi andishi • Litteratura: Kitu kilichonukuliwa kwa maandishi. • Kazi za kiubunifu zinazotumia lugha ili kuwasilisha wazo Fulani. • Kuwakilisha desturi, mila, utamaduni wa jamii kwa njia ya kisanaa

5: 2. Chimbuko na maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili • Kutokea katika fasihi

5: 2. Chimbuko na maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili • Kutokea katika fasihi simulizi • Kazi za mwanzo za ushairi katika hati za kiarabu • Riwaya ya Uhuru wa Watumwa • Kazi za tafsiri

5: 3. Tanzu na kumbo za fasihi andishi ya Kiswahili • 5. 3. 1

5: 3. Tanzu na kumbo za fasihi andishi ya Kiswahili • 5. 3. 1 Tamthilia • 5. 3. 2 Riwaya • 5. 3. 3 Ushairi

5. 3. 2 Fasihi Andishi - Tamthilia • Msingi wa sanaa yoyote ile ni

5. 3. 2 Fasihi Andishi - Tamthilia • Msingi wa sanaa yoyote ile ni uigaji. • Msanii huangalia kitu halisi, kisha hukiiga na kukitoa kwa njia fulani. Akifanya hivyo, usanii wake huwa ni kiwakilishi tu. • Maisha huwa ni mwigo: Mf. Ktk dini twaambiwa maisha halisi yatakuwa mbinguni. Unavyoishi sasa ndivyo utakavyokuwa huko juu (yaani hapa sisi sio halisi). “Tunapita tu” mahali kwetu ni pengine n. k • Matendo ya mila, utani nk, huwa ni uigazi

Tamthilia msingi wake ni Uigaji • Tamth. - andiko la kiuigizaji lenye kuonesha matendo

Tamthilia msingi wake ni Uigaji • Tamth. - andiko la kiuigizaji lenye kuonesha matendo na maneno. Ni igizo la kifasihi lililokusudiwa kutendwa (kuigizwa) jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani. • Istilahi ya tamthilia inatokana na neno mithali, (mithili) yaani mfano, au ishara ambalo msingi wake ni uigaji. Si kitu halisi. • Katika tamthilia, wahusika, matendo yao na nafasi zao humathilisha watu, matendo au nafasi halisi katika jamii. Wamathili

Tamthilia/Onesho/Mchezo • Tamth. - andiko la kiuigizaji lenye kuonesha matendo na maneno • Mlama,

Tamthilia/Onesho/Mchezo • Tamth. - andiko la kiuigizaji lenye kuonesha matendo na maneno • Mlama, 1983: Tamthilia ni sanaa ya maonesho, ambayo huwasilisha ana kwa ana tukio fulani kwa hadhira kwa kutumia usanii wa utendaji (vitendo, uchezaji, ngoma, uimbaji n. k)

Maana ya Sanaa za Maonesho • AINA 3 za SANAA – Za Uonesho-: -

Maana ya Sanaa za Maonesho • AINA 3 za SANAA – Za Uonesho-: - Uzuri umo katika kuona= uchoraji, uchongaji, nk. – Za Ghibu-: uzuri wake umo katika kusikia. ushairi, upigaji muziki, – Za vitendo: -Uzuri wake umo katika kuona na kusikia vitendo. – Aina zinajadiliwa kupitia katika UZURI. Je kazi/dhima?

S. M ni Sanaa za Vitendo • Kitendo cha sifa 4 –Mchezo –Mchezaji –Uwanja

S. M ni Sanaa za Vitendo • Kitendo cha sifa 4 –Mchezo –Mchezaji –Uwanja wa kuchezea –Watazamaji

Udhaifu wa mtazamo huo • Mchezo • Sifa 4 tu • Tamth. Ni ya

Udhaifu wa mtazamo huo • Mchezo • Sifa 4 tu • Tamth. Ni ya Kigeni. Je S. M za asili?

Maana kwa kuzingatia Uafrika: Ni tukio la kijamii lenye sifa: • Dhana Inayotendeka •

Maana kwa kuzingatia Uafrika: Ni tukio la kijamii lenye sifa: • Dhana Inayotendeka • Uwanja wa Kutendea • Watendaji • Hadhira • Kusudio la Kisanaa • Muktadha wa Kisanaa • Ubunifu (umathilishaji)

Sanaa za. Maonesho za Kiafrika • Sherehe – Unyago/Jando, Kutoa jina, kuota meno (hatua

Sanaa za. Maonesho za Kiafrika • Sherehe – Unyago/Jando, Kutoa jina, kuota meno (hatua kwenda nyingine) • Ngoma: (chombo, kitendo, sherehe) • Kusalia mizimu • Kupatikana mapacha n. k

Sana za Maonesho za Magharibi • Mahali pa kuonea. Kinachotendwa • Drama – Mpangilio

Sana za Maonesho za Magharibi • Mahali pa kuonea. Kinachotendwa • Drama – Mpangilio wa maneno huambatana na utendaji wa wahusika – Kuna uigizaji (wa tabia/matendo) – Huegemea katika maandishi – Mpangilio wa jukwa, taa, rangi, sauti. n. k

