Uchumi Binafsi Katika Kutumia kwa Ajili ya Mafanikio
Uchumi Binafsi: Katika Kutumia kwa Ajili ya Mafanikio ya Dunia na Akhera Kwa Mtazamo wa Qur’an na Sunna
Utangulizi • Katika Bukhari, Mtume rehema na amani zimfikie anasema, “Mwanamke anakuambia, nihudumie nipe matumizi, kama huwezi kunihudumia na kunitunza niache; na mtumwa/ mtumishi naye anakuambia nipe huduma na unitumie; na mwanao naye anakuambia nihudumie unanitelekeza kwa nani? ” • “Na atoe mwenye wasaa kwa kadiri ya wasaa wake. Talaq: 6) 3
Matumizi (Nafaqa) • Maana ya neno ‘Nafaqa’: • Linatokana na neno Infaq. Asili yake lina maana ya utoaji, na utoaji huu haufanyiki ila katika mambo ya kheri na mazuri tu. • Kisheria ni Kuwasimamia wanaokutegemea kwa njia nzuri – chakula chao, mavazi yao, elimu yao, afya yao na makazi yao na vinavyoendana na hivyo. 4
Matumizi (Nafaqa) • Maana nyingine ya Nafaqa. Nacho ni kiasi kinachotosheleza wale anao wahudumia kuanzia chakula, vinywaji, mavazi, makazi na ulinzi. • Vitu vitano hivi hukumu yake ni wajibu. Lakini vyote hivi lazima viwe na masharti. 5
Masharti ya utoaji • 1) Ukwasi wa mtoaji; • 2) Kuhitaji kwa anayepewa. • 3) Kuafikiana Dini isipokuwa kwa mke. • 4) Awe mtoaji mrithi kwa yule anayemhudumia. - kurithi kwa faradhi au udugu. 6
Masharti ya utoaji • Wanaona baadhi ya wanachuoni ni wajibu kwa ndugu kutoa huduma kijumla kutokana na dalili zenye kuonesha umuhimu wa kuunga udugu. Israa 26, “wapeni ndugu wa karibu haki zao, masikini, na mpita njia. ” Na Mtume kaamrisha kuunga udugu na katoa onyo dhidi ya kukata udugu. Si katika kuunga udugu mtu kuwa tajiri, anakula anachokitaka, anavaa anachokitaka, na anaishi anakokutaka yeye na ndugu zake wanakufa na njaa. 7
Masharti ya utoaji • Sharti la kwanza: • Yule anayepewa, awe hawezi kumiliki kwa kuwa ni mtu fukara na hawezi kuchuma. • Iwapo atakuwa ni mkwasi, analazimika kuchuma mwenyewe, hastahiki kuchumiwa kwa sababu yeye mwenyewe anaweza kuchuma. Na mtu anayejitosheleza mwenyewe Allah Atamtosheleza. 8
Masharti ya utoaji • Sharti la pili: • Kujitosheleza kwa mtoaji au ukwasi wa mtoaji. • Yule anayetoa awe anajitosheleza. Kama ni fukara halazimiki kutoa. • Je analazimika kuchuma ili aje atoe? Jibu, halazimiki. Kama vile ambavyo halazimiki kutafuta mali ili aje kutoa Zaka. • Kwa nini: Kwa sababu lile ambalo wajibu hautimu ila kwasipokuwa kwalo nalo linakuwa ni wajibu. Na lile ambalo wajibu hutimu isipokuwa kwalo si wajibu. 9
Masharti ya utoaji • Sharti la tatu: • Kuwiana au kuafikiana dini kati ya mtoaji na mpokeaji. Kama dini zao tofauti hakuna wajibu wa kutoa. Kama ambavyo hawarithiani. Ushahidi wa urathi ni hadithi ya Mtume: “Muislamu hamrithi kafiri wala Kafiri hamrithi Muislamu. ” 10
