MAADA MWEZESHAJI S GEORGE MAY 2017 MUUNDO WA

  • Slides: 16
Download presentation
MAADA MWEZESHAJI S. GEORGE MAY 2017

MAADA MWEZESHAJI S. GEORGE MAY 2017

MUUNDO WA MAADA • Wanasayansi wanaamini kwamba maada zimeundwa kwa chembe ndogo sana ambazo

MUUNDO WA MAADA • Wanasayansi wanaamini kwamba maada zimeundwa kwa chembe ndogo sana ambazo hazionekani kwa macho na hata kwa msaada wa darubini • Chembechembe hizo ni za aina tatu I. Atomi II. Molekuli III. Ayoni

MUUNDO WA MAADA • Maada inaweza kuundwa kwa aina moja wapo ya chembe hizo.

MUUNDO WA MAADA • Maada inaweza kuundwa kwa aina moja wapo ya chembe hizo. • Mfano- maji, sukari, glukosi na oksijeni zimeundwa kwa molekuli • Heliamu, neoni, na kriptoni zimeundwa kwa atomi tu • Munyu, salfeti ya kopa na kloraidi ya kalsiamu zimeundwa kwa ayoni tu.

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo wa chembe katika maada mbali

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo wa chembe katika maada mbali hutofautiana • Gesi mjongeo ni haraka zaidi kuliko kwenye vimiminiko • Mweneo hufanyika haraka zaidi kwenye hewa kuliko kwenye maji

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo katika gesi

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo katika gesi

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo katika vimiminiko

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo katika vimiminiko

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo wa chembe za maada hufanyika

Tofauti za mjongeo wa chembe za maada • Mjongeo wa chembe za maada hufanyika kwa pole kwenye maada yabisi • Mjongeo kwenye maada yabisi hauonekani na huwa ni wa mtetemo ambapo chembe hazisogei kutoka sehemu moja kwend sehemu nyingine • Mjongeo katika yabisi

NADHARIA YA MJONGEO WA CHEMBE ZA MAADA • Inaeleza kwamba chembe zinazounda maada ziko

NADHARIA YA MJONGEO WA CHEMBE ZA MAADA • Inaeleza kwamba chembe zinazounda maada ziko katika hali ya kujongea nyakati zote • Hufanya chembe hizo kuwa na nishati ya mjongeo • Nadharia hii hutusaidia katika kueleza dhana ya mweneo

NADHARIA YA MJONGEO WA CHEMBE ZA MAADA • Robert brown (1827) alichunguza chavua za

NADHARIA YA MJONGEO WA CHEMBE ZA MAADA • Robert brown (1827) alichunguza chavua za maua kwenye maji akaona kuwa chavua hizo zilikuwa zikijongea lakini hazikuwa na muelekeo maalumu. • Hii imetuwezesha kutambua mjongeo wa chembe za maada hauna uelekeo maalumu • Mjongeo wa chembe katika maada unaitwa mjongeo wa Brown

MABADILIKO YA MAADA • Mabadiliko ya maada yako ya aina mbili 1. Badiliko la

MABADILIKO YA MAADA • Mabadiliko ya maada yako ya aina mbili 1. Badiliko la kiumbo 2. Badiliko la kikemikali

BADILIKO LA KIUMBO • Katika badiliko la kiumbo la maada hakuna maada mpya inayotokea

BADILIKO LA KIUMBO • Katika badiliko la kiumbo la maada hakuna maada mpya inayotokea • Maada ya awali na iliyotokea zinakuwa na tabia za kikemikali zinazofana • Mfano- kubadilisha barafu kuwa kimiminiko au maji kuwa mvuke • Mmumunyo wa sukari katika maji • Kuweka usumaku wa muda katika chuma

BADILIKO LA KIUMBO a) Hakuna maada mpya inayotokea b) Ni rahisi kubadili uelekeo wa

BADILIKO LA KIUMBO a) Hakuna maada mpya inayotokea b) Ni rahisi kubadili uelekeo wa badiliko hilo na kupata hali ya maada ya awali c) Hakuna badiliko la uzani/uzito wa maada iliyohusika katika badiliko hilo d) Hakuna nishati iliyotolewa au kusharabiwa katika badiliko hilo

BADILIKO LA KIKEMIKALI • Hutokea pale ambapo maada hubadilika na kutoa maada nyingine yenye

BADILIKO LA KIKEMIKALI • Hutokea pale ambapo maada hubadilika na kutoa maada nyingine yenye tabia tofauti. • Maada mpya huwa na tabia tofauti na zile za awali. • Mara nyingi nishati hutolewa au kusharabiwa katika mabadiliko haya • Badiliko la kikemia likishatokea sio rahisi kuligeuza na kupata maada ya awali

BADILIKO LA KIKEMIKALI • • • Mfano wa mabdiliko ya kikemikali Chuma kupata kutu

BADILIKO LA KIKEMIKALI • • • Mfano wa mabdiliko ya kikemikali Chuma kupata kutu Kuungua kwa karatasi, kuni ikawa jivu Kuchacha kwa maziwa Kuiva kwa matunda Kuoza kwa matunda

BADILIKO LA KIKEMIKALI • Dutu mpya yenye tabia tofauti hutokea • Badiliko la uzani

BADILIKO LA KIKEMIKALI • Dutu mpya yenye tabia tofauti hutokea • Badiliko la uzani la dutu ilyohusika hutokea • Nishati hutolewa na kusharabiwa katika badiliko hilo • Ni vigumu kugeuza uelekeo wa badiliko hilo na kuweza kupata dutu ya awali

TOFAUTI YA BADILIKO LA KIUMBO NA KIKEMIKALI BADILIKO LA KIUMBO BADILIKO LA KIKEMIKALI Dutu

TOFAUTI YA BADILIKO LA KIUMBO NA KIKEMIKALI BADILIKO LA KIUMBO BADILIKO LA KIKEMIKALI Dutu yenye tabia tofauti haitokei Dutu yenye tabia tofauti hutokea Ni rahisi kugeuza muelekeo wa badiliko hilo Si rahisi kugeuza muelekeo wa badiliko hilo Kwa kawaida hakuna nishati inayotolewa au kusharabiwa Kwa kawaida huambatana na kusharabiwa au kutolewa kwa nishati Uzito wa maada iliyohusika haibadiliki Uzito wa maada iliyohusika hubadilika