Neno La Uzima Januari 2013 Toka tarehe 18

  • Slides: 25
Download presentation
Neno La Uzima Januari 2013

Neno La Uzima Januari 2013

Toka tarehe 18 Januari hadi 25 mahali pengi duniani huadhimishwa Juma la Sala kwa

Toka tarehe 18 Januari hadi 25 mahali pengi duniani huadhimishwa Juma la Sala kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, hali mahali pengine huadhimishwa karibu sikukuu ya Pentekoste. Mwaka huu mstari uliochaguliwa kwa ajili ya Juma la Sala ni: “Bana anataka nini kwako” (Mik 6: 6 -8).

Chiara Lubich alikuwa amezoea kueleza mstari wa Biblia kila mara. Ili kuendeleza msaada huo

Chiara Lubich alikuwa amezoea kueleza mstari wa Biblia kila mara. Ili kuendeleza msaada huo wake, tunashauri matini yake moja ya kueleza Mt 9: 13 (linganisha na Hos 6: 6) aliyoandika katika mwezi Juni 1996, ambayo inaweza kusaidia kuchimba ndani zaidi Neno linalotolewa: “Nataka rehema, wala si sadaka”

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13)

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13)

Nataka rehema, wala si sadaka. Unakumbuka Yesu aliposema maneno hayo? Alipokuwa akiketi nyumbani ale

Nataka rehema, wala si sadaka. Unakumbuka Yesu aliposema maneno hayo? Alipokuwa akiketi nyumbani ale chakula, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja na wakaketi pamoja naye. Mafarisayo walipoona waliwaambia wanafunzi wake: Mbona Mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye Yesu aliposikia, aliwaambia:

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13)

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13)

Yesu anatamka mstari wa nabii Hosea, na jambo hilo linadhihirisha kuwa anayapenda maneno hayo

Yesu anatamka mstari wa nabii Hosea, na jambo hilo linadhihirisha kuwa anayapenda maneno hayo na wazo lililomo: naam ni mwongozo anaoshika katika mwenendo wake. Kwa maana inadhihirisha utangulizi wa upendo mbele ya amri nyingine yo yote, juu ya kila sheria na agizo.

Huo ndio Ukristo: Yesu alikuja kusema kuwa Mungu anataka toka kwako, kuhusu wengine –

Huo ndio Ukristo: Yesu alikuja kusema kuwa Mungu anataka toka kwako, kuhusu wengine – wanaume na wanawake -, kabla ya yote, kuna upendo, na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu yaliyokwisha tangazwa katika Maandiko, kama yanavyoonyesha maneno ya nabii.

Upendo, kwa kila Mkristu, ni muhtasari wa maisha yake, sheria ya kimsingi ya mwenendo

Upendo, kwa kila Mkristu, ni muhtasari wa maisha yake, sheria ya kimsingi ya mwenendo wake, uamuzi wa kuishi kwake.

Daima upendo lazima itangulie sheria nyingine. Zaidi: upendo wa wengine, kwake Mkristo, ni msingi

Daima upendo lazima itangulie sheria nyingine. Zaidi: upendo wa wengine, kwake Mkristo, ni msingi imara ambamo anaweza kutekeleza miongozo mingine yote.

. . . nataka rehema, wala si sadaka

. . . nataka rehema, wala si sadaka

Yesu anataka upendo, na rehema ni sura yake moja. Anataka kuwa Mkristo aishi hivyo

Yesu anataka upendo, na rehema ni sura yake moja. Anataka kuwa Mkristo aishi hivyo hasa kwa sababu ndivyo alivyo Mungu.

Kwake Yesu, Mungu kwanza ni mwenye huruma, Baba anayewapenda wote, anayewaangazia jua lake waovu

Kwake Yesu, Mungu kwanza ni mwenye huruma, Baba anayewapenda wote, anayewaangazia jua lake waovu na wema.

Basi, ikiwa Mungu ni hivyo, ikiwa Yesu ni hivyo, nawe pia unapaswa kulisha hisia

Basi, ikiwa Mungu ni hivyo, ikiwa Yesu ni hivyo, nawe pia unapaswa kulisha hisia hizo sawa.