Masharti ya utoaji • Sharti la nne: • Awe yule anayetoa huduma ni mrithi kwa anayemhudumia. Tena urithi wenyewe uwe wa faradhi au udugu. Au kwa msonge wa nasaba. Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu, Baqarah 233, “Ni kwa mrithi mfano wa hivyo. ” Nao ni wazazi na watoto. 11
Masharti ya utoaji • Lakini sharti linataka aafikiane na yeye katika dini. Iwapo tofauti hii ipo kwa upande wa wazazi na watoto. Kuhusu wazazi Luqmani 15, “wakikuteza nguvu kunishirikisha mimi katika jambo usilokuwa nalo elimu, usiwatii, lakini ishi nao kwa wema. ” • Inaweza kusemwa kuwa anaishi na wazee wake kwa wema kwa kulazimika kuwahudumia. Yaani atakuwa akiwapa kile anachoweza. 12
Aina za Matumizi: • Matumizi ya mtu kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe (Nafaqatul insan ‘ala nafsihi) • Matumizi ya wazazi kwa ajili ya watoto wao (Nafaqatul Furu’i ‘alal uswul). • Matumizi ya Watoto kwa ajili ya wazazi wao (Nafaqatul Uswul ‘alal Furu’i) 13
Aina za Matumizi: • Matumizi ya Mume kwa mke (Nafaqatu Zzawjatu ‘ala Zzawj). • Matumizi ya Mmiliki kwa wafanyakazi wake (Nafaqatu al-Mama-liyk) • Matumizi ya Mtu na wanyama wake (Nafaqatul al-Baha-im) 14
Matumizi ya mtu kwa ajili ya nafsi yake (Nafaqatul insan ‘ala nafsihi) • Ni wajibu kwa mtu kuanza kujihudumia mwenyewe kama ana uwezo. • Kwa hadithi ya Jabir, Radhi za Allah Zimfikie, amesema, Mtume, Rehema na Amani Zimfikie, amesema, “(Katika matumizi) Ianze na nafsi yako – toa matumizi kwa ajili yake, kitakachozidi – tumia kwa ajili ya familia yako, kitakachozidi baada ya kutumia kwa ajili ya familia yako – tumia kwa ndugu zako wa karibu (nasaba). ” (Imepokewa na Muslim 997) 15
16
• Halikadhalika, Mtume Rehema na Amani zimfikie alimuona mtu nywele zake zimetimka na kuparaganyika, akasema, “Je mtu huyu hakupata cha kuchana nywele zake? ” Na safari nyingine alimuona mtu kavaa nguo chafu, akasema, “Je hakupata mtu huyu cha kufulia nguo zake? ” Abu Daud • Aidha alikuja mtu kwa Mtume Rehema na Amani Zimfikie ilihali amevaa nguo mbovu. Akamuuliza, “Je una mali ya aina gani? ” Naye alimjibu, “Kila aina ya mali, Mwenyezi Mungu Kanipa. ” Mtume akamwambia, “Basi Mwenyezi Mungu Akikupa mali hupenda aone athari ya neema yake na ukarimu wake kwako. ” Nasai
18
• Na hapana ubaya kwa Muislamu kupenda mazuri nyumbani mwake au katika nguo zake au viatu vyake au katika vyengine vyake, kwani Mtume, Rehema na Amani zimfikie amesema, “Hatoingia peponi mtu ambaye moyoni mwake mna chembe ya kiburi. ” Mtu mmoja akasema, “Mtu hupenda nguo zake ziwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri. ” Mtume akajibu Mwenyezi Mungu ni Mzuri Anapenda uzuri. ” Muslim.
