MRADI WA USAMBAZAJI WA TEKNOLOJIA YA BIOGESI KWA

MRADI WA USAMBAZAJI WA TEKNOLOJIA YA BIOGESI KWA MATUMIZI YA NYUMBANI TANZANIA(TDBP)

UTANGULIZI Programu ya uenezi wa mtambo wa biogesi ngazi ya kaya Tanzania(tdbp) ina majukumu ya kueneza mitambo ya bioges kwa njia ya kufundisha mafundi uashi na watumiaji na kuhamasisha uanzishwaji wa sekta binafsi ya makampuni ya ujenzi wa mitambo ya biogesi, ikishirikiana na wadau mbali ili kusisimua sekta binafsi kujihusisha na tecnolojia hii nchini.

Biogesi ni nini? Ni nishati itokanayo na kinyesi cha wanyama ambacho huchachuka ndani ya mitambo wa bioges na kuweza kutumika kwa ajili ya kupikia na kuwashia taa( japo kuna tafiti zinazoendelea kwa ajili ya kuzalisha nishati mbadala ya kuzalisha umeme). Ni gesi inayotokana na uchakachuaji wa vinyesi vya wanyama na masalia ya shambani na jikoni katika mazingira yasiyo na hewa ya oksijeni(ANAEROBIC DIGESTION).

HAKUNA HEWA YA OKSIJENI

Biogas ina nifaa? Biogesi inamfaa mtu yeyote mwenye uwwezo wa kufuga ng’ombe kuanzia idadi ya wawili na kuendelea. Kiasi cha gesi ipatikanayo kinategemea idadi ya mifugo iliyopo.

Maelezo kuhusu biogas yanaendelea…… Biogesi ni gesi salama kwa sababu hailipuki kama aina nyingine za gesi zinazowekwa kwenye mitungi na kukandamizwa. Biogesi kwa ujumla haina madhara kiafya na kimazingira

Biogesi ina matumizi mbali kupikia kwa kutumia majiko maalum na kutoa mwanga kwa kutumia taa maalum za biogesi ama taa za umeme kwa kutumia bioslurry/tope chujio), kuendeshea pampu za maji kwa kutumia injini maalum. Pia bioges inaweza kuendesha jokovu kwa kutumia injini maalum

Vitu vinne vikuu katika kufikia malengo ya kumiliki biogas MIFUGO KIPATO MAJI NIA

Je nitaweza Gharama za ujenzi wa mtambo? Mtambo wa biogesi hujengwa na vifaa vitumikavyo kwenye ujenzi wa nyumba. gharama za ujenzi hutegemea na bei ya vifaa vya ujenzi na hutofautiana kati ya sehemu moja na sehemu nyingine. Gharama ya awali inaweza kuonekana kwa juu lakini baada ya miaka miwili hadi mitatu, gharama hii huwa imeisharejeshwa kutumia biogesi badala ya nishati nyingine kama kuni , umeme, mkaa au mafuta ya taa

Baadhi ya Vifaa vinavyotumika kujengea mtambo…. .

Je nikijiandaa nitajengewa na nani? Mradi huu uliunda kampuni ambazo zilizalisha mafundi uashi waliopata mafunzo chini ya taasisi ya CAMATEC. Ambapo kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutekeleza mradi huu unasimamia kampuni hizi. FIDE kama mshirika mkuu unasimamia kampuni 13 toka utaratibu wa makampuni kupendekezwanayo ni KISIKI, D&B, KIRORE, KBC, RAM, CHANGAMKENI, KGB G. SULLE, MBIIC, NAGEMA, BAMAS, SIMA, ORON

Je, Mtambo ukiwa na hitilafu? Mtambo uliojengwa kwa ustadi hauhitaji matengenezo ya mara kwa mara hasa kama masharti ya kuhudumia mtambo yakifuatwa. Endapo mtambo unakuwa na hitilafu, mteja ni rahisi kuwasiliana na fundi pamoja na ofisi husika kwa ajili ya matengenezo ya mtambo. Matengenezo huhitajika tu kwenye sehemu fulani za vifaa vitakavyotumika kama majiko , taa ambapo sehemu hizo huchakaa na kubadilishwa.

Je, mimi mfugaji ninanufaika? Watu wote wenye mifugo kama ng’ombe, kuku, nguruwe nk. Wanaweza kuwa wateja wazuri wa biogesi. Ni vizuri kupata faida za ziada kutokana na mifugo mtu aliyo nayo kama hiyo nishati ya biogesi , mbolea bora zaidi na mazingira yaliyoboreshwa zaidi

Biogas ina faida yeyote? Biogesi ni nishati ya gharama nafuu kwa matumizi yake. Biogesi haina moshi wa harufu inapotumiwa Matumizi ya biogesi huwapunguzia akina mama adha ya kutafuta kuni, na kupata muda kwa shughuli nyingine za uzalishaji mali nje na ndani ya kaya zao Matumizi ya mbolea inayotoka kwenye mtambo huongeza uzalishaji wa mazao zaidi kulinganisha na matumizi ya mbolea ya viwandani Fursa za ajira , hasa kwa vijana waliofundishwa taaluma ya ujenzi wa mitambo na vile matumizi ya tope chujio(bio-slurry) na mboji kwa ajili ya mazao

SEHEMU YA PILI Historia fupi yateknolojia ya BIOGAS Tanzania.

