JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALMASHAURI YA WILAYA

  • Slides: 56
Download presentation
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI

TAARIFA YA IDARA KIKAO CHA WADAU WA ELIMU. TAREHE 10/1/2018. • UTANGULIZI • Idara

TAARIFA YA IDARA KIKAO CHA WADAU WA ELIMU. TAREHE 10/1/2018. • UTANGULIZI • Idara ya elimu sekondari kwa pamoja na Idara ya Elimu Msingi zilishiriki katika kikao cha wadau wa elimu wilaya kilichofanyika tarehe 5/1/2017, ambapo wadau mbali wa elimu wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Shule za Sekondari na Wakuu wote wa Shule za Msingi, Waratibu Elimu Kata , na Wadhibiti ubora wa Shule wa Wilaya walishiriki kikao hiki muhimu. Pia alikuwepo Mbunge wa jimbo la mpwapwa mjini Mh: George Malima Lubeleje, Mkuu wa Wilaya ya mpwapwa Mh: Jabir Shekimweri na Mgeni rasmi alikua aliekuwa naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi aliekua akishughulikia Elimu ndugu Bernad Makali.

YATOKANAYO NA KIKAO CHA WADAU KILICHOFANYIKA TAREHE 5/1/2017 • Katika kikao cha wadau kilichopita

YATOKANAYO NA KIKAO CHA WADAU KILICHOFANYIKA TAREHE 5/1/2017 • Katika kikao cha wadau kilichopita Katibu Mkuu Tamisemi pamoja na wadau mbali hawakufurahishwa na Hali ya elimu kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita , nakutaka mikakati madhubuti iwekwe na isimamiwe ili kubadili hali ya ufaulu kwa upande wa idara zote za elimu, baadhi ya Maazimio yaliyowekwa ni kama ifuatavyo-:

YATOKANAYO NA KIKAO CHA WADAU KILICHOFANYIKA TAREHE 5/1/2017 • 1 Idara kwa kushirikiana na

YATOKANAYO NA KIKAO CHA WADAU KILICHOFANYIKA TAREHE 5/1/2017 • 1 Idara kwa kushirikiana na wadau wa elimu wahakikishe wanakuja na mbinu mbadala za kupambana na mimba mashuleni na kutoa elimu kwa wanafunzi na wazazi juu ya madhara ya mimba za utotoni, na kuhakikisha watuhumiwa na wahusika wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. • 2. Kusimamia nidhamu za watumishi (walimu)na kuchukua hatua kali dhidi ya walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi pia agizo lilitolewa la kuchukua hatua kwa mwalimu John Daud wa Wotta Sekondari aliyetuhumiwa kumpatia mimba mwanafunzi.

3. Kuwaondoa katika nafasi zao Wakuu wa shule wasio jituma na wazembe wanaochangia matokeo

3. Kuwaondoa katika nafasi zao Wakuu wa shule wasio jituma na wazembe wanaochangia matokeo mabaya ya shule zao. 4. Ilishauriwa kuwepo na mkakati wa kuwahamisha walimu wa ziada waliopo katika shule za mijini kwa kuwapeleka katika shule za vijijini zilizo na upungufu wa walimu. • 5. Afisa Elimu Sekondari aliagizwa kufuatilia utendaji kazi wa Mkuu wa Shule Chinyika Sekondari ambae ilisemekana hakai kituoni, hivyo kupelekea maendeleo mabaya na hasa utoro wa wanafunzi wanaotoka kijiji cha Chaludewa, na walimu wanaoishi mbali na shule wakati zipo nyumba za walimu zisizokaliwa na walimu na badala yake mkuu wa shule amezigeuza kuwa mabanda ya kuku.

6. Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ndugu Jabir Shekimweri alitoa agizo la kuanzisha Debate Clubs

6. Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ndugu Jabir Shekimweri alitoa agizo la kuanzisha Debate Clubs na kuahidi kuwa atazifadhili clubs hizo. 7. Utoaji huduma Ofisini ufanyike kwa haki na kwa watendaji kutimiza wajibu wao, badala ya kutoa lugha za kebehi kwa wateja wao, na kuondoa urasimu katika kutoa huduma. • 8. Maafisa kutembelea na kukagua shule , badala ya kukaa ofisini 9. Kushirikiana na wadau mbali kuhakikisha suala la ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara vinakamilishwa kila shule

10. Kuhakikisha kunakuwepo na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kuwa ufaulu wa mitihani ya

10. Kuhakikisha kunakuwepo na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kuwa ufaulu wa mitihani ya kidato cha pili na cha nne unapanda na kufikia lengo la BRN asilimia 71% kwa kidato cha pili na cha nne

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WADAU WA ELIMU 2017 Idara ya elimu Sekondari kwa kushirikiana

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WADAU WA ELIMU 2017 Idara ya elimu Sekondari kwa kushirikiana na wadau wengine kama Madiwani na Waratibu Elimu wa Kata wamesimamia na kutekeleza agizo la kupambana na mimba shuleni, kwa kubuni mbinu mbali, ikiwemo mpango wa kuanzisha clubs za wasichana Girls CLUBS ambazo zitasaidia sana kuwaweka wasichana pamoja. kumekuwepo na juhudi za makusudi za kuwapatia wasichana elimu juu ya madhara ya mimba za utotoni na namna ya kukabiliana na vishawishi juu ya watu wasio na nia njema.

Timu ya Maafisa wanawake kutoka wilayani ilifika Shule ya Wasichana Mazae tarehe 4/12/2017 na

Timu ya Maafisa wanawake kutoka wilayani ilifika Shule ya Wasichana Mazae tarehe 4/12/2017 na kuzungumza na wasichana juu ya masuala mbali yanayowawezesha kujitambua kwa kuepuka mimba za utotoni na kujiwekea malengo ya kutimiza ndoto za baadae, zoezi hiili ni zoezi endelevu, wanafunzi wengi walivutiwa na ziara hii, na walikiri kutokufahamu mambo mengi, na kuwaomba maafisa kurudi tena.