• Katika riwaya nyingine imesimuliwa kuwa mtu mzuri wa sura alimjia Mtume Rehema na Amani zimfikie akamuuliza; “Mimi ninapenda uzuri, nami nimepewa vya kutosha kama unionavyo hata imekuwa sipendi mtu anipiku kwa uzuri wa nyuzi za viatu kuliko zangu. Je ni katika kiburi haya, “Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu? ” Mtume akajibu, “La, bali kiburi ni kuikataa haki na kuwadharau watu. ” Abu Daud 20
Matumizi ya wazazi kwa ajili ya watoto wao (Nafaqatul Furu’i ‘ala uswul)-1. • Ni wajibu kwa mzazi na wazazi wake kutoa matumizi kwa ajili ya watoto wake au wajukuu wao, Baqara 233; • “…na watoto ni wajibu kulishwa na kuvishwa kwa wema. ’ 21
Matumizi ya wazazi kwa ajili ya watoto wao (Nafaqatul Furu’i ‘ala uswul)-2. • Wajibu kwa Mzazi kutoa malipo kwa ajili ya kunyonyeshwa watoto wake. Kwa hadithi iliyotoka kwa Bi Aisha Radhi za Allah zimfikie, amesema kuwa Hind bin ‘Utbah amesema, “Ewe Mtume wa Allah, hakika Aba Sufyan ni mtu bakhili, na hanipi kinachonitosheleza mimi na mwanangu katika matumizi, ila kwa kile ninachokichukua bila ya yeye kujua. Mtume akamwambia, “Chukua kinachokutosheleza weye na mwanao kwa njia ya wema. ” Bukhari 2221 na Muslim 1714 22
• Mlango wa fadhila za kuhudumia watoto wako na unao wamiliki na dhambi ya anayewatelekeza au akawazuilia huduma. Kutoka kwa Abi Qilabah kutoka kwa Abi Asmaa, kutoka kwa Thawban amesema, amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie, “Shilingi bora zaidi aitoayo mtu ni ile shilingi aitoayo kwa wanawe, na shilingi aitoayo mtu kwa ajili ya kipando chake kwenye njia ya Allah, na shilingi aitoayo kwa wenzake, rafiki zake, katika njia ya Allah. ” Abu Qilabah amesema, ‘ameanza kutaja watoto. ’ na hakuna mtu mwenye ujira mkubwa zaidi kuliko mtu anayetoa huduma kuhudumia watoto wake wadogo, anawahifadhi, analinda heshima yao, au anamtarajia Allah Ampe manufaa kwa kupitia watoto wake. Na Awape utajiri. (Sahih Muslim) 23
Kutoka kwa Abi Huraira, Radhi za Allah zimfikie, amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie, “Shilingi unayoitoa katika njia ya Allah, na shilingi unayoitoa katika kumkomboa mtumwa, na shilingi unayoitoa katika kumsaidia maskini, na shilingi unayotoa kwa ajili ya familia yako, mkeo na wanao, yenye ujira mkubwa zaidi ni ile uliyoitoa kwa ajili ya familia yako. ” Sahih Muslim • Kutoka kwa Aby Mas’udi al-Badriyyi kutoka kwa Mtume Rehema na Amani zimfikie, ‘Muislamu akitoa huduma kwa familia yake, naye akitaraji radhi za Allah, inakuwa kwake yeye ni sadaka. ” Sahih Muslim, Bukhari, Tirmidhy Nasai 24
• Na Mtume alisema kuwaambia watu katika Hija yake ya kuaga, “walahunna alaykum rizkuhunna wakiswatuhunna bil ma’aruf” • “Nyinyi mna wajibu kwa wake zenu wa kuwalisha na kuwavisha kwa wema. ” 25
Matumizi ya watoto kwa ajili ya wazazi wao (Nafaqatul Uswul ‘alal Furu’i -1 • Ni wajibu kwa watoto kutoa matumizi kwa ajili ya wazazi wao. Kwa kauli ya Muumba, Luqman: 15; “Na uishi nao hapa duniani kwa wema. ” Israi: 23, “…na Tumewausia kuwafanyia wema wazazi wawili. ” • Na katika ihsani ni kuwahudumia wazazi wawili. Bali hili la kuwahudumia wazazi ni ihsani kubwa zaidi. 26
