NGUVU YA MAOMBI KUWAOMBEA WENGINE Somo la 4
NGUVU YA MAOMBI: KUWAOMBEA WENGINE Somo la 4 kwa ajili ya Julai 25, 2020
Neno la Mungu linatuhimiza “kuomba bila kukoma” (1 Wathethalonike 5: 17). Katika maelezo ya Paulo juu ya silaha za Mkristo, alisema kwamba tunapaswa “kudumu katika kuomba, ” na akawaomba Waefeso kuomba kwa jaili yake (Waefeso 6: 18 -19). Maombi yana nguvu hasa yanapotumika kuwapatanisha wengine, wawe waumini au sio waumini. Maombi ya upatanisho: Kuomba kati ya pambano Kuomba kwa ajili ya watu maalumu Kuombea waumini wengine Mungu husikia maombi yetu Jinsi ya kuomba
KUOMBA KATI YA PAMBANO “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. ” (Waefeso 6: 12) Tunaishi kwenye pambano kati ya ulimwengu unaoonekana na ulimwengu usioonekana. Pambano kati ya wema na uovu, kati ya Kristo na Shetani. Kila mmoja wetu anatumikia upande mmoja, na watu wengi wanazidi kupungua. Hakuna “huduma ya kijeshi ya lazima” katika upande wa Kristo. Hamlazimishi ye yote kumfuata. Haingilii kati kama hatujamruhusu. Maombi ya upatanisho ni njia ya “kumruhusu” Mungu kuingilia kati kwa Maisha ya watu tunaowaombea. Mungu huheshimu uchaguzi wetu wa kuwaombea na hufanya kazi kwa nguvu Zaidi kwa niaba yao.
KUOMBA KWA AJILI YA WATU MAALUMU “Akasema, ‘Simoni, Simoni! Tazama Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano. Lakini nimekuombea wewe ili Imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. ’” (Luka 22: 31 -32) Yesu alikuwa mtu wa Maombi wakati akiishi hapa duniani. Kadri pambano lilipvyokuwa gumu, ndivyo alivyojitoa zaidi kwa maombi. Hakuegemea katika nguvu zake mwenyewe kuyashinda majeshi ya mwovu. Daima alitegemea nguvu za Mwenye nguvu kupitia maombi. Aliacha mfano wa kuomba kwa ajili ya watu maalumu, kama alivyofanya kwa Petro. Yesu alijua kwamba Petro hakujua kama alikuwa anahitaji msaada usiku ule. Kwahiyo, Yesu aliomba kwa niaba yake. Mungu anatutia moyo kupeleka watu maalumu mbele ya kiti Chake cha enzi na kuwaacha mikononi Mwake. Ni lazima tudumu mpaka tuone matokeo. Kumbuka kuwa Yesu pia anaomnba kwa ajili ya kila mmoja wetu
KUWAOMBEA WAUMINI WENGINE “Siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu: ” (Waefeso 1: 16) Paulo alikuwa akiomba kwa ajili ya waumini wengine. Ni kipi alichokiuliza? Tazama Waefeso 1: 17 -23. Kwama Mungu awapatie hekima (aya. 17) Kwamba wamjue Mungu vyema (aya. 17) Kwamba wajue tumaini la mwito Wake (aya. 18) Kwamba wajue utukufu wa urithi ujao (aya. 18) Kwamba wajue nguvu ya Mungu (aya. 19 -23) Paulo pia alikuwa akishukuru ukuaji wa kiroho wa ndugu na dada zake, kama ilivyo katika ombi lake kwa Wafilipi 1: 3 -11. aliwaombea kuzidi kuendelea katika imani. Inatupasa kuwaombea ndugu na dada zetu kama Paulo alivyofanya, ili waimarishwe na kutiwa moyo katika safari yao ya Kikristo.
MUNGU HUSIKIA MAOMBI YETU “Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. ’” (Daniel 10: 12) Danieli alikuwa na hofu juu ya hali ya wale waliorudi kutoka Babeli hadi Yerusalemu. Danieli alikuwa ameshituka na akawaombea kwa siku 21. Inaonekana kwamba maombi yake hayakujibiwa baada ya siku nyingi. Hali ilikuwa haibadiliki hata kidogo. Mungu alituma njozi kwa nabii mwenye huzuni kwa wakati mwafaka. Alimhakikishia Danieli kwamba maombi yake yamesikiwa tangu siku ya kwanza. Mungu amekuwa akifanyia kazi mambo mengine ya pambano kabla ya kujibu ombi la Danieli. Anasikiliza kila ombi la kusihi, japokuwa inatupasa
JINSI YA KUOMBA Maombezi yetu lazima yawe ya bidi, ya dhati na maalumu. “Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka” (1 Samweli 12: 23) Paulo aliwaombea watu maalumu (k. m. washirika wake) na makanisa maalumu (k. m. Efeso au Filipi). Aliliomba kanisa pia kuomba kwa ajili ya uhuru wake au kwa ajili ya kuhubiri kwake ili kuimarishwa (Flp. 1: 19; Kol. 4: 3). Tunapaswa kuomba kwa ajili ya wale tunaowajua kuwa hawajakutana bado na Mwokozi (Yn. 17: 20), kwa ajili ya waumini kuimarishwa (Ef. 3: 14 -16), kwa ajili ya Mungu kupanua msamaha wake (1 Yn. 5: 16), kwa ajili ya ulinzi wa wale wanaopitia wakati mgumu (Matendo 12: 12)… Tunapowaombea wengine, tunakuwa mfereji wa mibaraka ya Mungu kwao.
“Kuombea kunamanisha nini? Ni mnyororo wa dhahabu unaomfunga mwanadamu mwenye ukomo kwenye kiti cha enzi cha Mungu asiye na ukomo. Wakala wa kibinadamu ambaye Kristo amemfia ili kumwokoa na kumwingiza katika kiti cha enzi cha Mungu, na haja yake inachukuliwa juu na Kristo aliyemnunua kwa damu Yake mwenyewe. Kuhani wetu Mkuu anaweka haki Yake katika upande wa maombi ya dhati, na maombi ya Kristo huchanganywa na yale ya mwombaji wa kibinadamu. ” E. G. W. (That I May Know Him, March 13)
“Anza kuomba kwa jili ya roho; mkaribie Kristo, karibu na upande Wake unaovuja damu. Hebu upole na roho ya utulivu inayopamba maisha yako, na hebu maombi yako ya dhati, ya kuvunjika moyo, na ya unyenyekevu yapande Kwake kwa hekima kwamba ili upate kufanikiwa katika kuokoa siyo roho yako tu, lakini roho za wengine pia. ” E. G. W. (Testimonies for the Church, book 1, cp. 86, p. 513)
- Slides: 9