Kumekuwepo na zoezi endelevu la kuwapima ujauzito wasichana mara kwa mara kila wanapotoka likizo

Kumekuwepo na zoezi endelevu la kuwapima ujauzito wasichana mara kwa mara kila wanapotoka likizo na kila baada ya miezi mitatu, hali hii inasaidia kwanza kuwafanya wanafunzi wakike kuwa makini, lakini pia inasaidia idara kupata takwimu juu ya idadi ya wanafunzi wajawazito. Idara imesimamia uteuzi wa walimu wa malezi kwa kila shule, na kutoa msisitizo juu ya walimu hawa ambao ni wanawake pia kujenga utamaduni wakuwasaidia wanawake wenzao kufikia malengo yao, kwani wengi wao wamekuwa kwa muda mrefu hawana msaada katika kuwasaidia wanafunzi wa kike kujitambua, na kuepuka mimba za utotoni. Jamii imesisitizwa kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahalifu wanaotembea na wanaowapa mimba wanafunzi.

Mwalimu alietuhumiwa kumpa mwanafunzi ujauzito Wotta sekondari aliachiwa huru na mahakama baada ya ushahidi

Mwalimu alietuhumiwa kumpa mwanafunzi ujauzito Wotta sekondari aliachiwa huru na mahakama baada ya ushahidi kukosekana .

2. Agizo la kusimamia nidhamu za watumishi limefanyika ambapo watumishi kumi na nne waliandikiwa

2. Agizo la kusimamia nidhamu za watumishi limefanyika ambapo watumishi kumi na nne waliandikiwa barua za onyo kwa uzembe kazini na nakala za barua zao aliandikiwa Mh, Mkuu wa wilaya, ambapo watumishi watano wamefikishwa mbele ya tume ya maadili ya walimu (TSC), ambapo mashauri yao yakinidhamu yanaendelea kusikilizwa ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa. Jedwali A, linaonesha idadi ya walimu walioandikiwa barua za maonyo na shule wanazotoka.

JEDWALI A. WALIMU WALIOPEWA BARUA ZA ONYO NA WALIOPO CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SN

JEDWALI A. WALIMU WALIOPEWA BARUA ZA ONYO NA WALIOPO CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SN JINA LA SHULE IDADI YA WALIMU 1 IHALA 6 2 MT IGOVU 01 3 VINGHAWE 02 4 03 5 MATOMONDO KIMAGHAI 6 PWAGA 01 7 MTERA 02 01

08 CHUNYU 03 09 KIBAKWE 02 10 BEREGE 01

08 CHUNYU 03 09 KIBAKWE 02 10 BEREGE 01

Aidha ni vyema ikafahamika kuwa barua za onyo zinaweza kuwanyima haki ya kupanda madaraja

Aidha ni vyema ikafahamika kuwa barua za onyo zinaweza kuwanyima haki ya kupanda madaraja na vyeo walimu waliopewa barua hizo. Kutokana na hatua hizi zilizochukuliwa zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa utendaji kazi miongoni mwa walimu wengine na hivyo kupelekea matokeo mazuri ya mitihani ya moko kwa kidato cha pili na cha nne 2017, mitihani ambayo ni kipimo cha matokeo ya mtihani wa taifa kwa kidato cha pili na nne kwa mwaka huu. 3. Agizo la tatu lilikuwawajibisha wakuu wa shule wasiotimiza wajibu wao, Hadi sasa Idara imemvua madaraka Mkuu mmoja wa Shule ya Sekondari Matomondo kwa utovu wa nidhamu na kwa kushindwa kuwaweka pamoja watendaji waliochini yake na hivyo kusababisha mpasuko na makundi katika kituo chake cha kazi. Ifahamike kuwa mahali pasipo na umoja hakuna mafanikio kwani pia hakuna utendaji.

Hata hivyo idara imeendelea kuratibu na kuwabaini wakuu wa shule wazembe ambapo mapendekezo yakufanya

Hata hivyo idara imeendelea kuratibu na kuwabaini wakuu wa shule wazembe ambapo mapendekezo yakufanya mabadiliko ya wakuu wa shule yatawasilishwa kwa Afisa Elimu Mkoa ambae ni Katibu Tawala Msaidizi Elimu kwa hatua zaidi. Aidha kwa kiasi kikubwa baada ya Idara kufanya vikao vya mara kwa mara na wakuu wa shule na kuwapatia maelekezo mbali juu ya namna ya kusimamia shule na kuweka mikakati imara ya kuongeza ufaulu katika maeneo ya kazi hali imebadilika kwa kiasi kikubwa. Kwa mwaka huu, idara imefanya vikao vipatavyo vi nne vya kazi na kuna dalili kubwa za matokeo mazuri ya mitihani ya Taifa kwa vidato vya pili na nne. Kiambata A kinaonesha shule zilizokuwa na ufaulu wa chini mwaka 2016 kwa mitihani ya ya Taifa kidato cha pili na jinsi zilivyoongeza ufaulu kwa mwaka 2017 katika Mitihani ya Taifa kidato cha nne cha pili. wakati kiambata B kinaonesha shule zilizoshuka kwa ufaulu mwaka 2017

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI SHULE ZILIZOPANDISHA UFAULU FTNA 2017

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI SHULE ZILIZOPANDISHA UFAULU FTNA 2017 KIAMBATA A. JINA LA SHULE 1 CHIPOGORO SS 2 QEEN ESTHER SS 3 MAZAE 4 MPWAPWA SS 5 GODE SS 6 MATOMONDO 7 MOUNT IGOVU SS 8 IKUYU SS 9 IHALA SS 11 IPERA SS 12 RUDI SS 13 BEREGE JUMLA DARAJA LA I-IV 2016 DARAJA LA I-IV 2017 M F T % 15 10 25 100. 0 15 21 36 100 0 68 68 100. 0 33 100 0 49 49 95. 9 0 49 49 100 88 97. 8 0 95 95 98 18 15 33 97. 1 12 23 35 97 29 17 46 92. 0 29 29 58 98 58 58 116 91. 3 58 54 80 92 12 16 28 90. 3 12 32 18 94 56 55 111 89. 5 56 46 49 95 40 46 86 86. 9 40 46 86 96 15 18 33 82. 5 15 23 36 97 48 46 94 94. 6 50 46 96 99 794 838 1632 92. 886 794 838 1632