Matumizi ya watoto kwa ajili ya wazazi wao (Nafaqatul Uswul ‘alal Furu’i -2 • Na katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bi Aisha Radhi za Allah Zimfikie, amesema Mjumbe wa Allah rehema na amani zimfikie, “Katika chakula kizuri mno ni kile anachokula mtu kutokana na chumo lake mwenyewe, na mwanawe ni katika chumo lake. ” imepokewa na Tirmidhy 1358; Abu Daud 3568, Nasai 7: 241; Ibn Majah 2137. Sahihi albani: 4144. 27
Matumizi ya watoto kwa ajili ya wazazi wao (Nafaqatul Uswul ‘alal Furu’i -2 • Na hadithi ya Amri ibn ‘As, Allah Amuie radhi amesema: kuwa Mtume Rehema na Amani Zimfikie, amesema, “Wewe na mali yako ni mali ya Wazazi wako; hakika watoto wenu ni katika machumo yenu mazuri, kuleni katika machumo ya watoto wenu. ” Abu Daud 3530; Sahihi albani, al-Irwaa, 838. 28
Matumizi ya Mume kwa mke (Nafaqatu Zzawjatu ‘ala Zzawj) • Ni wajibu mtu kumhudumia mkewe. Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu, Nasai 34; “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kuwafadhilisha baadhi yao juu ya wengine, na kwa sababu ya vile wanavyovitoa kutoka katika mali zao. ’. Na hadithi ya Jabir, Radhi za Allah zimfikie, ambayo ndani yake kuna maneno ya Mtume Rehema na Amani Zimfikie amesema, “Nyinyi mna wajibu kwa wake zenu kuwahudumia na kuwavisha, kwa wema. ” Muslim 1218. 29
Matumizi ya Mume kwa mke (Nafaqatu Zzawjatu ‘ala Zzawj) • Na kwa mujibu wa hadithi zilizotangulia ya Jabir “Kikizidi kitu ni kwa ajili ya familia yako. ” na ya Aisha. Ni wajibu kwa Mume kutoa matumizi ya chakula, matumizi ya pango la nyumba, na matumizi ya mavazi kulingana na mahitaji ya mke na hadhi yake. 30
• Mume analazimika kumpa huduma ya chakula mkewe, makazi, na mavazi yanayolingana naye, na yanayolingana na hadhi yake. Na matumizi haya yanalazimu kwa mke aliye katika mamlaka yako, na hali kadhalika aliyeachwa talaka rejea, muda kuwa bado yupo kwenye eda. Ama aliyeachwa talaka tatu, hasitahiki kupewa huduma wala makazi. Isipokuwa kama atakuwa mjamzito, anastahiki kuhudumiwa. Mwenyezi Mungu Anasema, Talaqa: 6, “Wakiwa ni wanawake wajawazito, wahudumieni mpaka wajifungue. ” 31
Matumizi kwa ajili ya Wafanyakazi (Nafaqatul Mama-liyk) • Hukumu ya matumizi ya wafanyakazi; Ni wajibu kwa Bwana kuwahudumia kwa wema wafanyakazi wake, Chakula, mavazi, na sehemu ya kuishi. “Tunajua majukumu Tuliyowafaradhia kwa wake zao, na wale wanaomilikiwa na mikono ya kiume. ” (Ahzab: 5) 32
• Na kauli ya Mtume rehema na amani zimfikie, “Kwa mwenye kumilikiwa ana haki ya chakula na mavazi. ” Muslim 1662 • Na ni wajibu kuwa mpole kwao na kutowapa shughuli zinazozidi uwezo wao. Kwa kauli ya Mtume Rehema na Amani zimfikie, “Wala msiwakalifishe kwa kuwapa kazi nzito kuliko uwezo wao, na mnapowapa kazi ngumu basi muwasaidie kuzifanya. ” Muslim, 1661. 33
Matumizi kwa ajili ya Wanyama (Nafaqatil Baha-im) • Ni wajibu kwa anayemiliki wanyama awalishe na awape maji na kusimamia mahitaji yao na kuwachunga inavyotakikana. Kwa kauli ya Mtume Rehema na Amani zimfikie, “Mwanamke aliingia motoni kwa sababu ya paka alimzuia, alimfungia, wala hakumpa chakula, wala hakumuacha ajitafutie vijidudu vya ardhini. ” Muslim, kutoka kwa Abu Huraira. 34
