UJUMBE UNAOFAA KUSAMBAZWA Somo la 12 kwa ajili
UJUMBE UNAOFAA KUSAMBAZWA Somo la 12 kwa ajili ya Septemba 19, 2020
“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka kati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemi za maji’ ” (Ufunuo 14: 6 -7)
Ufunuo 14: 6 -12 inawasiliza ujumbe wa mwisho ambao utatangazwa katika huu ulimwengu kabla ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Tumeitwa kuuhubiri ujumbu huu, kwa sababu kuja kwake mara ya pili kumekaribia. Huu ndio “ukweli wetu wa leo. ” Hebu tujifunze unabii huu wa ufunuo ujulikanao kama “ujumbe wa malaika watatu. ” Uweli wa leo Muktadha wa ujumbe Malaika wa kwanza: Injili ya milele Uchaji, utukufu, hukumu, na uumbaji Malaika wa pili: Wito wa mwisho Malaika wa tatu: Ibada ya kweli
“Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo. ” (2 Petro 1: 12) Mungu anayajua yajayo na anaitawala historia. Anaweza kutuma ujumbe mahsusi kwa wakati maalum katika historia ya mwanadamu (Isaya 46: 10; Amosi 3: 7). Huu hujulikana kama “ujumbe wa leo. ” Je; Upi ulikuwa ujumbe wa leo kwa watu wafuatao? Nuhu Gharika Jeremia Kujusalimisha kwa Babeli ili wasiangamizwe Yohana mbatizaji Kutayarisha njia ya Masihi Petro Maisha, Kifo, na ufufuo wa Yesu Wakati Petro akisambaza ujumbe wake wa leo, pia aliwahimiza wasikilizaji wake kuendelea kujifunza kweli zilizofunulia kabla yake (2 P. 1: 1621). Uvuvio wa Mungu ni endelevu na kamwe
MUKTADHA WA UJUMBE “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake n jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. ” (Ufunuo 14: 1) Katika Ufunuo, Mwanakondoo (Yesu) anaonekana katika historia yote ya Kanisa (Sr. 1 -12). Matukio yanayotangulia ujio wake, yamefuliwa (Sr. 13 -18), na tunahimizwa kuyatazama matukio hayo–“naja upesi” (22: 7)–na maisha yetu yajayo (Sr. 19 -22). Sura ya 13 hueleza mgogoro wa mwisho, kisha sura 14 hutambulisha wito wa mwisho na matokeo yake: ❶ ❷ ❸ ❹ Wabeba wito wa mwisho (fg. 1 -5) Ujumbe wa wito wa mwisho (fg. 6 -12) Matokeo ya kuukubali wito (fg. 13 -16) Matokeo ya kuutakaa wito (fg. 17 -20) Mavuno huwakilisha ukombozi wa wenye haki. Ukatwaji wa mizabibu huwakilisha kifo cha waovu. Vyote vitafanyika katika ujio wake wa mara ya pili, baada ya ujumbe wa mwisho kuwa umehubiriwa (Mathayo 24: 14).
INJILI YA MILELE “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka kati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa. ” (Ufunuo 14: 6) Ukweli wa leo ambao lazima uhubiriwe katika wakati wa mwisho una upekee maalum, lakini msingi wake ni Injili ya milele. Injili tunayolazimika kuihubiri ni Habari njema ya Neema ya Mungu, kafara yake, Nguvu yake ya ubunifu na ukombozi, Msamaha wake, Nguvu yake inayotufanya kuwa washindi, Upendo wake usio na mwisho… Kila mmoja anapaswa kupokea ujumbe huu. Haidhuru utaifa wake, rangi yake, hadhi, Imani au hali yake za kijamii. Kila mmoja lazima asikie Habari njema na apate nafasi ya kumkubali au kumkataa Yesu kama Bwana na Mwokozi wa wake binafsi.
UCHAJI, UTUKUFU, HUKUMU, NA UUMBAJI “akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemi za maji. ’ ” (Ufunuo 14: 7) Ujumbe wa malaika wa kwanza ni : Kumcha Mungu katika kila tunachofanya. Kumpa utukufu kwa kumfanya wa kwanza katika kila tunachowaza na tunachofanya. Tambua kuwa tutahukumiwa, Hivyo tunapaswa kuzishika amri zake (Mhubiri 12: 13 -14) Mwabudu Mungu Muumbaji, iheshimu amri ya nne (i. e. Sabato, Kutoka 20: 8 -11) Upo uhusiano kati ya kumcha Mungu, kumtii na hukumu. Utii ni matokeo ya kuwa na mahusiano yaokoayo na Yesu. Ni Haki yake pekee iliyo na wema wa kutosha kusimama katika Hukumu. Tu salama katika haki yake.
“Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. ’ ” (Ufunuo 14: 8) Katika kitabu cha Ufunuo, “Babeli” huwakilisha dini ya uongo inayojikita katika matendo ya mwanadamu, tamaduni za mwanadamu, na mafundisho ya uongo. Dini hii huchanganya kweli alizofundisha Yesu na mafundisho mengine na mawazo ya mwanadamu au Shetani. Ndani ya Babeli kila kitu kimechanganywa. Kwa sababu hii, Mungu anawaita wanaompenda Yesu na kumkubali kama Mwokozi wao kuyakimbia machafuko hayo. Kitabu cha Ufunuo kinatoa sura mbili nzima (17 na 18) kwa anguko la Babeli, hivyo wito wa kutoka kwake (Babeli) ni wa muhimu.
IBADA YA KWELI “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu […]’ ” (Ufunuo 14: 9 -10) Ujumbe wa malaika watatu ni endelevu. Injili ikisha kuhubiriwa ulimwenguni kote, ujumbe uneendelezwa na wito wa kuachana na machafuko ya mafundisho ya “Babeli. ” Mwitikio kwa jumbe hizo mbili unaoneshwa katika Ufunuo 13: 15 -18. Mnayama–ambaye ni sehemu na ni kichwa cha Babeli analeta chapa yake. Mungu anaweka mhuri wake kwa watu wake (Ufunuo 14: 1) Ujumbe wa malaika wa tatu unahusiana na ibada: Mwabudu Muumbaji katika siku aliyoiamua yeye, kataa pumziko la Jumapili (14: 12), na kataa kumwabudu mnyama kwa kushika sheria ya Mungu, ili kuepuka adhabu inayostahiri (14: 9 -11). Lazima tufanye maamuzi yetu wenyewe. Chaguzi zetu za kila siku zitaamua uamuzi wetu wakati huo.
“Mungu ameliita kanisa lake leo, kame alivyoiita Israeli ya zamani, kusimama kama nuru ulimwenguni. Kwa shoka lenye nguvu ya ukweli, jumbe za malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu, Amelitenga mbali na makanisa na ulimwengu ili kuwaleta katika utakatifu unaokaribiana kabisa na wake. Amewafanya kuwa wapokeaji wa sheria zake waliojitoa kweli kuu za unabii wa wakati huu […] malaika watatu wa Ufunuo 14 huwakilisha watu wanaopokea nuru ya ujumbe wa Mungu na kusonga mbele kama mawakala na kuitangaza tahadhali katika marefu na mapana ya nchi. ” E. G. W. (Testimonies for the Church, book 5, cp. 52, p. 455)
- Slides: 10