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI SHULE ZILIZOSHUKA KWA UFAULU FTNA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA IDARA YA ELIMU SEKONDARI SHULE ZILIZOSHUKA KWA UFAULU FTNA 2017 KIAMBATA B NA : JINA LA SHULE DARAJA I-IV 2016 DARAJA I-IV 2017 M F T % 1 CHINYIKA 19 10 29 100. 0 19 10 29 96 2 MIMASS 16 28 44 100. 0 16 28 44 90 3 MASA SS 19 27 46 97. 9 19 27 46 81 4 LUHUNDWA SS 30 15 45 97. 8 30 15 45 93 5 PWAGA SS 53 42 95 90. 5 53 42 95 90 6 VINGHAWE SS 28 29 57 89. 1 28 29 57 88 7 MBUGA SS 19 33 52 86. 7 19 33 52 83 8 KIMAGHAI 40 49 89 95. 9 52 79 131 87 9 CHUNYU 17 23 40 92. 0 21 17 38 89. 5 10 WOTTA 53 64 117 94. 4 51 67 118 89. 8 11 KIBAKWE 65 90 155 95. 9 63 81 144 93. 8 JUMLA 794 838 1632 92. 8856 794 838 1632

4. Agizo la nne lilikuwa kuhamisha walimu waliozidi mijini na kuwapeleka maeneo ya vijijni,

4. Agizo la nne lilikuwa kuhamisha walimu waliozidi mijini na kuwapeleka maeneo ya vijijni, Idara ya elimu Sekondari imefanikiwa kuhamisha walimu saba kutoka maeneo mbali, na mwalimu mmoja tu kutoka Shule ya Sekondari vinghawe iliyopo mjini, na kumpeleka Shule ya Sekondari Matomondo, kutokana na sababu mbali ikiwemo ukata , kama inavyojieleza katika jedwali hapo chini. JEDWALI B

S/N KITUO HATUA ILIYO ALICHOPENDEKEZ FIKIWA WA KUHAMIA 01 AISACK KILENDYA VINGHAWE MATOMONDO AMEHAMIA

S/N KITUO HATUA ILIYO ALICHOPENDEKEZ FIKIWA WA KUHAMIA 01 AISACK KILENDYA VINGHAWE MATOMONDO AMEHAMIA 02 RICHARD MALIMBA MT IGOVU KIBAKWE AMEHAMISHIW A, OFISI YA MKAGUZI WA NDANI 03 THERISIA YUST IHALA MATOMONDO AMEHAMIA MKOA WA ARUSHA, HAKUR IPOTI KITUO ALICHOHAMISH IWA 04 RICHARD MLULU RUDI BEREGE AMEHAMIA 05 ISDIDORY MICHAEL IPERA BEREGE AMEHAMIA 06 NELSON NYAOMBO KIBAKWE MASSA UHAMISHO UMESITISHWA 07 SALAMA CASMIR RUDI KIBAKWE AMEHAMIA

S/N JINA LA MWALIMU KITUO HATUA ILIYO ALICHOPENDE FIKIWA KEZWA KUHAMIA 08 ASHA NYANGARIKA

S/N JINA LA MWALIMU KITUO HATUA ILIYO ALICHOPENDE FIKIWA KEZWA KUHAMIA 08 ASHA NYANGARIKA LUHUNDWA KIBAKWE AMEHAMIA 09 FORTUNATA KUSUDYA IKUYU KIBAKWE AMEHAMIA

Uhamisho huu umesaidia kurekebisha ikama katika vituo husika na hasa kuimarisha nguvu kwa shule

Uhamisho huu umesaidia kurekebisha ikama katika vituo husika na hasa kuimarisha nguvu kwa shule ya Sekondari Kibakwe ambayo ni ya kidato cha Tano na Sita. • 5. Afisa Elimu Sekondari aliagizwa kufuatilia utendaji wa kazi wa Mkuu wa Shule Chinyika Sekondari, juu ya tuhuma zakutokukaa kituoni. Katika ziara ya kustukiza iliyofanywa na Maafisa kutoka Halmashauri ilibaini kuwa mkuu wa shule yupo kituoni, uthibitisho wa kitabu cha mahudhurio na mahojiano na walimu vilidhihirisha kuwa Mkuu wa Shule yupo kituoni. • Kuhusu suala la nyumba za walimu kutumika kufugia kuku, ilibainika kuwa nyumba zote zinakaliwa na walimu na kuku wanafugwa na walimu wanaoishi katika nyumba hizo, • 6. Agizo la tano lilitolewa na Mhesh. Mkuu wa Wilaya ndugu Jabir Shekimweri ambae alitaka shule zote za Sekondari kuunda Debate Clubs ambazo angetoa ufadhili, hatua

iliyofikiwa ni kuwa kila shule ina debate club na debate hufanyika mara moja kwa

iliyofikiwa ni kuwa kila shule ina debate club na debate hufanyika mara moja kwa wiki kati ya jumatano na ijumaa jioni kulingana na utaratibu wa kila shule vile kila shule imeunda subjects clubs na asilimia Kubwa ya shule zote 25 za Sekondari za Serikali zina clubs za Rushwa. 7. Agizo lililotolewa na Mgeni Rasmi ni namna watendaji wa idara wanavyohusiano na wateja wao Kwa maana ya watu wanaoitaji huduma Idara ya Elimu Sekondari imeendelea kuweka rekodi yakuwa na mahusiano mazuri na watendaji waliochini yake kwakuendelea kutoa huduma bora kwa kila mtu bila upendeleo na kufuata sheria na taratibu za kazi , aghalabu hakuna malalamiko yoyote yaliyofikishwa katika ofisi ya malalamiko yakihusu rushwa , upendeleo unyanyasaji wa aina yoyote, wala urasimu katika utoaji wa huduma.

