UUMBAJI NA ANGUKO Somo 1 kwa ajili Oktoba
UUMBAJI NA ANGUKO Somo 1 kwa ajili Oktoba 6, 2018
FUNGU LA KUKARIRI “Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki” (Mwanzo 15: 5 -6)
Umoja na maelewano aliokuwa ameupanga Mungu kwa ajili ya wanadamu uliharibiwa na dhambi. Hata hivyo, Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kubuni mpango wa kurejesha umoja huu. Urejeswaji wa mwisho ungekuja kupitia kazi ya Kristo, lakini Mungu aliwachagua wanadamu waoneshe upendo na neema yake kwa ulimwengu. 1. Umoja wa Kwanza Kuumbwa ili kupenda 2. Umoja wa wavujika Tangu Adam hadi Gharika Mnara wa Babeli 3. Kuurejesha Umoja Mungu amuita Adamu Israeli ya chaguliwa
KUUMBWA ILI KUPENDA “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwanzo 1: 27) Mungu aliumba kila kitu kikiwa “chema sana” (Mwanzo 1: 31). Dunia, wanyama na wanadamu wakihusiana mmoja kwa mwingine kwa amani. Wanadamu, tofauti na wanyama, waliumbwa kwa sura ya Mungu. Walifanywa kuwa mawakili wa uumbaji. Mungu ni upendo (1 Yohana 4: 8), Hivyo sura ya Mungu hujumuisha uwezo wa kupenda. Sura ya Mungu ili tengenezwa na watu wawili, mwanaume na mwanamke. Kwa pamoja waliubwa kwa sura ya Mungu. Huo ni umoja wenye upendo katika Msingi wake.
“Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani] Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua. ”(Mwanzo 4: 8) Dhambi ya Adamu na Hawa iliharibu maelewano, umoja na upendo kati ya mwanaume na mwanamke, Jamii ya wanadamu na uumbaji, Jamii ya wanadamu na Mungu. Mwanaume alimlaumu mwanamke (Mwanzo 3: 12) Asili ikaharibika (Mwanzo 3: 17 -18) Kaini akamuua Habili (Mwanzo 4: 8) Mwanadamu akaharibika kabisa (Mwanzo 6: 5) Hata hivyo, Mungu alichagua waliosalia (Nuhu na familia yake) na kuwapa wanadamu nafasi ya pili. Upinde wa mvua hutusaidia kukumbuka kuwa Mungu bado anataka kutimiza mpango wake wa awali kwa ajili yetu. Gharika likaweka ukoma wa historia ya mwanadamu (Mwanzo 6: 7)
“Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote. ” (Mwanzo 11: 9) Wanadamu walijaribu kutafuta umoja bila Mungu. Hii ilipelekea ibada ya sanamu na kujitukuza wenyewe. Mungu alilazimika kuukomesha umoja huo wa uongo kwa kuumba lugha tofauti. Dhambi ilileta ukosefu wa umoja miongoni mwa wanadamu na kuharibika kwa mpango wa mungu wa awali. Dhambi ilisababisha: Machafuko kwenye ibada. Kusambaa kwa kasi kwa uovu na ukosefu wa maadili juu ya nchi. Kugawanyika kwa wanadamu katika tamaduni, lugha na rangi. MNARA WA BABELI
MUNGU AMUITA IBRAHIMU “Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. ” (Yakobo 2: 23) Alikuwa mtiifu. Tumaini lake lilijengwa juu ya ahadi ya Mungu. Aliamini kuwa Mungu angetimiza ahadi yake; Uzao kama nyota za angani. Aliuamini mpango wa Mungu wa wokovu. Mungu alijaribu kurejesha umoja tena kupitia kwa Ibrahimu ni baba wa waamino wote. Tunaweza kujifunza dhana za msingi za umoja miongoni mwa wakristo katika kielelezo chake:
ISRAELI YA CHAGULIWA “Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu…” (Kumbukumbu la Torati 7: 7 -8) Mungu aliwachagua Israeli kama watu wake kwa sababu aliwapenda. Hawakuwa wamefanya lolote la kuwafanya wafae kuchaguliwa. Mungu alitaka kupeleka ujumbe wake kwa ulimwengu na kuwakomboa wanadamu kupitia kwa Israeli. Aliwapa nyenzo zote za kiroho walizohitaji ili kutimiza kusudi hilo. Kanisa la kikristo ni Israeli mpya. Ni lazima tuelewe kuwa hatuna chakujivuna mbele yake(Mungu). Mungu alituchagua ili tuwe wamoja na yeye kwa sababu tu anatupenda (Wagalatia 3: 28)
“Hoja yenye ushawishi zaidi tunayoweza kutoa kwa ulimwengu kuhusu utume wa Kristo ni kuonekana katika umoja mkamilifu. Umoja kama ulio kati ya Baba na Mwana unapaswa kudhihirishwa miongoni mwa wote wanao iamini kweli. Wale walio na umoja hivyo katika utii dhati kwa neno la Mungu watajazwa nguvu. Kama wote wangejiweka wakfu kwa Bwana, na kupitia utakaso wa ile kweli wakiishi katika umoja mkamilifu, Nguvu ya ushawishi ingeambatana na utangazaji wa hiyo kweli! Ni huzuni iliyoje kwamba makanisa mengi yanapotosha ule msukumo utakasao wa ile kweli, kwa sababu hawaidhihirishi ile neema iokoayo ambayo ingewafanya wawe wamoja pamoja na Kristo, kama Kristo alivyo na umoja na Baba! Kama wote wangefunua umoja na upendo unaopaswa kuwepo miongoni mwa ndugu, Nguvu ya Roho mtakatifu ingejidhihirisha katika msukumo wake uokao. Kwa uwiano na umoja wetu na Kristo ndivyo itakavyokuwa nguvu yetu ya kuokoa roho. ” E. G. W. (Manuscript 88, 1905, “One, Even as We Are One”)
- Slides: 9