Somo la 10 kwa ajili ya Juni 8

  • Slides: 10
Download presentation
Somo la 10 kwa ajili ya Juni 8, 2019 NYAKATI NDOGO ZA TAABU

Somo la 10 kwa ajili ya Juni 8, 2019 NYAKATI NDOGO ZA TAABU

“ ‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka”

“ ‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka” (Ephesians 4: 26)

Biblia ndiyo mwongozo halisi wa mwenendo. Inatoa ushauri wa thamani juu ya namna ya

Biblia ndiyo mwongozo halisi wa mwenendo. Inatoa ushauri wa thamani juu ya namna ya kutatua migogogro baina ya watu. Migogoro hii wakati mwingine huleta shida nyumbani. Wiki hii tumejifunza aya nyingi za Biblia ambazo zitatusaidia kuzuia na kutatua migogoro baina ya wanafamilia. Vipande saba vya ushauri kuzuia migogoro. Mashauri juu ya utatuzi wa migogoro: Kutawala hasira. Upendo wa kweli. Umuhimu wa msamaha.

“Mnafiki wewe! Itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa

“Mnafiki wewe! Itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. ” (Matayo 7: 5) Kabla ya kujaribu kurekebisha madhaifu ya watu wengine, lazima tutambue kwamba madhaifu yetu wenyewe ni makubwa, na ni lazima yarekebishwe kwanza. Kukosoa makosa ya wengine huzalisha shida zaidi badala ya kutatua. “Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. ” (Mithali 19: 11) Unapohisi umekosolewa, jiulize mwenyewe: inastahili kuanzisha ugomvi kwa sababu ya hii? Tafakari kilichotokea, shirikisha hisia zako kwa namna iliyo chanya, na pendekeza suluhu ambayo kwa hakika itakuwa bora kwa kila mmoja aliyehusika.

“Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; basi acheni ugomvi kabla haujafurika. ”

“Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; basi acheni ugomvi kabla haujafurika. ” (Mithali 17: 14) Kabla ya kuanzisha ugomvi, fikiria madhara yake katika siku mbili hadi tatu zijazo. Na ni nini madhara yake katika mwaka mmoja au miwili? Wanandoa wengi wamegombana juu ya mambo ambayo leo yamekuwa funzo. “Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. ” Warumi 14: 19) Tunaweza kuzuia ugomvi kwa kufuata vipande viwili vifuatavyo vya ushauri: 1. Fanya kila kitu ambacho huleta amani na maelewano nyumbani kwako. 2. Tafuta njia ya kuendeleza makuzi binafsi ya mwenzi wako.

“Tena iweni wafadhiri ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo

“Tena iweni wafadhiri ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. ”(Waefeso 4: 32) Lazima ujifunze kusamehe kama Kristo naye alivyokusamehe, hasa kama unafikiri mwenzi wako hasitahili msamaha wako. “kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. ” (Warumi 3: 23) Kubali kwamba mwenzi wako ni mdhambi na hajakamilika. Wakubali kama Kristo naye alivyokukubali wewe. Kwa maombi tafuteni kukua pamoja katika utakatifu. “Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo y wengine. ” (Wafilipi 2: 4) Usifanye kazi kwa ajili yako mwenyewe; uweke ustawi wa mwenzi wako mbele. Vyovyote vilivyo vyema kwao, vitakuwa vyema kwako pia.

KUTAWALA HASIRA “‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado

KUTAWALA HASIRA “‘Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka. ”(Waefeso 4: 26 -27) Ni wakati gani hasira huwa dhambi? Hasira isiyo ya haki ambayo hutoka kwenye ubinafsi ni dhambi dhidi yao wanaoitoa. Kama hasira ya haki ikiimarika, hatimaye huwa chuki, ambayo ni dhambi pia. Paulo anatutia moyo kutotunza hasira, lakini kutatua ugomvi kabla siku haijaisha. Unaweza ukawa na sababu nzuri ya kukasirika, lakini usiitumie kama udhuru wa kuendelea kuwa hivyo. Waombee wale wanaokuumiza, wasamehe na uwe mbaraka kwao.

UPENDO WA KWELI “Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. ” (Wakolosai

UPENDO WA KWELI “Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. ” (Wakolosai 3: 19) Baadhi ya watu wanadhana potofu ya upendo. Wanafikiri kwamba kadri wanavyowapenda wenzi wao, ndivyo wanavyolazimisha dhamira zao kwamba wenzi wao ni wenye furaha. Wanaweza kutumia vurugu au kuwalazimisha kufanya hivyo. Upendo wa kweli haulazimishi wala kuleta vurugu. Huiga upendo wa Mungu. Haukasirishwi kwa haraka. Hauweki akiba ya makosa. Haupendezwi na uovu. Daima huwa unahifadhi (1 Kor. 13; 1 Yoh. 4: 7 -8). Pale upendo wa kweli unapotawala, huduma ya kuheshimiana inakuwa jambo la kawaida. Pande zote zinahisi kuwa na ulinzi na usalama.

UMUHIMU WA MSAMAHA “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani watu wote, na huo utakatifu,

UMUHIMU WA MSAMAHA “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. ” (Waebrainia 12: 14) Mtume Paulo anatushauri kuwa na amani na watu wote, zaidi ya kuwa na wasi (Warumi 12: 18). Ni kwa namna gani hii inahusiana na msamaha? Kama tumesababisha kosa, lazima tukiri hatia zetu na kwa dhati kabisa kuomba msamaha. Kama mtu fulani ametukosea, ni lazima tusamehe hata kama hataki kuomba msamaha. Kama Mungu alitusamehe sisi, je, haitupasi kuwasemehe wengine pia (Matayo 18: 21 -35)? Lengo letu daima liwe kurejesha mahusiano yaliyovunjika, hivyo kuirejesha tena amani kwao.

“Kama mapenzi ya Mungu yametimizwa, mume na mke wataheshimiana kila mmoja na kuuzidisha upendo

“Kama mapenzi ya Mungu yametimizwa, mume na mke wataheshimiana kila mmoja na kuuzidisha upendo na kujiamini. Chochote kitakachoharibu amani na umoja wa familia lazima kiangamizwe kabisa, na wema na upendo lazima ufurahiwe kwa ubora kabisa. Yeye ambaye huiweka wazi roho ya huruma, uvumilivu, na upendo, roho ya namna hiyo itamrudia. Mahali Roho wa Mungu anapotawala, hapatakuwa na mazungumzo yasiyofaa katika mahusiano ya ndoa. Kama kweli Kristo atakuwa ndani yetu, tumaini la utukufu, kutakuwa na mwunganiko na upendo katika nyumba. Kristo anayedumu katika moyo wa mke atakubaliana na Kristo anayedumu katika moyo wa mume. Watakuwa wanajitahidi pamoja kwa ajili ya nyumba Kristo alizoenda kuandaa kwa ajili ya wale wampendao. ” E. G. W. (Counsels for the Church, cp. 21, p. 131)