Idara itaendelea kutoa huduma bora na kwa wakati hasa ikizingatiwa wateja wengi wanatoka maeneo

Idara itaendelea kutoa huduma bora na kwa wakati hasa ikizingatiwa wateja wengi wanatoka maeneo ya vijiji vya mbali hivyo kuitaji huduma mapema na kwa wakati ili wawahi kurudi katika maeneo ya kazi. Aidha watendaji wote Idarani wamekuwa wakipatikana kabla ya saa moja kamili asubuhi na si zaidi ya saa moja na nusu asubuhi.

8. Agizo la nane kutoka kwa mgeni rasmi lilikuwa kwa Maafisa kutokukaa ofisini badala

8. Agizo la nane kutoka kwa mgeni rasmi lilikuwa kwa Maafisa kutokukaa ofisini badala yake watembelee shule na kuzikagua , agizo hili lilifanyiwa kazi licha ya ukata uliokuwa ukiikabili Idara ya Elimu Sekondari, na Shule zipatazo 20 kati ya 27 zilitembelewa shule ambazo hazikutembelewa ni Wotta , Rudi, Ipera Queen Esther , Aglam , Ikuyu, Mbuga na Matomondo, Idara imejipanga kwa kiwango cha juu kabisa kuhakikisha kuwa kipindi cha mwaka ujao wa 2018 shule zote za binafsi na serikali zinatembelewa na kukaguliwa mara kwa mara, . kwa mwaka 2017 kila afisa idarani alipatiwa shule za mjini za kukagua mara kwa mara bila ratiba maalumu na ndipo walimu wazembe walipobainika. Kazi ya kutembelea shule hizi kumeleta mafanikio makubwa sana kwani ilibainika kuwa walimu wengi ni wazembe na hawajitumi kazini hivyo kuwachukulia hatua mbali za kinidhamu waliobainika na hali kwa sasa ni tofauti kabisa. Idara imeshirikiana na idara ya wadhibiti ubora katika kazi hiyo.

9. Agizo la tisa lilikuwa kushirikiana na wadau mbali kuhakikisha kila shule ya sekondari

9. Agizo la tisa lilikuwa kushirikiana na wadau mbali kuhakikisha kila shule ya sekondari inakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara, agizo hili limetekelezwa kiasi, na tayari maabara 6 kati ya maabara 72 zinazohitajika zimekamilika kwa idadi ya vyumba viwili na zinatumika. Idara kwa kushirikiano na wadau wa Haki Elimu walifanya kikao cha pamoja kilichowaweka pamoja wadau wote kama Waratibu, Walimu wakuu na Wakuu wa Shule na Madiwani wa kata za Pwaga, na Vinghawe mwezi April 2017, na baadae mwezi Novemba Idara kwa kushiriana na wadau wa Haki Elimu, ikaendesha kikao cha Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Vinghawe na Diwani wa Kata ya Vinghawe ambapo elimu juu ya umuhimu wa Maabara na umuhimu wa uchangiaji wa Maabara ulitolewa kwa wananchi. Wadau wa Haki Elimu wa aliahidi kuchangia gharama za ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara endapo wananchi watajitoa na kuanzisha ujenzi huo.

imeahidi bati za kukamilisha ujenzi huo, Idara kupitia kitengo cha Takwimu imeendelea kuratibu na

imeahidi bati za kukamilisha ujenzi huo, Idara kupitia kitengo cha Takwimu imeendelea kuratibu na kushauri umuhimu wa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya Maabara kwani Serikali imetoa vifaa vyote vya Maabara kwa Shule zilizokamilisha ujenzi wa vyumba va Maabara, kwa shule zote Nchini hii imekuwa chachu na ndio njia kuu ambayo imeendelea kutumika kuhamasisha ujenzi wa Maabara kwani pale ujenzi unapo kamilika Serikali inatoa vifaa vyote na kupunguza gharama ya ununzi wa vifaa kwa kiasi kikubwa sana. Jedwali na C hapo chini linaonesha shule zilizokamilisha maabara na shule zilizopewa vifaa wakati jedwali na D linaonesha hatua mbali za ujenzi wa Maabara zizofikiwa, katika kata zote wilaya ya mpwapwa na orodha ya shule zilizopata mgao wa vifaa vya maabara baada ya kukamilisha ujenzi.

S/N JINA LA SHULE VYUMBA VILIVYOKAMI LIKA 1 MAZAE 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA

S/N JINA LA SHULE VYUMBA VILIVYOKAMI LIKA 1 MAZAE 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA 2 PWAGA 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA 3 CHUNYU 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA 5 CHINYIKA 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA 6 MPWAPWA 3 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA 7 WOTTA 2 WAMEPATIWA VIFAA VYA MAABARA

SN JINA SHULE 1 2 Berege 3 4 5 6 Chinyika Chipogoro Chunyu Godegode

SN JINA SHULE 1 2 Berege 3 4 5 6 Chinyika Chipogoro Chunyu Godegode Ihala 7 Ikuyu 8 9 10 11 Ipera Kibakwe Kimagai Luhundwa 12 Massa 13 Matomondo 14 15 16 17 18 19 20 21 22 Mazae Mbuga Mima Mount Igovu Mpwapwa Mtera Dam Mwanakianga Pwaga Rudi 23 Ving'hawe HATUA YA ILIYOFIKIWA UJENZI 2 Kuta zimekamilika na 1 haijaanza kujengwa. kuta zimekamilika 2 usawa wa madirisha na 1 haijaanza kujengwa. 1 kuta zimekamilika na 1 iko hatua ya msingi. 2 Zimepauliwa na 1 haijanza kujengwa 3 kuta zimekamilika 1 iko hatua ya kupaua 2 kuta zimekamilika na 1 iko hatua ya msingi. 1 kuta zimekamilika, 1 iko hatua ya msingi na 1 haijaanza kujengwa. 2 ziko usawa wa madirisha na 1 haijaanza ujenzi. Moja Haijaanza kujengwa 3 ziko hatua ya kupiga paa. 2 ziko hatua ya paa na 1 haijaanza kujengwa. 3 ziko hatua ya msingi. 2 kuta zimekamilika na 1 iko hatua ya msingi. 3 ziko hatua ya msingi. 2 zimekamilika na 1 haijanza kujengwa. 2 kuta zimekamilika na 1 haijaanza kujengwa.

