Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB Tarehe
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Tarehe: 19/05/2017 Mtoa mada: Dickson Pangamawe
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu katika sekta ya kilimo kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo nchini.
MALENGO MAKUU YA BENKI YA KILIMO 1. Kuwezesha kufikiwa kwa utoshelezi wa chakula endelevu na usalama wa chakula nchini; 2. Kuwezesha mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kufikia uzalishaji wenye tija na kibiashara katika kukuza uchumi endelevu wa uhakika na kupunguza umaskini.
MIKAKATI YA KUFIKIA MALENGO YA BENKI • Kushirikiana na wadau wakubwa wa sekta ya kilimo katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini, • Kuhamasisha na kushirikiana na taasisi za fedha nchini ziweze kushiriki kikamilifu katika kutoa mikopo katika sekta ya kilimo, • Kuhamasisha na kuwezesha wakulima wakubwa wanaosaidiana na wadogo katika kuwafundisha kilimo cha kisasa na Kuwapatia masoko kwa mazao wanayozalisha, • Kushirikiana na serikali wakati wa kutunga, kupitisha au kurekebisha sera mbali za kilimo ili ziweze kuwanufaisha wakulima na wawekezaji katika sekta ya kilimo,
MIKAKATI YA KUFIKIA MALENGO YA BENKI • Kuwezesha na kusaidia uendelezaji wa masoko ya kilimo nchini, • Kuwezesha wawekezaji/wajasiriamali wadogo na wa katika sekta ya kilimo na kuwaunganisha katika vikundi ili kuwapatia soko la uhakika la mazao yao, • Kufuatilia utafiti wenye tija katika sekta ya kilimo kwa kushirikiana na vyuo vya kilimo na taasisi za utafiti nchini, • Kutafuta fedha za riba nafuu na dhamana kwa ajili ya mikopo kwa wakulima wadogo
MIKOPO YA MUDA MFUPI (Mwaka 1– 2) Mikopo ya muda mfupi hutolewa kukidhi mahitaji ya wakulima yafuatayo: • Kuwezesha uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo, • Kulipia gharama za kukodisha zana bora za kilimo kama matrekta, • Ununuzi wa mbegu bora/upatikanaji wa Mitamba bora, viuatilifu/madawa na mbolea/marisho kwa wakati, na • Gharama za uendeshaji za vifaa na mashine bora za umwagiliaji
MIKOPO YA MUDA WA KATI (Miaka 2 – 5) Mikopo ya muda wa kati hutolewa kukidhi mahitaji yafuatayo: • Upanuzi wa mashamba ya wakulima/Ranchi, • Kuchimba visima vya maji na mabwawa ya kuvunia maji/Majosho na Maji kwa Mifugo, • Ununuzi wa zana na mashine bora za kuvunia na kusindika mazao/Zana za Kukamulia na Kusindika, • Ununuzi wa vyombo vya kusafirishia mazao kutoka vijijini, • Ujenzi wa maghala bora na mashine za uhifadhi
MIKOPO YA MUDA WA MREFU (Miaka 5– 15) Mikopo ya muda wa mrefu itatolewa kukidhi mahitaji yafuatayo: • Upanuzi mkubwa na uanzishaji wa mashamba ya wakulima/Ranchi, • Ununuzi wa mashine bora za kulimia/mifugo, kuvunia/kukamulia na kusindika mazao, • Ujenzi wa maghala bora na mashine za uhifadhi/Collection Centres, • Miundombinu na mashine za umwagiliaji, • Miundombinu ya bara, masoko na umeme, na • Uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji
RIBA NA MAREJESHO • Mikopo ya Riba Nafuu Kati ya 8% - 12% Kwa Mwaka • Marejesho ni Baada ya Mavuno/Uzalishaji na Mauzo, kuzingatia mpango kazi, na mtiririko wa mapato na matumizi ya mradi.