Matumizi kwa ajili ya Wanyama (nafaqatil Baha-im) • Hadithi hii inazungumzia uwajibu wa kuwa na matumizi mpaka kwa wanyama anaowamiliki mtu. Kuingia kwa mwanamke huyu motoni ni kwa sababu ameacha kumuangalia kimatumizi paka, na ni hivyo kwa wanyama wengine wenye kumilikiwa. • Mmiliki wa mnyama akishindwa kumhudumia mnyama atalazimishwa amuuze au amkodishe au amchinje ikiwa ni katika wanaoliwa. Kwa sababu kuendelea na kubaki nae na kushindwa kumhudumia ni udhalimu. Na dhuluma inawajibika kuiondosha. 35
Mpango wa matumizi – Njia nyepesi ya kutumia fedha. • Kutumia na kuweka akiba ni vitu viwili vyenye kuingiliana. • Mtu kudhibiti matumizi yake ya kila siku kunamuwezesha kuweka akiba. • Na kuweka akiba kunamuwezesha mtu kutumia, hasa katika vitu vyenye bei kubwa. 36
Mpango wa matumizi – Njia nyepesi ya kutumia fedha. • Maana ya ‘Nafaqa' ni, ‘Kutumia fedha kwa werevu, fedha zilizotengwa kwa ajili ya kujikimu na mahitaji ya maisha ya kila siku. ” • Hakuna mwisho katika matumizi. Pale matumizi yanapokuwa hayadhibitiwi yatakuwa ni yenye kuathiri maeneo yote ya mtu ya maisha yake ya kila siku, hasa ya kifedha. • Njia nyepesi ya kutumia fedha iliyo nzuri ni kujua na kuwa hadhiri na matumizi yako. Na hili linawezekana kwa makusudi kwa kutengeneza Bajeti binafsi – au mpango wa matumizi. 37
Upangaji wa Bajeti kwa ajili ya matumizi ya Familia. • Zipo hatua mbili kuu ambazo ni lazima zipitiwe katika upangaji wa matumizi ya familia. • Hatua ya kwanza: • Ni kujua vyanzo vya kipato cha familia, kama ni kazi ni nani anayefanya kazi, mume au mke? Kama ni biashara, ajira rasmi na kilimo ni vivyo hivyo. 38
Upangaji wa Bajeti kwa ajili ya matumizi ya Familia. • Hatua hii itakuwezesha kujua kipato halisi kwa mwezi au mwaka. Ukisha kujua kipato cha familia kwa mwezi/mwaka, hatua ya pili inafuatia. • Kiislamu mwanamke halazimiki kuchangia kipato chake katika kuendesha maisha ya familia. Jukumu hilo kidini ni la mwanamume. Mwanamke akichangia, kwake inakuwa ni sadaka njema. 39
Upangaji wa Bajeti kwa ajili ya matumizi ya Familia. • Hatua ya Pili: • Orodhesha mahitaji ya familia ukizingatia mahitaji muhimu kwanza: • kama vile, chakula, kodi ya nyumba, ada na matumizi mengine muhimu kwa watoto wanaosoma kama wapo. 40
Upangaji wa Bajeti kwa ajili ya matumizi ya Familia. • Katika kodi ya nyumba ingiza malipo ya umeme na maji kama yapo. • Mahitaji mengine muhimu ya kifamilia ni kama: - madeni, matibabu, mavazi, sadaka na Akiba. 41
Matumizi yasiyo ya lazima • Matumizi yasiyo ya lazima sana, ni yale yanayotengwa kwa ajili ya burudani kama vile kwenda fun-city, Dar es salaam zoo, kutoa zawadi, michango ya hiari na kadhalika. • Matumizi haya kwa kiwango kikubwa hutegemea na kipato cha familia husika. 42
Matumizi yasiyo ya lazima • Ni rahisi kushughulikia mahitaji muhimu, kama kiasi cha pesa kwa kila hitaji kinajulikana, kama vile kodi ya vyumba ambayo hulipwa kila mwezi. • Kama malipo ni kwa kila mwaka, unazidisha mara 12 na unapata kiasi halisi kinachohitajika. Au unagawanya kiasi cha mwaka mara kumi na mbili na unapata kujua unahitajika kulipa kiasi gani kwa mwezi. 43
Matumizi ya lazima • Panga matumizi kwa kuzingatia uzito wa mahitaji muhimu kwa mwezi. • Baadhi ya mahitaji muhimu ni: Chakula, kodi ya nyumba, Maji/umeme, Mkaa/kuni/gesi, nauli ya kwenda kazini na kurudi, Sabuni za kufulia na Sabuni za kuogea. 44
Matumizi ya lazima • Mahitaji ya wanafunzi kama wapo: - Nauli, Maji ya kunywa, chai, mahitaji ya kishuleni, Madaftari, kalamu n. k. Sadaka • Itakuwa vema kama utapata ushauri kutoka kwa wataalamu wa mambo ya fedha ili wakusaidie namna ya kupanga bajeti yako vizuri na kukuonesha jinsi ya kubana matumizi. 45