10. Agizo la kumi lilikuwa kuweka mikakati mbali ya kuinua ufaulu kwa lengo la

10. Agizo la kumi lilikuwa kuweka mikakati mbali ya kuinua ufaulu kwa lengo la kufikia malengo ya BRN ya asilimia 71 ya Ufaulu kwa kidato cha pili na cha nne. Hatua mbali za kuwakutanisha wadau wote wa elimu zilifanyika ikiwemo kufanya tathimini ya matokeo ya mitihani kwa mwaka 2015 na sababu za Wilaya kutofikia asilimia 71, kwa kidato cha nne zilibainishwa, kama ifuatavyo-: a) Usimamizi duni wa Wakuu wa shule , ambapo Wakuu wengi wa shule si wabunifu, na wameshindwa kuwaweka walimu pamoja, wakati mwingi pia wameshindwa kuwepo vituoni.

b. ) Uzembe wa hali ya juu wa walimu, kutowajibika ipasavyo c). Utoro wa

b. ) Uzembe wa hali ya juu wa walimu, kutowajibika ipasavyo c). Utoro wa reje reja wa walimu na wanafunzi d). Kutomaliza mada kwa wakati e. ) Kuwepo mazoezi machache sana, au hakuna kabisa f. ) Mitihani michache ya maandalizi kwa ajili ya wanafunzi kidato cha pili na nne g. ) Kutokuwepo na mitihani ya ushindani kwa wanafunzi ushirikianao duni wa wazazi na shule h). Waratibu Elimu Kata kutoshiriki kutoa mawazo wala ufuatiliaji wa Shule za Sekondari i. ) Shule nyingi kukosa Maabara j. ) Upungufu wa walimu kwa masomo ya sayansi k. ) Kutokuwepo na programu ya chakula shuleni

Baada ya kuzibaini changamoto hizi idara ilianza haraka utaratibu wa kuzifanyia kazi changamoto hizi

Baada ya kuzibaini changamoto hizi idara ilianza haraka utaratibu wa kuzifanyia kazi changamoto hizi ikiwemo kukutana na wakuu wa shule mara nne kwa kipindi cha mwaka jana na kuwekeana mikakati mbali ya kutatua changamoto hizi ilikuinua ufaulu, licha ya hatua mbali zilizochukuliwa katika kufikia malengo ya asilimia 71 ya ufaulu, matokeo ya mtihani ya kidato cha pili kwa mwaka 2016 yalionekana kupanda na kuvuka malengo ya BRN kwa ufaulu wa asilimia 92, sambamba na mwaka jana 2017 kwa ufaulu kama huo , wakati matokeo ya mtihani kidato cha nne yalikuwa 42 %kutoka asilimia 52% ya mwaka 2015 kama jedwali E linavyo onesha hapo chini. JEDWALI E HALI YA UFAULU KWA KIDATO CHA NNE KWA MWAKA 2015/2016

MWA KA WALI OFA NYA % WASI % OFA NYA DV DVII DV IV

MWA KA WALI OFA NYA % WASI % OFA NYA DV DVII DV IV DV O WALI % OFA ULU WALI % OSHI NDW A I 2015 1622 1565 96 24 4 18 58 110 309 755 48 810 52 2016 1472 1432 97 40 3 28 40 149 620 595 837 58 595 42

JEDWALI F HALI YA UFAULU KWA KIDATO CHA PILI KWA MWAKA 2015/2016/2017 MWAKA 2015

JEDWALI F HALI YA UFAULU KWA KIDATO CHA PILI KWA MWAKA 2015/2016/2017 MWAKA 2015 WALIOF ANYA DV DVII DV IV DV O I WALIOFAU LU % WALIOFELI % 1506 99 241 898 KWA 131 1375 91. 3 PILI 131 KWA 8. 7 JEDWALI F HALI 137 YA UFAULU KIDATO CHA MWAKA 2015/2016 126 95 145 277 1112 124 1629 92. 7 128 7. 28 2017 1870 104 170 334 1107 151 1719 92 151 2

NAFASI ZA SHULE KIWILAYA MATOKEO MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE 2016 Katika mtihani

NAFASI ZA SHULE KIWILAYA MATOKEO MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE 2016 Katika mtihani wa Taifa kidato cha Nne mwaka 2016 zipo shule kumi duni na kumi bora kiwilaya zilizopangwa kwa mgawanyo ufuatao. JEDWALI G SHULE KUMI BORA CSEE 2016

SN JINA LA SHULE 1 MPWAPWA 2 MTERA 3 QUEEN ESTHER 4 BEREGE 5

SN JINA LA SHULE 1 MPWAPWA 2 MTERA 3 QUEEN ESTHER 4 BEREGE 5 KIMAGHAI 6 MADANYA 7 IPERA 8 LUHUNDWA 9 KIBAKWE 10 CHUNYU

Jedwali H Hapo shule linaonesha shule kumi duni kiwilaya kwa mitihani ya kidato cha

Jedwali H Hapo shule linaonesha shule kumi duni kiwilaya kwa mitihani ya kidato cha nne 2016. JEDWALI H 1 MASSA 2 RUDI 3 GODE 4 IKUYU 5 CHIPOGORO 6 CHUNYU 7 MBUGA 8 PWAGA 9 VINGHAWE 10 WOTTA

NAFASI YA WILAYA KATIKA MKOA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016 Wilaya ya mpwapwa imeendelea

NAFASI YA WILAYA KATIKA MKOA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016 Wilaya ya mpwapwa imeendelea Kubaki katika Nafasi ya Tano katika matokeo ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Nne kwa mwaka 2016 kama ilivyokuwa mwaka 2015. Katika Halmashauri Nane za Mkoa wa Dodoma.

