KATI YA VINARA VYA TAA Somo la 2

  • Slides: 10
Download presentation
KATI YA VINARA VYA TAA Somo la 2 kwa ajili ya Januari 12, 2019

KATI YA VINARA VYA TAA Somo la 2 kwa ajili ya Januari 12, 2019

Ufunuo huanza kwa barua ya wazi kwenda kwa makanisa saba Asia ndogo (Uturuki). Mpangilio

Ufunuo huanza kwa barua ya wazi kwenda kwa makanisa saba Asia ndogo (Uturuki). Mpangilio wa makanisa ni sawa na ule ambao msambaza barua angeliutumia kusambaza barua. Yesu Kristo anatoa barua kwa Yohana. Kila kitu kwenye hii barua kina maalum, ikijumuisha muundo na ujumbe wake kwa kila kanisa. Bado una maalumu kwetu leo, takribani miaka 2000 tangu zitolewe. Pergamo BAHARI YA AEGEA Smirna Patmo Thiatira Sardi Filadelfia Efeso Laodikia Ufunuo wa Yesu Kristo kwa Yohana (Ufu. 1: 9 -18) Wapi: Patmo (1: 9) Lini: Katika siku ya Bwana (1: 10) Vipi: Kama Kuhani mkuu (1: 12 -18) Barua kwa makanisa Saba (Ufu. 1: 11, 19 -20; 2: 1 -7) Jinsi ya kutafsiri (1: 11, 19 -20) Ujumbe kwa waefeso (2: 1 -7)

“Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na

“Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. ”(Ufunuo 1: 9) Nini kilikuwepo Patmo ? • Patmo ni kisiwa kilichofungwa (10 x 6 mi— 16 x 10 km). Warumi walianzisha sehemu ya adhabu hapo. Kwa nini Yohana alikuwa hapo? • Alituhumiwa kwa uzushi wa kuhubiri habari za Yesu Kristo alipokuwa mzee. Mfalme wa Rumi Domitian akamfunga pale kati ya 81 na 96 Baada ya Kristo) Yesu alifanya nini kwa ajili ya Yohana ? • Yesu alimletea maneno ya matumaini na ya kutia moyo, kama alivyofanya kwa wale vijana wadogo kwenye tanuru la moto na kwa Stefano alipokuwa akiuwawa. Tunaweza kuwa na uhakika kuwa Yesu atakuwa nasi daima tunapopitia mateso ili tuwe mashahidi waamini.

SIKU YA BWANA “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu,

SIKU YA BWANA “Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu. ” (Ufunuo 1: 10) Je; Tutafsiri vipi“Siku ya Bwana”? Jumapili • “Siku ya Bwana” ilitumika kuashiria Jumapili mara ya kwanza katika karne ya pili. Haimaanishi “Jumapili” katika wakati wa Yohana. Kuja kwa Yesu mara ya pili • Hii ingemaanisha kuwa Yohana alikuwa tayari akipokea maono ya kuja kwa Yesu mara ya pili wakati anapokea ufunuo huu mpya (Is. 13: 6; 2 P. 3: 10). Dhana hii haiungwi mkono na aya za Ufunuo. Sabato • Katika agano la Kale, Mungu (Bwana) aliita sabato“yake”, Hivyo ni siku yake (|Kut. 31: 13; Is. 58: 13). Yesu pia anjiita“Bwana wa Sabato” (Mt. 12: 8; Mr. 2: 28 Hivyo Yohana alipokea Ufunuo katika siku ya Sabato, Siku ya Bwana.

“Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu

“Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho. ’”(Ufunuo 1: 17) Mwonekano wa nje wa Yesu ulikuwaje katika Ufunuo 1? Ufunuo 1: 13 -16 Danieli 10: 5 -6 Vazi refu mshipi wa dhahabu Nywele nyeupe nguo za kitani mshipi wa dhahabu --- Macho ya moto Nyayo za shaba Sauti ya maelfu Upanga kinywani --- Uso kama jua Uso kama umeme Mtu aliyevaa kwa namna aliyoiona Yohana na Danieli ni Yesu aliyevalia kama Kuhani mkuu.

UFUNUO WA YESU KRISTO “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono

UFUNUO WA YESU KRISTO “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho. ’”(Ufunuo 1: 17) Yohana alimuona Yesu akitembea kati ya vinara saba vya taa ambavyo ni ishara ya makanisa saba (1: 20) Ujumbe kwa kila kanisa unaanza na “Nayajua matendo yako. ” (2: 2, 9, 13, 19; 3: 1, 8, 15). Yesu daima yu kati ya watu wake. Anawajua watu wake na anamjua kila mmoja wetu. Ni mkuu na mwingi wa utukufu, lakini hatupaswi kuuogopa uwepo wake. Ndiye aliyekufa na kufufuka. Anao ufunguo wa mauti. Ana nguvu dhidi ya mauti na awajali walio hai.

BARUA KWA MAKANISA SABA “ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa

BARUA KWA MAKANISA SABA “ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia. ”(Ufunuo 1: 11) Ujumbe kwa makanisa saba huko Asia unaweza kutafsiriwa katika ngazi tatu tofauti zinazokamilishana (1: 19): WAKATI HUSIKA (KIHISTORIA) Ujumbe wa Yesu kwa kila kanisa linalo kutana katika miji saba katika Asia ndogo wakati wa Yohana. WAKATI UJAO (KIUNABII) Ujumbe kwa wakati wa kihistoria wa kanisa tangu wakati wa Yohana hadi wakati. YA JUMLA Ujumbe kwa kila kanisa na muumini katika kila wakati historia.

UJUMBE KWA KANISA LA WAEFESO “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo

UJUMBE KWA KANISA LA WAEFESO “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye kati ya vile vinara saba vya dhahabu: ’” (Ufunuo 2: 1) Efeso ulikuwa mji muhimu sana katika Asia. Yohana alikuwa mchungaji katika mji huo uliojaa ukosefu wa maadili na uchawi (Matendo 19: 19) Kanisa lilisimama imara katika hali hiyo yenye changamoto. Hata hivyo, walisahau upendo wa kwanza kama walivyofanya Israeli wa zamani (Yeremia 2: 2) Kanisa hili huwakilisha kanisa la kikristo la karne ya kwanza (inakisiwa. kuanzia 31 hadi 100 baada ya Kristo) Hebu tuufuate ushauri wa kimbingu ili tu tunze wema wao na kuepuka makosa yao : (1) Kumbuka upendo wako wa kwanza; (2) Tubu; (3) na utende matendo mema.

“Yeye [Yesu] hutembea kati ya makanisa yake katika urefu na upana wa dunia. Anawatazama

“Yeye [Yesu] hutembea kati ya makanisa yake katika urefu na upana wa dunia. Anawatazama kwa matarajio makubwa kuona kama wako katika hali ya kiroho ambayo wanaweza kuueneza ufalme wake. Kristo yuko katika kila kusanyiko la kanisa. Anamjua kila aliyeunganishwa na huduma yake. Anawajua wale ambao mioyo yao inaweza kujazwa na mafuta ya Roho mtakatifu, ili waweze kuwaambukiza wengine. Wale ambao kwa uaminifu hubeba kazi ya Kristo kwa ulimwengu, wakiiwakilisha tabia ya Mungu katika maneno na matendo, wakikamilisha kusudi la Bwana kwa ajili yao, machoni pake ni wa thamani sana. Kristo anawafurahia kama vile mtu afurahiavyo bustani iliyotunzwa vyema na harufu nzuri ya maua aliyoyapanda. ” E. G. W. (Testimonies for the Church, vol. 6, cp. 53, p. 418)