. . . nataka rehema, wala si sadaka

. . . nataka rehema, wala si sadaka

“. . . wala si sadaka”. Ikiwa huna upendo kwa ndugu, Yesu hapendezwi na

“. . . wala si sadaka”. Ikiwa huna upendo kwa ndugu, Yesu hapendezwi na ibada yako. Hapokei sala yako, kushiriki kwako ùEkaristi, sadaka unazoweza kufanya, ikiwa hayo yote hayachanui toka moyo wako ulio na amani na wote, umejaa upendo kwa wote.

Unakumbuka maneno yale ya maana sana ya mafundisho ya mlimani? “Basi ukileta sadaka yako

Unakumbuka maneno yale ya maana sana ya mafundisho ya mlimani? “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako” (Mt 5: 23 -24).

Maneno hayo yanasema kuwa ibada inayompendeza Mungu zaidi ni upendo wa jirani, unaopaswa kuwekwa

Maneno hayo yanasema kuwa ibada inayompendeza Mungu zaidi ni upendo wa jirani, unaopaswa kuwekwa kama msingi kwa ibada ya Mungu. Ungetaka kumtolea Mungu kipaji, hali ukiwa na hasira na ndugu yako (au ndugu yako kwako), baba yako angekuambia nini? “Upatane, halafu njoo, unitolee kipaji unachotaka”.

Lakini kuna zaidi. Upendo, licha ya kuwa msingi wa maisha ya Kikristo, pia ni

Lakini kuna zaidi. Upendo, licha ya kuwa msingi wa maisha ya Kikristo, pia ni njia wima wa kulinda ushirikiano na Mungu. Watakatifu wote wanasema hivi, mashahidi wa Injili waliotutangulia, na pia wanang’amua Wakristo wanaoishi imani yao: wakisaidia ndugu zao, hasa wahitaji, ibada yao inaongezeka, ushirikiano na Mungu hupata nguvu zaidi, wanatambua kuwa kuna pingu kati yao na Bwana: na hiyo inajazia zaidi furaha maisha yao.

. . . nataka rehema, wala si sadaka Basi, utaishije Neno hilo jipya la

. . . nataka rehema, wala si sadaka Basi, utaishije Neno hilo jipya la uzima?

Usibague kati ya watu unaokutana nao, usimtenge mtu, bali uwatolee wote unachoweza, ukimwiga Mungu

Usibague kati ya watu unaokutana nao, usimtenge mtu, bali uwatolee wote unachoweza, ukimwiga Mungu Baba.

Tengeneza mizozano midogo kwa mikubwa yasiyompendeza Mungu na kutilia uchungu maisha, jua lisichwe –

Tengeneza mizozano midogo kwa mikubwa yasiyompendeza Mungu na kutilia uchungu maisha, jua lisichwe – yanavyosema Maandiko (rej. Ef 4: 26) – na uchungu wenu bado haujawatoka, kwa mtu yeyote.

Ukijimudu hivyo, yote utakayofanya yatampendeza Mungu na kudumu kwa milele. Ikiwa unafanya kazi au

Ukijimudu hivyo, yote utakayofanya yatampendeza Mungu na kudumu kwa milele. Ikiwa unafanya kazi au unapumzika, ikiwa unasoma au unacheza, ikiwa unakaa na watoto wako au kusindikiza mke wako au bwana wako matembezini, ikiwa unasali au kujitolea sadaka, ikiwa unatekeleza matendo yale ya ibada yanayolingana na wito wako wa Kikristo, yote yatakuwa vifaa halisi kwa Ufalme wa Mbinguni.

Paradisi ni nyumba tunayojenga hapa duniani, na kukalia baadaye mbinguni. Na hujengeka na upendo.

Paradisi ni nyumba tunayojenga hapa duniani, na kukalia baadaye mbinguni. Na hujengeka na upendo.

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13)

Nendeni mkajifunze, maana yake maneno haya: Nataka rehema, wala si sadaka (Mt 9: 13) “Parola di Vita” inatangazwa na Movement of Focolare. Matini hii Imetolewa katika Città Nuova, n. 10/1996 Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. Placido D’Omina (Sicily, Italy). Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzima kwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti. Kwa kupata maelezo www. focolare. org PPS hiyo, katika lugha mbali inatangazwa katika www. santuariosancalogero. it (na hapo unaweza kupakua)