MATOKEO YA MITIHANI YA MOKO KIDATO CHA NNE NA PILI MWAKA 2017 NA MUELEKEO

MATOKEO YA MITIHANI YA MOKO KIDATO CHA NNE NA PILI MWAKA 2017 NA MUELEKEO WA UFAULU KIDATO CHA NNE NA PILI MWAKA 2017 Katika mitihani ya moko iliyofanyika kimkoa kwa kidato cha pili na cha nne mwaka 2017 hali ya kupanda kwa ufaulu inaonekana kwa upande wa vidato vyote viwili , Ni matumaini ya Idara kuwa kwa mwaka huu Ufaulu wa Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne yataongezeka kwani mitihani ya moko huakisi matokeo ya mitihani ya Taifa.

UFAULU MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE 2017 UKILINGANISHA NA MWAKA 2016. JEDWALI I

UFAULU MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE 2017 UKILINGANISHA NA MWAKA 2016. JEDWALI I MWA KA WALI OSAJI LWA WALI OFAN YA % WASI OFAN YA % 2016 1622 1542 95. 06 80 0. 4 2017 1301 1209 92. 92 92 7. 071 DV DVII DV IV DV O WALI OFAU LU % WALI OSHI NDW A % 50 123 207 477 685 857 55. 57 685 44. 4 67 103 132 589 318 891 73. 69 318 26. 3 I

MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE MWAKA 2017. WATAHINIWA WALIOFANYA NA WASIO FANYA MTIHANI

MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE MWAKA 2017. WATAHINIWA WALIOFANYA NA WASIO FANYA MTIHANI WA CSEE 2017 Wanafunzi 54 kati ya wanafunzi 1042 waliosajiliwa kufanya mtihani wa Kidato cha nne hawakuweza kufanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari kutokana na sababu mbali ambapo wanafunzi 14, hawakuwezi kufanya mtihani huo kwa sababu ya mimba, wakati 29, ilisababishwa na utoro, 3 ugojwa na 3 sababu nyinginezo. Jedwali J hapo chini linaonesha idadi ya wanafunzi walioanza kidato cha kwanza mwaka 2014, na waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017.

SHULE WALIOANZA KDT CHA 1 2014 WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI 2017 WALIOFANYA MTIHANI 2017 WASIOFANYAKATI

SHULE WALIOANZA KDT CHA 1 2014 WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI 2017 WALIOFANYA MTIHANI 2017 WASIOFANYAKATI YA WALIOSAJILIWA BEREGE 57 60 117 30 31 61 30 30 60 0 1 1 CHINYIKA 19 4 23 15 2 17 0 0 0 CHIPOGORO 13 9 22 10 5 14 10 4 14 0 1 1 CHUNYU 31 22 53 20 15 35 0 0 0 GODE 13 15 28 6 7 13 0 0 0 IHALA 45 74 119 40 40 80 40 37 77 00 3 3 IKUYU 17 12 29 12 5 17 12 4 16 0 1 1 IPERA 47 54 101 33 31 64 0 0 0 KIBAKWE 114 87 201 60 81 141 59 76 135 1 5 6 KIMAGHAI 34 34 65 23 20 43 21 18 39 2 2 4 LUHUNDWA 23 18 41 10 13 23 10 10 20 0 3 3 MASSA 32 18 50 16 9 25 00 0 0

MATOMON DO MAZAE 01 0 04 04 0 0 0 0 00 01 05

MATOMON DO MAZAE 01 0 04 04 0 0 0 0 00 01 05 0 0 0 0 01 06 MBUGA 01 0 0 01 01 MIMA 0 0 01 0 0 0 01 MT IGOVU 04 01 0 02 04 6 MPWAPWA 0 03 0 0 0 03 0 3 MTERA DAM 0 0 0 0 MWANAKIA NGA PWAGA 0 01 01 02 0 0 0 01 01 2 01 0 03 03 0 0 0 04 4 RUDI 0 0 0 0 VINGHAWE 0 0 0 02 02 0 2 WOTTA 0 01 02 03 0 0 0 01 02 3 MADANYA 0 0 0 0 01 01 01 QUEEN ESTHER JUMLA KUU 0 0 01 01 14 14 20 29 2 1 3 18 36 54

MIKAKATI ILIYOFANYWA ILI KUNYANYUA UFAULU KWA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI NA NNE 2017.

MIKAKATI ILIYOFANYWA ILI KUNYANYUA UFAULU KWA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI NA NNE 2017. Baada ya matokeo yasiyoridhisha ya mwaka 2016 Idara imefanya vikao vya wadau mbali na wakuu wa shule kwa jumla ya vikao vitano vya kazi na kutembelea shule zote ishirini na sita, Mkakati wa kuzitambua shule zenye watahiniwa wengi na kutembelea mara kwa mara ulifanywa. Aidha katika kikao kilichofanyika tarehe wakuu wa shule na Idara walikubaliana kununa mashine za kuzalishia mitihani ili wilaya iweze kuwa na mitihani mingi ya maandalizi jambo lililofanikiwa na kuwezesha kwa kipindi cha mwaka huu kufanyika mitihani ya moko pre national na mitihani ya ndani ya utimilifu wa ufundishaji.