Historia ya Tamth. Afrika Mashariki • Waingereza Kenya (Iliandaliwa kuwa mahali pa kuzamia na

Historia ya Tamth. Afrika Mashariki • Waingereza Kenya (Iliandaliwa kuwa mahali pa kuzamia na kukaa ) • Ujio na Makazi ya Walowezi –Kuchukuliwa kwa mashamba na Ardhi. (Taz. Mulokozi, 2017: 2223) –Kuanza kurejeshwa kwa maaskari –Mpango wa kuwapumbaza –Ujio wa mtaalamu: Mwalimu

Kenya: Usuli wa kazi za Hyslop • 1944 Mfanyakazi Jeshini – Akaanzisha kitengo cha

Kenya: Usuli wa kazi za Hyslop • 1944 Mfanyakazi Jeshini – Akaanzisha kitengo cha elimu jeshini kuwatumbuiza askari 30, 000 Mash. Ya kati (Waganda, Kenya na Wa Tz) – Muziki na Tamthilia, na Filamu • Mf. 1945: Filamu ya Akili Mali n 1945: - Vita iliisha akarudi Uk

Hyslop… � 1953: Alirudi Kenya kama Mwl. wa Shule akikazia Tamth. �Tamth Zake zikafanyiwa

Hyslop… � 1953: Alirudi Kenya kama Mwl. wa Shule akikazia Tamth. �Tamth Zake zikafanyiwa majaribio na kisha kuchapishwa tokea 1957. �Wanafunzi wake walifanya majaribio kama hayo na kazi zao zikachapwa baadaye.

Nchini Tanzania • Hali ya Sanaa hii Tanzania –Uigaji wa zile za Uingereza –Vichekesho

Nchini Tanzania • Hali ya Sanaa hii Tanzania –Uigaji wa zile za Uingereza –Vichekesho –Udhati –Azimio –Baada ya Miaka ya 1970

Tanzania hadi miaka ya 1960 • Tangu 1922 zilikuwa zikiigizwa mashuleni • Mashindano ya

Tanzania hadi miaka ya 1960 • Tangu 1922 zilikuwa zikiigizwa mashuleni • Mashindano ya Maigizo tangu 1960 • 1967: Youth Drama association • 1968: Wakati Ukuta (E. Hussein) • 1970: Alikiona (E. Hussein)

Urithi wa Waingereza, Tz. �Kwa Tanzania: - Kazi za Shakepeare �Julius Ceasar, Macbeth, Merchants

Urithi wa Waingereza, Tz. �Kwa Tanzania: - Kazi za Shakepeare �Julius Ceasar, Macbeth, Merchants of Venice �Maana yake haikueleweka kwa Wa Tz. �Walioziigiza hawakuzielewa. Walizikariri tu. Waliona fahari kuzungumza na kuvaa kama Wahusika wa Kiingereza.

Kazi za Hyslop na Athari kwa Wanafunzi �Mgeni Karibu (G. Hyslop, 1957) �Afadhali Mchawi

Kazi za Hyslop na Athari kwa Wanafunzi �Mgeni Karibu (G. Hyslop, 1957) �Afadhali Mchawi (G. Hyslop, 1957) �Baadaye waandishi wengine wakaibuka na kuendelea kuandika: �Nakupenda, Lakini… (H. Kuria, 1961) �Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (G. Ngugi, 1972) �Mtawa Mweusi (Ngugi wa Thiong’o)

Maudhui ktk Tamthilia za Mwanzo • • • Vichekesho zaidi (Taz. Fasihi III, 1983)

Maudhui ktk Tamthilia za Mwanzo • • • Vichekesho zaidi (Taz. Fasihi III, 1983) Masuala ya rushwa katika jamii, urithi, Magendo ya dawa Vs. Uaminifu (fitina) Kumchagulia mtu mchumba Umaskini ktk ndoa Vs. Mapenzi ya kweli – Umri ktk Ndoa. (Mzee ana pesa, Kijana mapenzi) – Mapenzi ktk Ndoa: Wanandoa hutafuta nini?

Kabla ya Azimio (Hazikuchapishwa) • Vichekesho (Taz. Kiango ktk Kisw) – Kuwacheka washamba –

Kabla ya Azimio (Hazikuchapishwa) • Vichekesho (Taz. Kiango ktk Kisw) – Kuwacheka washamba – Kuwacheka wazungu weusi • Kufuata kampeni mbali (ujinga, maradhi, uvivu, n. k)

Baada ya Azimio hadi miaka ya 1970 • Wakati Ukuta (E. Hussein, 1968) •

Baada ya Azimio hadi miaka ya 1970 • Wakati Ukuta (E. Hussein, 1968) • Kinjektile (E. Hussein, 1969) • Tiba (Nkwera, 1969) • Mashetani (Hussein 1971) • Aliyeonja Pepo (F. Topan, 1970) • Hatia (P. Muhando, 1972) • Tambueni Haki Zetu (P. Muhando, 1973)

Athari za Azimio la Arusha • Umuhimu wa Azimio • Kulikuwa na hali gani

Athari za Azimio la Arusha • Umuhimu wa Azimio • Kulikuwa na hali gani • Watu walilitafsirije? • Azimio lilisema nini • Wanafasihi walilitafsirije?

