KUPENDA REHEMA Somo la 12 kwa ajili ya











- Slides: 11
KUPENDA REHEMA Somo la 12 kwa ajili ya Septemba 21, 2019
Kulingana na kanuni za ufalme alizofundisha Yesu, ni zipi zinapaswa kuwekewa kipaumbele cha juu katika maisha yetu? Je, kuwajali wale wenye mahitaji ni moja ya vipaumbele vya juu? Tuwatendeeje wale wenye uhitaji? Vipaumbele vyetu Mtazamo wetu Huruma Ukarimu Wapatanishi Walinzi
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. ” (Mathayo 6: 33) Yesu aliorodhesha vipaumbele vikuu vya raia wa ufalme wa Mbinguni: 1 Kujitosheleza mahitaji yetu mhimu (Mathayo 6: 25 -32) • Msilemewe na hayo. Mungu daima hutoa. Kuutafuta ufalme wa mbingui (Mathayo 6: 33) 2 • Ufalme wa Mungu uko kati, siyo sisi. 3 Kutafuta haki ya ufalme (Mathayo 6: 33) • Kuwasaidia wale wenye uhitaji na walionyanyaswa. Kutii mamlaka (Mathayo 22: 21) • Tii mamlaka (Romans 13: 1 -7), isipokuwa kama inaenda kinyume na Sheria ya Mungu (Matendo 5: 29). Tufanyeje pale kipaumbele cha 3 na 4 vinaposhindana? 4
HURUMA “Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? ” (Yakobo 2: 15 -16) Ni lazima tuombe hekima ya Mungu kabla ya kutenda Matarajio Ni lazima tujifunze kutambua hali za wengine na kutenda pale tu tunapokuwa na maelezo sahihi Maombi Ni lazima tutambue hisia za wanaoumia Elimu Huruma Kama Wakristo, lazima tuwe na huruma na kuwasaidia wale walio na uhitaji. Huu usiwe msaada wa mpaka usukumwe. Zingatia yafuatayo: Ni lazima tusaidie daima, hata kama wale tunawasaidia hawatendi kama turivyotarajia
“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. ” (2 Wakorintho 9: 7) UKARIMU Wakati wote hatuwezi kuwasaidia wahitaji tulionao tu. Kuna watu tunaoweza kuwasaidia wanaoishi mbali. Katika shida hizo, msaada wa kifedha ni jambo jema. Biblia inatushauri kuwa wakarimu (Mit. 19: 17). Ukarimu wetu ni mwitikio wa ukarimu wa Mungu (1 Nyak. 29: 14; 2 Kor. 8: 9). Ni tiba bora kwa ubinafsi. Ukarimu si jambo la wakati mmoja au la kulazimishwa. Roho ya ukarimu ni lazima iendelezwe; shauku ya kudumu ya kuwasaidia wengine.
WAPATANISHI “Heri wapatanish; maana hao wataitwa wana wa Mungu. ” (Mathayo 5: 9) Kuna migogoro ya kisiasa, kiuchumi na chuki kati ya mataifa, jamaa na makundi ya kikabila au jamii ambayo huleta maumivu na kuhitaji msaada wa kibinadamu. Tumeitwa kuitika kwa wenye uhitaji na kupatanisha mgogoro kwa kadri ya uwezo wetu. Yesu alitufundisha kutoanzisha migogoro: usikasirike, usitunze chuki, wapende adui zako, waombee wanaokuudhi… “Injili ya amani" hutengeneza fikra zetu juu ya wengine na namna ya kuwachukulia.
“Piga kelele, usiache; paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao. ” WALINZI (Isaya 58: 1) Sisi ni mikono na miguu ya Yesu duniani ambao inatupasa kufanya mema kwa wenye uhitaji. Pia tumeitwa kuwa sauti ya Yesu kupiga kelele wa ajili ya haki. Kama manabii wa kale, ni lazima tuwe sauti ya wale wasiokuwa nayo. Ni lazima tuongee kuwalinda wasio na ulinzi. Sauti yetu moja inaweza isibadili halisi, lakini hatuwezi kunyamaza. Kwa nyongeza, sauti yet kama kanisa mahalia, kitaifa na la kiulimwengu ina nguvu.