MIKOPO HULENGA MAHITAJI MNYORORO WA THAMANI Uzalishaji Pembejeo na Umwagiliaji Mahitaji ya mikopo wakati wa Kuvuna Kuhifadhi, Kusindika na Usafirishaji PHF (S/T, M/T & L/T Loans) S/T, M/T, L/T, & Inventory Finance 1. Kuongeza Uzalishaji 2. Kuongeza thamani ya mazao YOTE Usambazaji wa mazao na uuzaji nje ya Nchi KWENYE Walaji na Wauzajai reja S/T, M/T, LT/L, & T/Finance 3. Miundo mbinu ya masoko
SEKTA ZA KILIMO ZA KIPAUMBELE Kwa kuanzia Benki imetoa kipaumbele katika sekta za kilimo zifuatazo: i. Nafaka (Mahindi na Mpunga), ii. Mazao ya viwanda (Miwa na Korosho), iii. Mifugo (Ng’ombe wa maziwa na nyama), iv. Kilimo cha Matunda, Mboga na viungo, v. Mbegu za mafuta ya kupikia (Alizeti na Ufuta), vi. Mazao ya Misitu na ufugaji wa Nyuki, vii. Ufugaji wa Kuku pamoja na Ufugaji wa samaki.
SEKTA NYINGINE ZA KILIMO • Benki inatarajia kuzifika Sekta nyingine za Kilimo kwa siku za usoni kutokana na umuhimu wake katika kuinua uchumi wa wananchi. Sekta hizo ni kahawa, Pamba, Chai, Tumbaku, Miti, … n. k
MPANGO SHIRIKISHI WA BENKI NA WADAU Benki inashirikiana na wadau muhimu katika sekta ya kilimo/mifugo kufanya kazi kwa pamoja. Wadau hao ni; i. Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ii. Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIC), iii. BOT iv. Tume ya Maendeleo ya Ushirika Nchini (TCDC), v. MIVARF, vi. Wanunuzi wa Mazao na Wasindikaji vii. Wauzaji na wasambazaji wakubwa wa pembejeo. viii. Halmashauri za wilaya
KWANINI MPANGO SHIRIKISHI? . . . . • Kurahisisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati. • Kurahisisha kutoa elimu kwa wakulima wadogo. • Kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za wakulima wadogo.
KWANINI MPANGO SHIRIKISHI? . . . . • Usimamizi wa wakulima hasa wadogo utakuwa imara Zaidi na hivyo kujenga vikundi vya wakulima vilivyo imara. • Marejesho ya mikopo kwa wakulima wadogo yanakuwa mazuri. • Masoko ya mazao kwa wakulima wadogo yanakuwa ya uhakika kutokana na wingi wa mazao.
MPANGO SHIRIKISHI TADB • • Mikopo Kwa Wakati Kuwaunganisha Wakulima na Masoko Kusimamia Mikopo Mikataba ya Utatu (TADB, Wakulima na Mnunuzi) WADHAMINI • • Dhamana ya angalau 50% ya Mkopo Mkataba wa Kudhamini Wakulima CHAMA • • Maombi ya Mkopo Mkataba na Mnunuzi Mkataba na Watoa Huduma Mkataba wa Utatu (TADB, Wakulima na Mnunuzi) MNUNUZI • • • Mkataba wa Manunuzi Mkataba wa Utatu (TADB, Wakulima na Mnunuzi) Malipo kupitia Akaunti ya Chama TADB
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO Kwa kuanza Benki inatoa mikopo kwa vikundi vya wakulima wadogo vilivyosajiliwa. 1. MAMLAKA YA KUKOPA • Barua ya maombi ya mkopo. • Muhtsari wa kikao cha Mkutano Mkuu kilichoidhinisha kukopa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), • Nakala ya kitabu cha usajili wa wanachama.
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO 2. UHALALI WA MKOPAJI • Cheti cha Usajili inayokipa Mamlaka Chama Kukopa. • Katiba ya Chama iliyosajiliwa. • Cheti cha ukomo wa madeni na makisio yaliyopitishwa na Ofisi ya ushirika (Kwa vyama vya ushirika tu).