Katika ukaguzi wa mwisho uliofanyika katika vituo kumi na saba kati ya vituo 26

Katika ukaguzi wa mwisho uliofanyika katika vituo kumi na saba kati ya vituo 26 sawa na asilimia 65 ya vituo vyote ilionesha ufundishaji wa mada za masomo umekamilika kwa asilimia moja. Kila shule iliweza kufanya mitihani minne ya maandalizi iliyoandaliwa kwa weledi kwa ngazi ya wilaya na mtihani wa moko Mkoa uliondaliwa kwa ngazi ya mkoa. Tuna amini matokeo yatakuwa mazuri mwaka huu kwani mara nyingi matokeo ya mitihani ya moko hutofautiana kidogo na matokeo ya mwisho.

MIKAKATI YA KUONGEZA UFAULU KWA MWAKA 2018 • Kuanzia January mwaka huu idara imejipanga

MIKAKATI YA KUONGEZA UFAULU KWA MWAKA 2018 • Kuanzia January mwaka huu idara imejipanga kwa kiwango cha juu kuhakikisha kuwa matokeo ya mitihani kwa vidato vyote vya mitihani yanakuwa mazuri , kwa kushika nafasi za juu katika Mkoa na hata Taifa. • Ifuatatayo ni mikakati iliyowekwa ili kupandisha ufaulu kwa mwaka 2018 • 1. Ufuatilaiji wa karibu sana wa ufundishaji kwa shule zote , Idara imejipanga vilivyo kwakutumia maofisa wake na maofisa wa ukaguzi wa elimu wilaya kuhakikisha suala la ufundishaji kinasimamiwa kwakaribu kuliko kipindi kingine kilichowahi kutokea • 2. Kuwashirikisha Waratibu Elimu Kata kwa asilimia moja katika suala zima la ufuatiliaji wa ufundishaji na Usimamizi wa shule.

3. Kuwaandikisha mikataba maalumu wakuu wa Shule ya kiutendaji kwa ufanisi, (Commitment ) juu

3. Kuwaandikisha mikataba maalumu wakuu wa Shule ya kiutendaji kwa ufanisi, (Commitment ) juu ya usimamizi madhubuti utakaopelekea kupanda kwa ufaulu katika shule zao, mkataba huo utaeleza malengo na namna ya kuyafikia atakayopewa Mkuu wa Shule. Mkuu wa shule ataingia mkataba na walimu waliopo chini yake. 4. Kutumia mbinu shirikishi kwa shule zilizopo maeneo ya jirani kwa kuweka kambi na kufanya maandalizi ya pamoja, mbinu hii itahusu wanafunzi wa kidato cha nne kuhamia katika shule mojawapo kati ya shule zilizojirani na kuweka kambi ya pamoja ambapo kwa pamoja walimu wa shule zote mbili zilizoungana watashirikiana kuwaanda wanafunzi wao. 5. Kuhakikisha kila shule inatoa huduma ya chakula shuleni, wazazi wahamasishwe na wachangie huduma ya chakula kwa watoto wao shuleni, muda wa shule ya mwisho kuanza kutoa huduma hiyo ni tarehe 30 February.

6. Kila shule iwasilishe mpango kazi wake wa mwaka huu, ikiambatanishwa na kalenda ya

6. Kila shule iwasilishe mpango kazi wake wa mwaka huu, ikiambatanishwa na kalenda ya shule na ionesha jinsi shule ilivyojipanga kufikia malengo yake , mpango kazi wa kila shule utapimwa kwa matokeo yake mwisho wa mwaka ambapo hatua za wazi kabisa zitachukuliwa kwa walioandaa bila kutekeleza. 7. Kila Ofisa katika Idara atapewa Uratibu wa Tarafa ya Kielimu kwa maana ya kusimamia na kuratibu maendeleo ya jumla ya elimu katika Tarafa yake, utekelezaji wa mpango kazi utatolewa ripoti kila baada ya miezi mitatu. 8. Mada zote za masomo kwa vidato vya mitihani kukamilishwa mapema Septemba, na kuanza kufanya mazoezi mengi ya kujiandaa.

9. Kutokana na ukweli kuwa moja ya sababu kubwa ya ufaulu duni wa wanafunzi

9. Kutokana na ukweli kuwa moja ya sababu kubwa ya ufaulu duni wa wanafunzi wengi ni kutokuwa na mazoezi ya kutosha , kitengo cha Taaluma kitaratibu kwa karibu mitihani ya kujipima wanafunzi ya kila mwezi yaani monthly tests, zitakazo tumiwa kama “ continous assessment” kwa wanafunzi, mazoezi haya ya kila mwezi yatatumika katika kuwachuja wanafunzi na kuwabaini wanafunzi wasio jiweza ambao watapewa mafundisho maalumu. 10. Kuwa na mitihani Mikubwa Minne ya kujiandaa kabla ya kuingia katika Mtihani wa mwisho taifa kwa vidato vya mitihani, mitihani hii itatungwa kwa fomati ya mitihani ya Taifa, kidato cha nne na cha pili , inapendekezwa ifanyika kuanzia midterm ya kwanza mwezi machi , mwezi juni , Moko , na Pre- National. Mitihani hii mikubwa itaenda sambamba na mazoezi ya kila mara na mitihani ya kila mwisho wa mwezi, monthly test itakayofuatiliwa na Ofisi ya wilaya kwa umakini wa hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote.

 • 10. Kuwa na mitihani Mikubwa Minne ya kujiandaa kabla ya kuingia katika

• 10. Kuwa na mitihani Mikubwa Minne ya kujiandaa kabla ya kuingia katika Mtihani wa mwisho taifa kwa vidato vya mitihani, mitihani hii itatungwa kwa fomati ya mitihani ya Taifa, kidato cha nne na cha pili , inapendekezwa ifanyika kuanzia midterm ya kwanza mwezi machi , mwezi juni , Moko , na Pre- National. Mitihani hii mikubwa itaenda sambamba na mazoezi ya kila mara na mitihani ya kila mwisho wa mwezi, monthly test itakayofuatiliwa na Ofisi ya wilaya kwa umakini wa hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote. • 11. Utaratibu wa zamani wa Kufanya masahihisho ya mitihani ya nyuma ya Taifa Past paper Solving Kuanzia mwezi julai ambapo mada nyingi zitakuwa zimefundishwa. Hapa kila shule inahimizwa kuwa na benki ya maswali kwa mitihani ya miaka kumi iliyopita au zaidi. • 12. Kufuatilia na kufanya tathimni ya utekelezaji wa mikakati hii kila mwisho wa mwezi.