Umaskini upo katika kila jamii. Umaskini humwibia mwanadamu haki zake za msingi. Huwaacha watu njaa; huwanyima huduma za matibabu, maji safi, elimu, fursa ya kazi, na matokeo ya mara kwa mara ya kujihisi kukosa uwezo, kukosa matumaini, na kukosekana kwa usawa. Kila siku, zaidi ya watoto 24, 000 hufariki kutokana na hali isiyozuilika iliyosababishwa na umaskini. Waadventista Wasabato wanaamini kwamba matendo ya kupunguza umaskini na matendo ya udhalimu ni sehemu muhimu ya wajibu wa kijamii wa mkristo. Biblia kwa uwazi inafunua shauku ya Mungu kwa maskini na matarajio Yake ya namna wafuasi wake wanavyopaswa kuwachukulia wale ambao hawawezi kujihudumia wenyewe. Wanadamu wote wamebeba sura ya Mungu na ni wapokeaji wa mibaraka ya Mungu (Luka 6: 20). Katika kufanya kazi na maskini tunafuata mfano na mafundisho ya Yesu (Mathayo 25: 35, 36). Kama jumuiya Waadventista Wasabato husimamia haki kwa maskini na “fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; uwatetee watu wote walioachwa peke yao" (Mithali 31: 8) na dhidi ya wale “wanaowanyang’anya maskini haki yao" (Isaya 10: 2). Tunashiriki na Mungu ambaye “humfanyia mhitaji haki yake" (Zaburi 140: 12).
Kufanya kazi ili kupunguza umaskini na njaa ina maana kubwa zaidi ya kuonyesha huruma tu kwa maskini. Ina manisha kutetea sera za umma ambazo zinatoa haki na usawa kwa maskini, kwa ajili ya uwezeshaji na haki za binadamu. Inamanisha kudhamini na kushiriki katika miango inayoeleza visababishi vya umaskini na njaa, kuwasaidia watu kujenga maisha bora. Dhamira hii ya haki ni tendo la upendo (Mika 6: 8). Waadventista Wasabato wanaamini pia kuwa ni wito wa kuishi maisha ya unyenyekevu na adabu ambayo ni ushuhuda dhidi ya uyakinifu (mali) na tamaduni za utajiri. Waadventista Wasabato wanaungana na jumuiya ya kimataifa katika kusaidia Jumuiya ya Madora ya Mipango-Maendeleo ya Milenia kwa kupunguza umaskini angalau kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2015. Katika kuboresha hili, washirika wa Waadventista Wasabato kwa asasi za kiraia, serikali na wengine, wanafanya kazi kwa pamoja kitaifa na kimataifa ili kushiri katika kazi ya Mungu ya kudumisha haki katika ulimwengu uliovunjika.
Kama wafuasi wa Kristo tunaingia katika kazi hii tukiwa na tumaini thabiti, tukiwa tumetiwa nguvu kwa maono ya ahadi ya Mungu ya mbingu mpya na nchi mpya mahali ambapo hakuna umaskini wala udhalimu. Waadventista Wasabato wameitwa kuishi kwa ubunifu na uaminifu ndani ya maono hayo ya Ufalme wa Mungu kwa kutenda ili kuumaliza umaskini sasa. Tamko hili lilipitishwa na kupigiwa kura na Kamati Tendaji ya Halmashauri Kuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato Juni 23, 2010, na lilitolewa katika kikao cha Halmashauri Kuu huko Atlanta, Georgia, Juni 24 -Julai 3, 2010.
“Huruma ya ndani ya Mwokozi wetu iliamshwa kwa maumivu na wanadamu walioanguka dhambini. Kama ungelikuwa mfuasi wake, ungeliongeza upendo na huruma. Kutojali kwa ole za mwanadamu lazima kutoe nafasi ya kuiishi shauku iliyo katika maumivu ya wengine. Wajane, yatima, wagonjwa na walio katika kufa, daima watahitaji msaada. Hapa ndipo palipo na fursa ya kutangaza injili—kumshikilia Kristo, tumaini na mfariji wa wanadamu wote. Wakati mwili wenye maumivu unapokuwa umepona, na ulionyesha shauku halisi katika kuteseka huko, moyo hufunguliwa, na unaweza kumwagilia mtende wa mbingunu. Ukiwa unamtazama Yesu na kuchota ufahamu kutoka kwake na nguvu na neema, unaweza kuipandikiza faraja yake kwa wengine kwa sababu Mfariji yuko na wewe. ” E. G. W. (Counsels on Health, p. 34)









