UUMBWAJI UPYA WA SAYARI DUNIA Somo la 13
UUMBWAJI UPYA WA SAYARI DUNIA Somo la 13 kwa ajili ya Machi 27, 2021
Kila siku sayari yetu inakuwa mbali kutoka katika uumbaji halisi wa Mungu. Dhambi imesababisha maangamizi katika viumbe vya asili na jamii ya wanadamu. Vyote dunia na wanadamu wanahitaji urejeshwaji kamili. Mpango halisi wa Mungu ulikuwa ni kurejesha hatua kwa hatua kila kitu pamoja na wa Israeli, akianzia Yerusalemu. Kwa sababu Israeli ilimkataa, alibadili mpango Wake. Hatua ya urejeshwaji. Isaya 65: 17 -25 Urejeshwaji wa Kiungu. Isaya 66: 1 -18 Ushirikiano wa Mwanadamu kwa ajili ya urejeshwaji: Kushiriki ujumbe. Isaya 66: 19 -20 Ukuhani wa kiulimwengu. Isaya 66: 21
HATUA ZA UREJESHWAJI “Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. ” (Isaya 65: 17) Katika nchi mpya, “simba atakula majani kama ng’ombe” (aya. 25). Asili itairudia hali yake kamilifu. Mungu hakutaka afanye badiliko kubwa na la ghafla. Alihitaji aboreshe hali kidogo. Yerusalemu ilitarajiwa kuwa mahali ambapo matarajio ya kuishi ni zaidi ya miaka 100 (aya. 20), nchi ingezalisha sana (aya. 21), na watu wangeishi kwa amani (aya. 22). Watu kutoka mataifa mengine weangelikuja Yerusalemu, na kila mmoja angeliipokea Injili. Ndipo Mungu angeliurejesha ulimwengu mzima, na kuwapatia wanadamu uzima wa milele.
UREJESHWAJI WA KIUNGU “Wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu. ” (Isaya 66: 18) Mungu huwajari wale “wanaotetemekea neno Langu” (aya. 2, 5) anapoleta urejeshwaji. Urejeshwaji wake unahusisha: Kuwakataa wanafiki (aya. 3) Kuwarejesha wanyenyekevu (aya. 5) Kuwaadhibu wanaomuumiza mtakatifu (aya. 5) Kuwafariji waumini (aya. 13) Kuwaharibu waabudu sanamu (aya. 17) Nia ya Mungu ni kumrejesha kila mmoja. Anamhitaji kila mmoja kuitikia wito Wake, hii ndio shauku Yake kubwa (1 Tim. 2: 4). Mungu atawakusanya wanadamu wote ili kila mmoja auone utukufu Wake kabla ya urejeshwaji wa jumla na wa mwisho (aya. 18).
KUUSHIRIKI UJUMBE “Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa […] Nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. ” (Isaya 66: 19) Katika mpango halisi wa Mungu, angelituma wainjilisti kutokea Yerusalemu kwenda katika pande zote za ulimwengu baada ya Israel kuwa imerejeshwa Hata hivyo, Israeli ilimkataa Masihi aliyekuja kuwarejesha. Kwahiyo, Yesu alilichagua Kanisa la Kikristo kuuhubiri ujumbe Wake (Mathayo 28: 19 -20). Ujumbe uliufikia ulimwengu katika kizazi kimoja (Wakolosai 1: 23). Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Wale wanaoamini na kushukuru kwa kazi yetu ni sadaka kwa Mungu (Is. 66: 20). Sisi ni “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu” kando na wao (Warumu 12: 1).
“‘Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na walawi, asema BWANA. ” (Isa. YA 66: 21) Ni akina nani walio “baadhi yao” katika fungu hili? Ni wa Mataifa. Watu kutoka kila taifa walioamini na kujiunga na waongofu (Waefeso. 2: 14). Sisi ni taifa la makuhani (1 Pt. 2: 9). Ukuhani huu haujikiti juu ya ukuhani wa Walawi. Badala yake unajikita katika kazi ya Yesu Kuhani wetu Mkuu (Waebrania. 6: 20). Hata hivyo, kuinuliwa kwa Wamataifa haihusishi kunyanyashwa kwa Wayahudi. Paulo aliwalinganisha watu wa Mungu na mti wa mzeituni. Matawi halisi ni wana wa Israeli, na Wamataifa ni matawi madogo yaliyoshikishwa kwenye mti huo (Warumi. 11: 17 -18). Watu wote ni sawa katika Kanisa la Mungu, na kila mmoja wetu ana utume wa kubeba.
UREJESHWAJI WA MWISHO “‘Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. ” (Isaya 66: 23) Katika urejeshwaji wa Mwisho, mbingu na nchi zitafanywa upya. Uumbaji mpya na jamii ya wanadamu iliyorejeshwa vitabaki milele (Is. 66: 22). Katika Nchi mpya, “Wala mauti haitakuwamo tena; wala maombolezo wala kilio wala naumivu” (Uf. 21: 4). Tutamwabudu Mungu pamoja kila Sabato. Na kila mwezi tutakusanyika kula matunda ya Mti wa Uzima (Uf. 22: 2). Hili litatokea ni shukrani sana kwa kafara kuu ya Yesu kwetu. Kitabu cha Isaya kinamalizia na onyo: kila mmoja asiyetaka kuishi milele atakufa milele (Is. 66: 24; Uf 20: 14 -15).
E. G. W. (Prophets and Kings, cp. 60, p. 731) “Msafiri mwenzangu, bado tuko kati ya vivuli na shida za shughuli za kidunia; lakini kitambo kidogo Mwokozi wetu atatokea kuleta ukombozi na pumziko. Hebu kwa imani tuutazamie uzima wa milele kama ulivyoonyeshwa kwa mkono wa Mungu. Yeye aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwenguanayafungua malango ya Paradiso kwa wote wanaomwamini. Siyo mbali pambano litapiganwa, ushindi utapatikana. Siyo mbali tutamwona Yeye ambaye matumaini yetu ya uzima wa milele yamewekwa. Na kwa uwepo Wake majaribu na mateso ya maisha haya yataonekana si kitu”
“The great controversy is ended. Sin and sinners are no more. The entire universe is clean. One pulse of harmony and gladness beats through the vast creation. From Him who created all, flow life and light and gladness, throughout the realms of illimitable space. From the minutest atom to the greatest world, all things, animate and inanimate, in their unshadowed beauty and perfect joy, declare that God is love. ” E. G. W. (The Great Controversy, cp. 42, p. 678)
- Slides: 9