 • 13. Idara imejipanga kuhakikisha michezo inazingatiwa na kuwekewa programu maalumu kwa kila

• 13. Idara imejipanga kuhakikisha michezo inazingatiwa na kuwekewa programu maalumu kwa kila shule, kila shule lazima iwe na mwalimu wa michezo na Mkuu wa shule ahakikishe kuwa viwanja vya michezo vinakuwepo na wanafunzi wote wanashiriki michezo, michezo hujenga afya ya mwili na akili lakini husaidia kuwaweka bize wanafunzi na kusahau vitendo visivyofaa • 14. Kuanzisha bendi kuwa na wimbo wa shule na kuhakikisha wanafunzi wanaimba nyimbo ya Tanzania nakupenda kila jumatatu na ijumaa, wimbo huu huwakumbusha wanafunzi mambo makubwa waliyofanya waasisi wetu na kuwajengea dhana ya uzalendo na kuipenda nchi yao. Uchunguzi uliofanywa kwa shule zenye bendi wanafunzi wengi huvutiwa na parade ya bendi na hivyo kupunguza utoro shuleni, Pared pia huwajenga wanafunzi kuwa wakaka mavu

 • 15. Vidato vya mitihani kuwa na mitihani mikubwa minne ya kujipima kabla

• 15. Vidato vya mitihani kuwa na mitihani mikubwa minne ya kujipima kabla ya kuingia katika mitihani yao ya Taifa, • 16. Mitihani minne ya kujipima ifanyike na kusahihishwa kiwilaya, Ratiba ya mitihani hiyo itatolewa na Ofisi ya Taaluma kabla ya February. • 17. Kutakuwepo mitihani miwili mikubwa ya mwisho kwa kidato cha sita kwa maana ya katika ya January na katika ti ya Machi kabla ya kuingia katika mitihani yao ya Taifa mwezi Mei mwakani. • 18. Kusimamia kikamilifu na kuhakikisha walimu wanaopangwa kufundisha vidato vya mitihani ni walimu werevu Competent teachers , )Mkuu wa shule makini anatambua vizuri uwezo wa walimu wake wote wakiwa darasani , kwani yeye ni mkaguzi namba moja shuleni.

 • 19. Wakuu wa shule kuwa na vipindi na kufundisha japo vipindi vichache

• 19. Wakuu wa shule kuwa na vipindi na kufundisha japo vipindi vichache ili kuonesha mfano wa uwajibikaji , kwani hata barua za uteuzi wa nafasi zao unasisitiza juu ya kufundisha ilikuwa mfano kwa walimu wengine. • 20. Kutovumulia kwa namna yoyote ile uzembe na kutojituma kwa walimu na kuchukua hatua stahiki kwa walimu wazembe na wasiojituma • 21. Kuwa na vikao kila robo ya mwaka kuhakikisha tathimini inatolewa na kuratibu mafanikio na changamaoto za mikataba iliyowekwa. • Ni imani yetu kuwa mikakati hii ikisimamiwa ipasavyo kwa hakika malengo ya BRN, ya ufaulu wa asilimia 71 kwa kidato cha pili na nne yatafikiwa na kupitwa. • Aidha Idara imepanga kufuatilia kwa karibu suala la uhuishaji wa Clubs mbali Mashuleni, Kama Clubs za Wasichana, Debate na Clubs za rushwa. • Uwepo wa club hizi hasa Clubs za kupambana na rushwa, unawajengea wanafunzi uelewa wa madhara ya rushwa tangu wakiwa shuleni , na kuwajengea moyo wa uzalendo wangali wadogo, Club hizi zitaratibiwa kikamilifu na si kwa maneno

MAONI • Idara ya elimu Sekondari kwa pekee kabisa inapongeza juhudi za wazi na

MAONI • Idara ya elimu Sekondari kwa pekee kabisa inapongeza juhudi za wazi na za makusudi zinazofanywa na mkuu wa wilaya katika kuleta mabadiliko ya kweli katika elimu, tunaadi kwa hali na mali kumuung mkono kwa kuhakikisha kuwa kwanza tunatumia faida ya uchache wa shule tulionao kuhakikisha mabadiliko ya kweli yanatokea katika Idara yetu, kwa kuhakikisha tunafuatilia na kusimamia malengo tuliyojiwekea kwa kuhakikisha yanafanikiwa badala ya kuwa na mikakati mingi kila mwaka inayoishia kuandiliwa bila kutekelezwa , Ni imani yetu kuwa sisi kama wadau wa elimu tukishirikiana tutaleta matokea chanya na kuibadilisha wilaya ya mpwapwa kielimu kwa kuleta mapinduzi makubwa ya kimfumo na kiutendaji, na hasa ikizingatiwa Mkoa wa Dodoma ndio Makao makuu ya Nchi Hivyo, unatakiwa kuwa mfano bora kwa matokeo makubwa kila sekta.

MAONI • Tunawatakia utendaji mwema kwa mwaka huu mpya kwa pamoja tukalete mabadiliko chanya

MAONI • Tunawatakia utendaji mwema kwa mwaka huu mpya kwa pamoja tukalete mabadiliko chanya katika Wilaya yetu ya Mpwapwa. Kauli mbiu ya mwaka huu kwa upande wetu ni Mafanikio ya elimu ni kutekeleza mikakati, kila mmoja atimize wajibu wake inawezekana. • Ahsanteni na karibuni tujadiliane kwa pamoja. • LEONARD MSIGWA • MKUU WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI