Lesoni ya 5 ajili ya Agosti 4 2018

  • Slides: 9
Download presentation
Lesoni ya 5 ajili ya Agosti 4, 2018

Lesoni ya 5 ajili ya Agosti 4, 2018

Baada ya kumpiga mawe Stefano, Sanhedrini ilimpa uwezo Sauli wa Tarso (Paulo) kutesawafuasi wa

Baada ya kumpiga mawe Stefano, Sanhedrini ilimpa uwezo Sauli wa Tarso (Paulo) kutesawafuasi wa Yesu Mnazarayo. Sauliakawa “mtume”wa Sanhedrini kumaliza kikundi kiitwacho “njia. ”Lakini Yesu aliingiliakati na kumweka Sauli chini ya amri yake. Alikuwa na sehemu ya Pauli kwenye mikakati yake kama mtume kwa mataifa. q Mtume wa Sanhendrini. Kulitesa Kanisa. Matendo 9: 1 -2 Kuzipiga teke ncha za miiba. Matendo 9: 3 -9 q Mtume wa Yesu. Uongofu wa Paulo. Matendo 9: 10 -18 Paulo. Dameski. Matendo 9: 19 -25 Paulo. Yerusalemu. Matendo 9: 26 -31

KULITESA KANISA Mdo 9: 1 -2 “Lakini Sauli, akazidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi

KULITESA KANISA Mdo 9: 1 -2 “Lakini Sauli, akazidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua kwenda Dameski zilizoandikiwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake awafunge na kuwaleta Yerusalemu. ” (Matendo 9: 1 -2) Sauli alielezea jinsi alivyokua na shauku nzito kwamba ilimpasa kutenda mambo mengi kupingamana na kutesa wale wote walioamini Kristo Yesu. (Matendo 26: 9 -11) Mtu aliye kufa kwa kuangikwa alilaaniwa na Mungu, hivyo hangekubali kamwe kwamba Masihi aliangikwa na kufa. (Kumbukumbu 21: 22 -23) Sanhedrini ilimpa Sauli uwezo, kwa hiyo akawa shalia wao, mjumbe rasmi. Neno la Kiyunani kwa shalia ni apóstolos (yaani mtume). Sauli alikuwa mtume wa Sanhedrin. Alisafiri Damaski. Alitaka kuwakamata waumini wa "Njia" na kisha kuwaleta Yerusalemu kuhukumiwa kwa uasi Alisafiri Kazikazini kwa maili 135 hadi Dameski. Alinuiya kuwakamata waumini wa ile“njia” ili kuwarudisha Yerusalemu wahukumiwe kwa kosa la kufundisha upotofu.

Mdo 9: 3 -9 KUPIGA MATEKE MCHOKOO “Akasema, U nani wewe Bwana? Naye akasema,

Mdo 9: 3 -9 KUPIGA MATEKE MCHOKOO “Akasema, U nani wewe Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe, ni vigumu kwako wewe kuupiga mateke mchokoo. ’” (Matendo 9: 5) Wote waliosafiri pamoja na Paulo waliona mwanga na kuanguka chini, lakini ni yeye tu alipofuka. Sauli pekee alielewa kilichotamkwa maana maono haya yalikua kwa ajili yake tu. Sauli alikuwa akitesa Kanisa, lakini Yesu alimwona Sauli alikuwa anamtesa. "Yeye awagusaye ninyi aigusa mboni la jicho lake. " (Zakaria 2: 8) Mchokoo ni fimbo ndefu yenye ncha kali. Wakulima hutumia kumuelekeza fahali au mifugo. Kuupiga mateke mchokoo huleta madhara tuu. Sauli alipiga mateke “mchokoo” wa dhamira yake, maana alikua na mashaka kama kweli Yesu ndiye Masihi wa kweli. Alipomuona uso Yesu aliyefufuka mashaka yake yote yalimwisha.

UONGOFU WA PAULO Mdo 9: 10 -18 “Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba,

UONGOFU WA PAULO Mdo 9: 10 -18 “Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula, akapata nguvu. ” (Matendo 9: 18) Paulo alikua na shauku ya kumfuata Yesu akamuuliza, “Ungependa nifanye nini? ” Kisha akawa kipofu kwa siku tatu. Paulo alijitengana msimamo wake kama Mtume wa Sanhendrini na akawa mjumbe wa Yesu Kristo. Alipaswa kukutana na Kanisa na kuwa mshiriki. Kisha afanye kazi pamoja na Kanisa. Anania aliitwa kwa sababu hiyo. Alikua na mashaka mengi, lakini hata hivyo alikutana na Paulo. Alimrejeshea uwezo wa kuona na kuuthibitisha mwito wake. Anania alimuhimiza Paulo kubatizwa na kujiunga na Kanisa.

Mdo 9: 19 -25 PAULO DAMESKI “Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni

Mdo 9: 19 -25 PAULO DAMESKI “Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. Hata siku nyingi zikapita, wayahudi wakafanya shauri ili wamwue; ” (Matendo 9: 20, 23) Mtu yule aliyekuja kuwakamata wanafunzi wa “masihi wa uongo” aliwatetea katika masinagogi. . Akitumia maadiko alithibitisha Yesu ni Masihi. Wayahudi waliingiwa na hofu hivyo waliomba msaada wa serikali ili Paulo akamatwe. (2 Wakorintho 11: 32 -33) Waumini walimsaidia Paulo, wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu. Tukio hili halikumvunja moyo Mtume huyu mpya, kwani kesha onywa kwamba atateseka. (Matendo 9: 16)

Mdo 9: 26 -31 PAULO YERUSALEMU “Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiungana wanafunzi, nao

Mdo 9: 26 -31 PAULO YERUSALEMU “Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiungana wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. ” (Matendo 9: 26) Kanisa Yerusalemu hawakuamini uongofu wa mtesi mkali wao kwamba ni kweli, ingawaje Paulo aliongolewa miaka mitatu kabla. Mungu alimtumia Barnaba kuondoa mashaka yao. Paulo aliendeleza kazi ya Stefano Yerusalemu; kazi ile aliyoipinga hapo mwanzo. Naye pia kama vile Stefano mahubiri yake yalikataliwa. Maisha yake yalikuwa hatarini. Maono yalimtokea kumuondoa Yerusalemu(Matendo 22: 17 -21). Alisaidiwa tena kutoroka na ndugu zake katika imani.

Kitabu hiki cha Matendo na Wagalatia huzungumzia msururu wa maisha ya Paulo tangu uongofu

Kitabu hiki cha Matendo na Wagalatia huzungumzia msururu wa maisha ya Paulo tangu uongofu wake hadi safari yake ya kwanza ya umishonari. Uongofu wa Sauli Kule Dameski (Matendo 9: 1 -18) Kuhubiri Dameski (Matendo 9: 1922) Dameski tena na kutoroka kupitia ukuta wa mji (Matendo 9: 23 -25) Ukaaji kule Uarabuni (Galatians 1: 17 Kurudi tena Yerusalemu baada ya miaka mitatu tangu kuongoka (Galatians 1: 18) Kuhubiri majimbo ya Shamu na Kilikia (Galatians 1: 21) Atumwa kama mmishonari pamoja na Barnaba (Matendo 13: 1 -3) Barnaba amleta Paulo Antiokia (Matendo 11: 2526)

“Kila wakati Bwana huwapa wanadamu kazi yake. Hapo ndio penye muungano kati ya uanadamu

“Kila wakati Bwana huwapa wanadamu kazi yake. Hapo ndio penye muungano kati ya uanadamu na uungu. Ndipo mtu anaitii nuru takatifu iliyomdhihirikia. Kama Sauli angesema, Bwana, sioni haja ya kufuata maagizo yako, kufanyia kazi wokovu wangu, hivyo basi hata ange dhihirishiwa nuru mara kumi zaidi ingekuwa kazi bure. Inampasa mwanadamu kuungana na uungu. Na ingawaje ni pambano gumu mwanadamu kuunga nia yake na uungu, abayo huja na lengoo na saa ya uumuzi mkuu kwa mapenzi ya mungu, akitegemea ushurutishwaji wa neema inayomwandama kila siku maisha yake. […] Fuata na utii uongozi wa Roho Mtakatifu. t. ” E. G. W. (Mawazo, Tabi, na Utu, Kitabu cha. 2, Sura. 84, Kur. 757)