Matumizi ya lazima • Kupanga bajeti hakuna maana kuwa ni lazima ufuate hivyo unaweza ukabadilisha matumizi kufuatana na umuhimu wa mahitaji yanavyojitokeza mwezi hadi mwezi. • Shaurianeni kwa pamoja jinsi ya kupunguza matumizi. Watoto wanaweza kushirikishwa pia, lakini jambo hili litategemea umri walionao. 46
Hatua za Kutumia fedha kwa njia nzuri: • Hatua ya kwanza: • Jifunze namna ya kudhibiti matamanio yako. Watu wanalelewa kuwa ni wenye kutumia tangu wakiwa umri mdogo, na kutumia kwa njia ya kusukumwa na matamanio. • Jifunze namna ya kufanya matumizi makubwa kutokana na mipango na bajeti ulizojiwekea, ndio utakuwa umeanza kuzuia manunuzi yanayosukumwa na matamanio ya nafsi. 47
Hatua za Kutumia fedha kwa njia nzuri: • Hatua ya Pili: • Ni kujipa muda wa kutosha kabla ya kufanya manunuzi makubwa. • Mtazamo wa kiakili na kiweledi ni kuchukua muda wa kutosha wa kufanya utafiti na kutathmini njia mbali za kununua hiyo bidhaa unayoitaka. Na pia kuangalia thamani ya hiyo bidhaa kutoka kwa wauzaji tofauti kabla ya kuamua kufanya manunuzi. 48
Hatua za Kutumia fedha kwa njia nzuri: • Hatua ya tatu: • Ni kujipamba na tabia ya kutumia fedha taslimu au kadi ya plastiki yenye fedha kwa manunuzi yako yote. • Tabia hii itakuwezesha kujenga na kuwa na tabia ya kujua na kudhibiti matumizi yako. 49
Hatua za Kutumia fedha kwa njia nzuri: • Ni rahisi na hatari kununua vitu vilivyo nje ya uwezo wetu kwa kutumia kadi za mikopo (Credit card). • Na kile kinachoanza kama deni dogo ni rahisi kuwa kubwa na likachukua miaka kulilipa. 50
Wigo wa Wanaokutegemea Kisheria 51
• Swali: Mtu ana nduguze wawili halisi wote Matajiri. Lakini yeye ni fukara. Ni yupi kati ya wawili anayewajibika kumhudumia ndugu yao. • Jibu: Wote wawili wanawajibika kumhudumia, nusu kwa nusu. Kwa sababu ya kuwepo sababu ya kurithiana. Na hukumu inazunguka pamoja na sababu yake. Tunasema, hawa ndugu wawili wanamrithi ndugu yao nusu kwa nusu. Na wao wanawajibika kumhudumia nusu kwa nusu. 52
• Swali: Mama ana watoto wawili. Mama ni mwenye uwezo. Na mmoja wa watoto wake ana uwezo. Lakini wa pili fukara. Nani anayepasa kutoa kumsaidia mwingine. • Jibu: Mama anawajibika kutoa theluthi moja, na ndugu theluthi mbili. 53
• Swali: Baba na mama wana mtoto fukara. Nao ni matajiri. Nani kati ya wawili hawa anawajibika kutoa huduma. • Jawabu: Anayewajibika hapo kutoa nafaqa ni baba. Baqara 233: “Kwa yule aliyezaliwa, baba anawajibika kumhudumia na kumvisha kwa wema. ” • Talaq: 6, “Iwapo wake zenu watawanyonyesheeni wenenu, wapeni ujira wao. ” anayeambiwa ni baba. Hapa hapaangaliwi uwezo, bali panaangaliwa jukumu. 54
• Swali: Mke akiwa mkwasi na mume fukara. Je anawajibika mke kumhudumia mumewe? • Jibu: Analazimika mke kutoa huduma kwa mumewe. Ushahidi kauli ya Allah Baqarah: 233. wa alal warithi mithlu dhalika. “Na kwa mrithi mfano wa hivyo. ” kama ulivyowajibika kumhudumia yeye, naye anawajibika. Kauli ya Ibn hazm. • Kauli sahihi ya jamhuri ya wanazuoni, mke hawajibiki kumhudumia mumewe. Bali anaweza kumpa sadaka. Kama Mtume alivyosema kumuambia mke wa ibn Mas’ud, “Mumeo na wanao wana haki zaidi ya sadaka yako. ” 55
- Slides: 55