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO 3. TAARIFA ZA KINA JUU YA MRADI WA KILIMO • Mpango wa Biashara. • Wasifu wa viongozi wa Chama. • Taarifa ya uzalishaji kwa misimu mitatu (3) ya nyuma na Matarajio ya mavuno kwa msimu ujao (Taarifa ikionesha Jumla ya Ekari zilizolimwa, Jumla ya mavuno yaliyopatikana, Bei ya Mauzo kwa kilo/tani moja na Jumla ya Mauzo yaliyopatikana). • Bajeti/gharama za kuhudumia shamba kwa ekari moja kuanzia kulima, mbegu, mbolea, madawa, palizi, kuvuna mpaka huhifadhi ghalani.
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO • Kalenda ya zao na Mpango mkakati kuanzaia kupanda, palizi, mbolea mpaka kuvuna na kupeleka gharani/kuuza. • Taarifa na Mkataba baina ya Chama na mtoa huduma ya Mbolea, Mbegu na Madawa. Taarifa ya msambazaji pembejeo iambatane na vielelezo vyake kama Leseni ya Biashara, Vyeti vya usambazaji Pembejeo kutoka mamlaka husika.
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO • Mkataba wa kuuza mazao kwa mnunuzi mwenye uwezo na ambaye Chama kimeridhia au utaratibu wa mauzo uliokubalika kama mfumo wa stakabadhi ghalani. • Taarifa za upatikaji wa Ghala la kuifadhi Mazao (au Mkataba wa ukodishaji Ghala kama chama hakina Ghala).
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO TAARIFA ZA FEDHA • Taarifa ya Benki kwa miezi 12 ya hivi karibuni. • Makadirio ya Mtiririko wa fedha/Makadirio ya Mapato na Matumizi. • Taarifa za ukaguzi wa fedha za Chama kwa miaka mitatu. • Taarifa ya Mikopo yote ya nyuma na ya sasa ambayo Chama iliwai kukopa/inadaiwa na taasisi yeyote ya fedha (mikataba ya mikopo iambatanishwe).
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO TAARIFA JUU YA DHAMANA ZA MKOPO • Aina ya dhamana zinazowekwa na Chama (Dhamana zinazokubaliwa na Benki ni Mashamba yenye hati miliki au za kimila, Nyumba zenye hati au leseni za makazi au Mali zinginezo zenye hati miliki.
TARATIBU ZA MAOMBI YA MKOPO TAARIFA/NYARAKA ZINGINE • Profoma invoices/Ankara kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, mashine au zana za kilimo.
MALENGO YA BENKI 2017 • Kuendelea kuwawezesha wakulima wadogo kupitia vikundi vilivyopo kwenye mfumo rasmi. • Kuangalia makundi maalum hasa vijana na wakinamama. • Kuongeza mazao ya kipaumbele katika maeneo tofauti. • Kupanua wigo wa kukopesha: – Mabenki na Taasisi za kifedha – Wakulima wa kati na wakubwa wanaojishughulisha na kilimo cha kibiashara – Taasisi mbali zinazojihusisha na huduma za kilimo i. e. watengeneza mbolea, mbegu na za kilimo.
MALENGO YA BENKI 2017 • Kuongeza eneo la kutoa huduma, tunatarajia kufungua Ofisi za Kanda katika mikoa ifuatayo: – Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Mtwara • Tayari benki imewaandikia wakuu wa mikoa wote nchini bara na Zanzibar kuwasilisha miradi ya kilimo yenye tija kwa ajili ya kuiwezesha.
HITIMISHO Benki inawakaribisha wadau kutoa mawazo/ mapendekezo ya namna ya kuwafikia wakulima wadogo kwa ufanisi.
Asanteni sana kwa Kunisikiliza
MAWASILIANO Jengo la Acacia, 84 Barabara ya Kinondoni, S. L. P 63372, Dar es Salaam Simu: +255 22 292 3501/2 Fax: +255 22 292 3501 Web: www. tadb. co. tz
- Slides: 29