FUNGUO ZA UMOJA WA FAMILIA Somo la 7

  • Slides: 8
Download presentation
FUNGUO ZA UMOJA WA FAMILIA Somo la 7 kwa ajili ya Mei 18, 2019

FUNGUO ZA UMOJA WA FAMILIA Somo la 7 kwa ajili ya Mei 18, 2019

Kudumisha umoja katika familia kunahitaji juhudi za kila mwanafamilia. Familia itakuwa na umoja imara

Kudumisha umoja katika familia kunahitaji juhudi za kila mwanafamilia. Familia itakuwa na umoja imara kama kila mwanafamilia atakuwa na funguo zifuatazo: Yesu Upendo Unyenyekevu Kujishusha Kujitoa

YESU “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu

YESU “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. ” (Wagalatia 3: 28) Kuishi katika Kristo huleta mabadiliko ya kimwili katika maisha yetu (Warumi 6: 22; 2 Wakorintho 5: 17). Msalaba wa Kristo huondoa mipaka yote inayotenga watu. Kwa kadri tunavyoishi karibu na Yesu, ndivyo tunavyokuwa karibu na wengine. Hii ni kweli pia kwa ngazi ya familia. Yesu anapokuwa kiini cha kila moyo wa mwanafamilia, kuna kuwa umoja kati ya mume na mke, kati ya wazazi na Watoto, kati ya kaka na dada…

UPENDO “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa

UPENDO “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. ” (1 Yohana 4: 7) Neno la kiyunani ágape linatumika katika agano la jipya kwa ajili ya upendo wa Mungu na upendo tunaopaswa kuonesha. Aina hii ya upendo ni Zaidi ya upendo wa kimili. Ni kipawa cha Roho Mtakatifu. (Warumi 5: 5). ____ • Huvumilia na hufadhili Hebu linganisha tabia yako na maana ya ____ • hauhusudu upendo wa ágape katika 1 Wakorintho ____ • hautakabari 13: 4 -7. Je; Ni mabadiliko gani unaweza ____ • haujivuni kufanya maishani? ____ • haukosi kuwa na adabu Andika jina ____ • hautafuti mambo yake lako ____ • hauoni uchungu pembeni ya ____ • hauhesabu mabaya sentensi zinazofanana na ukweli maishani mwako leo: ____ ____ • haufurahii udhalimu • bali hufurahi a kweli • huvumilia yote • huamini yote • hutumaini yote • hustahimili yote

UNYENYEKEVU “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila

UNYENYEKEVU “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. ” (Philippians 2: 3) Kwa sababu ya Dhambi, ubinafsi umekuwa sehemu inayorithiwa ya ubinadamu. “Kama majivuno na ubinafsi vingewekwa kando, dakika tano zingeondoa hata yaliyo magumu zaidi. ” (Ellen G. White, Early Writings, p. 119) Paulo anatuhimiza kuiga mfano wa unyenyekevu wa Kristo (fg. 4 -8). Tunaweza kuufikia unyenyekevu wa kweli tu kama tutapiga magoti miguuni pa msalaba.

KUJISHUSHA “hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. ” (Waefeso 5: 21) Wale wanaompenda Mungu

KUJISHUSHA “hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. ” (Waefeso 5: 21) Wale wanaompenda Mungu wameitwa kujishusha kila mmoja kwa mwenzake. Paulo anatoa mifano mitatu ya kujishusha: Wake wajishushe kwa waume zao • Waefeso 5: 22 Watoto wajishushe kwa wazazi wao • Waefeso 6: 1 Watumwa wajishushe kwa Mabwana zao • Waefeso 6: 5 Mambo haya tayari yalikuwa yakitegemewa katika jamii. sasa, kwa nini ushauri wa Paulo uwe mpya? Tunawezaje kuubeba katika jamii yetu leo? Kwanza, kujishusha katika Kristo kuna pande mbili. Pili, kuna masharti katika mifano ya awali ya kujishusha: Waume wajishushe kwa Kristo • Waefeso 5: 25 -33 Wazazi wasiwachokoze watoto • Waefeso 6: 4 Mabwana wasiogofye • Waefeso 6: 9

KUJITOA “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,

KUJITOA “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. ” (Mwanzo 2: 24) Kila familianza kwa kujitoa. Kujitoa huku huenea kwa familia yote: Kujitoa katika viapo vya Ndoa Kujitoa kwa kaka na dada Kujitoa miongoni mwa Watoto na wazazi Kujitoa kwa ndugu Kukosa kujitoa husababisha matatizo na mgawanyiko (Tazama kisa na Yusufu na ndugu zake). Kujitoa kuliko imara hujenga muunganiko wa familia ulio imara na wakudumu (Tazama

“Sababu ya mgawanyiko na kutofautiana katika familia na kanisa ni kujitenga na Kristo. Kuja

“Sababu ya mgawanyiko na kutofautiana katika familia na kanisa ni kujitenga na Kristo. Kuja karibu na Kristo ni kukaribiana mmoja kwa mwenzake. Siri ya umoja wa kweli katika kanisa na katika familia siyo diplomasia, si usimamizi, si jitihada za kibinadamu za kushinda matatizo ingawa kutakuwa na mengi ya kufanya – bali ni muungano na Kristo. ” E. G. W. (The Adventist Home, cp. 27, p. 179)