KUSHIRIKI NENO Somo la 7 kwa ajili ya

  • Slides: 9
Download presentation
KUSHIRIKI NENO Somo la 7 kwa ajili ya Agast 15, 2020

KUSHIRIKI NENO Somo la 7 kwa ajili ya Agast 15, 2020

Yesu alisema: “[Maandiko] Yananishuhudia. ” (Yohana 5: 39) Yesu ndiye kiini cha Biblia nzima.

Yesu alisema: “[Maandiko] Yananishuhudia. ” (Yohana 5: 39) Yesu ndiye kiini cha Biblia nzima. Ndiyo maana Biblia ina nguvu sana. Mungu amekua akijinyesha Mwenyewe kwa jamii ya wanadamu kwa njia mbali, na Biblia ni njia Yake ya pekee. Siyo kitabu cha kusoma-soma tu, lakini ni cha “kuliwa” (Ezekiel 3: 3). Inatupasa kuyaacha Maandiko yajaze fikra zetu, na kutupatia nguvu ya kushirikisha kiini chake kwa wengine; hilo ndilo, pendo na tabia ya Yesu. Ni nini Biblia inasema kuhusu yenyewe? Ubora wake Nguvu yake ya kuumba Ni nini tunaweza kufanya nayo? Kupata Zaidi ya faida zake Kuamini katika ahadi zake Kushirikisha

UBORA WAKE “Neno lako ni taa ya miguu yangu, mwanga wa njia zangu. ”

UBORA WAKE “Neno lako ni taa ya miguu yangu, mwanga wa njia zangu. ” (Zaburi 119: 105) Biblia imelinganishwa na ishara nyingu zinazoonyesha ubora wake. Zaburi 119: 105 Yeremia 23: 29 Luka 8: 11 Mathayo 4: 4 Mwanga Moto Nyundo Mbegu Mkate Akili yenye giza huangazwa Huteketeza dhambi zetu Huponda mioyo yetu migumu Hupandikiza uzima ndani yetu uletao matunda kwa ajili ya ufalme wa Mungu Hushibisha roho zetu na kung’arisha nafsi zetu Pale tunapojifunza Neno, maisha yetu hubadilishwa kwa wema Wake, yakifungwa na pendo Lake, yakishangazwa na neema Yake, na kuridhika katika uwepo Wake.

NGUVU YAKE YA KUUMBA “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena

NGUVU YAKE YA KUUMBA “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. ” (Waebrania 4: 12) Hapo mwanzo, Mungu “alisema, na ikawa; Yeye aliamuru, na ikasimama. ” (Zaburi 33: 9) Nguvu ile ya Neno la Mungu linaloumba inapatikana katika Neno Lake lililoandikwa, yaani Biblia. Roho yule aliyefanya kazi katika Uumbaji ndiye aliyeyavuvia Maandiko Matakatifu. Roho Mtakatifu anaweza kufanya uumbaji mpya ndani yetu. Tunachopaswa kufanya ni kumwacha afanye kazi katika maisha yetu kwa kadri tunavyosoma Biblia. Roho Mtakatifu pia atabadilisha maisha ya watu wengine pale tunapowasaidia kuyaelewa Maandiko.

KUPATA ZAIDI YA FAIDA ZAKE “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,

KUPATA ZAIDI YA FAIDA ZAKE “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki. ” (2 Timotheo 3: 16) Biblia imejaa faida kwa ajili ya maisha yetu. Hebu tuangalie baadhi yake. 2 Petro 1: 4. inatufanya kuwa washirika wa ahadi za kiungu Yakobo 1: 21. Huokoa roho zet Matendo 20: 32. Hutupatia urithi pamoja na waliotakaswa 2 Timotheo 3: 15, 17. Hutupatia hekima, uimara, na utayari wa kufanya kazi njema 2 Timothe 3: 16. Andiko. Huufunua ukweli na kuupinga uongo Kuonya. Hufunua dhambi zetu Kuongoza. Hubadili makosa yetu Kuadibisha. Hufunua haki ya Kristo

KUAMINI KATIKA AHADI ZAKE “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri

KUAMINI KATIKA AHADI ZAKE “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. ” Isaya 40: 31 Luka 12: 27 -28 (Wafilipi 4: 19) Kuna zaidi ya ahadi 3, 000 katika Biblia. Mungu amedhamiria kutimiza kila ahadi katika maisha yetu, na Anatusihii kuzidai ahadi hizo. Zinathibitisha kwamba Mungu hujali mahitaji yetu ya kimwili na ya kiroho. Siku ile tutakapokutana Naye uso kwa uso, tutasema: “Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi zake njema, aliyoahidi. ” (1 K. 8: 56) Hata hivyo, ahadi Zake zina masharti. Kukosa imani kunaweza kuzifuta (Waebrania 4: 2). Isaya 33: 16 Isaya 43: 2 Zaburi 4: 8 Zaburi 91: 11 Mibaraka ya ahadi za Mungu zinakuwa zetu pale tunapozidai kwa imani na kuamini kwamba ni kweli kwa sababu Kristo daima ni mwaminifu.

“Maandiko Matakatifu yanapaswa yapokelewe kama neno la Mungu kwetu, siyo lililoandikwa tu, lakini lililotamkwa

“Maandiko Matakatifu yanapaswa yapokelewe kama neno la Mungu kwetu, siyo lililoandikwa tu, lakini lililotamkwa […] Hivyo pamoja na ahadi zote za neno la Mungu. Ndani yake Anaongea na sisi mtu mmoja, akiongea moja kwa moja kama vile tunaisikiliza sauti Yake. Ni katika ahadi hizi Kristo huwasilisha neema na nguvu Zake kwetu. Ni kama majani kutoka katika mti ule ambao ‘ni wa kuwaponya mataifa. ’ Ufunuo 22: 2. Zikipokelewa, zikatendwa, zitakuwa nguvu ya tabia, msukumo na chakula cha kusitawisha maisha. ” E. G. W. (The Ministry of Healing, cp. 7, p. 122)

KULISHIRIKISHA “Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa

KULISHIRIKISHA “Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi, huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao. ” (Isaya 50: 4) Mungu “huamsha” masikio yetu na kutupatia hekima pale tunapojifunza Biblia katika mfumo wa kila siku. Pia Hutupatia “ulimi wa hao wafundishwao” ili tuishirikishe habari njema kwa wengine. Neno la Mungu halipaswi kufungiwa katika mioyo yetu. Furaha ya wokovu hutusukuma kufanya kila liwezekanalo kuushirikisha ujumbe wake kwa wale wasioujua bado. Paulo alituamuru kufanya lifuatalo: “Lihubiri neno; uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. ” (2 Tim. 4: 2)

“Elimu inayopatikana kwa kuyachunguza Maandiko ni ufahamu wa kivitendo wa mpango wa wokovu. Elimu

“Elimu inayopatikana kwa kuyachunguza Maandiko ni ufahamu wa kivitendo wa mpango wa wokovu. Elimu ya namna hiyo itarejesha sura ya Mungu ndani ya nafsi. Huipatia nguvu na kuiimarisha akili dhidi ya majaribu, na kumfaa mwanafunzi kuwa mtendakazi pamoja na Kristo katika utume wake wa rehema kwa ulimwengu. Itamfanya kuwa mwanafamilia ya mbinguni; na kumwandaa kushiriki urithi wa watakatifu katika haki. ” E. G. W. (Christ’s Object Lessons, cp. 2, p. 42)