Dhamira kutokana na Azimio la Ar �Tafuta Tamthilia za wakati huo �Kuondoa unyonyaji �Kuwabeza

Dhamira kutokana na Azimio la Ar �Tafuta Tamthilia za wakati huo �Kuondoa unyonyaji �Kuwabeza wasaliti �Kujenga Umoja �Kuhimiza ufanyaji kazi �Kila mara kumbuka yale yaliyotokea katika jamii. Fasihi ni zao la jamii katika kipindi maalumu cha historia

Miaka ya Ukombozi 1970 - 1980 �Ukombozi kutokana na nini �Sura mbali za ukombozi

Miaka ya Ukombozi 1970 - 1980 �Ukombozi kutokana na nini �Sura mbali za ukombozi �Ujinga (elimu), Usawa, Mila, Uhuru n. k �Tafuta tamthilia za kipindi hiki: �Mashetani, Damu Imemwagika, Tone la Mwisho, Dhamana mabatini, Mkwava wa Uhehe n. k

Tamthilia za Ebrahim Hussein • • Alikiona (1969) Kinjeketile (1969) Wakati Ukuta (1970) Mashetani

Tamthilia za Ebrahim Hussein • • Alikiona (1969) Kinjeketile (1969) Wakati Ukuta (1970) Mashetani (1971), Jogoo Kijijini na Ngao ya jadi (1976) Arusi (1980) Jambo la Maana (1982) Kwenye Ukingo wa Thim (1988)

Baadhi ya Tamthilia za Muhando �Hatia 1972 �Tambueni haki zetu, 1973 �Heshima yangu, 1974

Baadhi ya Tamthilia za Muhando �Hatia 1972 �Tambueni haki zetu, 1973 �Heshima yangu, 1974 �Pambo 1975 �Harakati za ukombozi 1982 �Nguzo mama 1982 �Abjadi yetu, 1983 �Lina ubani 1984

Baada ya 1980 • Je baada ya 1980 kuna mwelekeo maalumu unaoweza kuelezwa kuhusu

Baada ya 1980 • Je baada ya 1980 kuna mwelekeo maalumu unaoweza kuelezwa kuhusu tamthilia (fasihi) ya Kiswahili kama ilivyokuwa kwa miaka ya Uhuru, Azimio, Ukombozi? Ni maudhui ya aina moja? Kwanini? • Giza Limeingia, 1980 • Ayubu, 1984 • Ngoma ya Ng’wanamalundi (1999)

Baada ya Miaka ya 1980… • • • Kaptula la Marx, 1999 Ngome ya

Baada ya Miaka ya 1980… • • • Kaptula la Marx, 1999 Ngome ya Mianzi, 2000 Amezidi (1995) Nje Ndani (2017) Tafuta tamthilia nyingine na uangalie zinaeleza nini. Je unaweza kuziweka katika mkabala upi? Tetea uamuzi wako kwa hoja za kitaaluma

Tamthilia za Kiswahili Kenya Tazama kazi za hawa wafuatao: Ngugi wa Thiong’o Jay Kitsao

Tamthilia za Kiswahili Kenya Tazama kazi za hawa wafuatao: Ngugi wa Thiong’o Jay Kitsao Nyaigoti Chacha Kithaka wa Mberia n. k Tafuta tamthilia nyingine na uangalie zinaeleza nini. Je unaweza kuziweka katika mkabala upi? Tetea uamuzi wako kwa hoja za kitaaluma • Athari za utandawazi ktk tamthilia za Kiswahili kwa TZ na Ky ni zipi? • • •

5: 4. Fani na maudhui katika fasihi andishi • • MAUDHUI: Tumezungumzia Dhamira mbali.

5: 4. Fani na maudhui katika fasihi andishi • • MAUDHUI: Tumezungumzia Dhamira mbali. Ujumbe Migogoro Msimamo (anasimamia upande upi) Mtazamo (zuri/baya), dhanifu/yakinifu/dini Falsafa (Nini, kwanini na Kwa vipi)

Fani katika Fasihi Andishi • • • Muundo (mpangilio/mfuatano) Mtindo (tofauti za uandishi) Wahusika

Fani katika Fasihi Andishi • • • Muundo (mpangilio/mfuatano) Mtindo (tofauti za uandishi) Wahusika Mandhari Lugha (Tamathali, Methali, Taswira nk) Jina la Kitabu (Anwani)

Ujielezaji kwa namna mbali MAENDELEO YA KENYA 1900 MAENDELEO YA KENYA 2014

Ujielezaji kwa namna mbali MAENDELEO YA KENYA 1900 MAENDELEO YA KENYA 2014