Tenknolojia ya biogas imekuwa kwa muda mrefu. Na iliingia nchini katika miaka ya 1970 , Teknolojia hii imetokea katika nchi za mashariki ya kati hasa India na hatimaye kutua Nchini kupitia shirika la SIDO. Kwa wakati huo Nchi Nyingi za mashariki ya kati hasa India walikuwa wanatimia Muundo wa pipa linaloelea yaani(FLOATING DRUM)na huo ndio muundo tulioanza nao Nchini. .

Inaendelea………. Uliingiwa na changamoto katika kutekeleza muundo huu kutokana na mapipa kupata kutu na hatimaye kutoboka, hivyo ikawa changamoto katika marekebisho hivyo kuongeza gharama kwa mtumiaji. Baadaye Taasisi ya Camatec ikabuni aina mpya ambayo ilikuwa suluhisho ya awali. ikijulikana “Chinese Fixed Dome”-Mwaka 1983.

Inaendelea……. Miaka michache baadaye maboresho yalifanyika tena katika harakati za kupunguza gharama za ujenzi wa mitambo na kuzalisha aina mpya inaoitwa“ MODIFIED CAMARTEC DOME - MCD”. Aina hii ya mtambo ambayo ndiyo tunayoineza kwa sasa inaweza kupatikana kwa ujazo wa kiwango cha 4 m 3, 6 m 3, 9 m 3 na 13 m 3 na rahisi kujenga.

Inaendelea………. Kwa kushirikiana na Tasisi ya SNV mwaka 2011 Watafiti walibuni aina ya mtambo unaostawi maeneo ya wafugaji yaliyokithiri kwa ukame. Mtambo huu unaitwa “SSD”-Solid State Digester. Na nimaarufu sana hasa kwa maeneo mengi ya milima ya upare hasa Same na Mwanga. Ambayo yanaonekana ni makame na kuwa na maji hafifu kuhudumia mtambo.

Inaendelea……. . Mitambo hii imeleta sifa kubwa ndani na nje ya Tanzania na kuwapa watu fursa ya kujifunza namna ya kujenga mitambo hii na inavyozalisha gesi ya kutosha na hivyo kumrahisishia mtumiaji.

Muonekano wa mtambo wa biogas juu ya ardhi…. . CHEMBA YA KUINGIZIA MBOLEA Chemba ya majaribio Chemba Ya Kukorogea Chemba Mtanuko Mdomo wa kutolea mbolea

Je, hivi tumejenga mitambo mingapi? ? ? MWAKA 2009 50 MWAKA 2010 210 MWAKA 2011 300 MWAKA 2012 416 MWAKA 2013 528 MWAKA 2014 204

SEHEMU YA TATU TOPE CHUJIO-Bio slurry Na Utengenezaji wa Mboji-Compost Making

Nini maana ya tope chujio-Bio slurry. Ni masalia yaliyotolewa katika Mtambo(Biogas plant) inayotumika katika kuongeza rutuba katika udongo kwa ajili ya uzalishaji wa mimea. Inatokana na mtengano wa Viumbe hai katika mtambo wa biogesi.

Tope chujio ina sifa yeyote? ? Haina harufu na haiwavutii wadudu kama vile inzi nk. Tope chujio hushambulia mchwa na wadudu wote ambao wanavutiwa na samadi mbichi. Utumiaji wa tope chujio hupunguza kazi ya kupalilia. Matumizi ya tope chujio ipasavyo kupunguza kazi ya kupalilia kwa asilimia 50% Tope chujio ni bora katika kuhifadhi rutuba katika udongo, inaongeza virutubisho na kuiongezea ardhi uwezo wa kuhifadhi maji. Tope chujio inazuia bacteria. Uchakachushwaji wa samadi unaua bacteria zinazosababisha magonjwa kwa mimea.

UTENGENEZAJI WA MBOJI-COMPOST MAKING. Mboji ni kitendo cha kuvunja kemikali kutoka katika mimea na wanyama kwa ajili ya kuzalisha humus.

Kwanini tope chujio kwa utengezaji wa mboji? Tope chujio lina sifa ya; Virutibisho kwa mmea Kuimarisha udongo Umuhimu wa mboji katika kilimo. Mkulima anaweza akarutubisha ardhi yake kwa kutumia mboji iliyotengenezwa kutumia tope chujio. Inaongeza afya kwa udongo inayohitajika kwa mmea katika kiwango mahsusi.

Inaendelea…. . Faida zitokanazo na mboji Gharama nafuu na rahisi kupatikana Inasaidia kuboresha afya ya ardhi/udongo kwa muda mrefu Rahisi kueleweka na kuandaa Inasaidia kutopoteza maji haraka kwenye ardhi na kufanya ardhi kuwa na unyevu kwa muda mrefu. Humuongezea kipato mfugaji anapopeleka sokoni kwani ina soko zuri ikitegemewa na uhifadhi bora.

Wadau katika biogas. Katika utekelezaji wa biogas tumeweza kushirikiana na; KKKT dayosesi ya Same-kupitia mfuko wa Sabine Samekaya saccos. Mwanga Bank. World Vision.

Mbinu za kupata wateja Mbinu ambazo zinatumika ni kama ifuatavyo; 1. Mlango kwa mlango 2. Kutumia watu mashuhuru katika eneo husika 3. Kutumia mikutano ya hadhara. 4. Kutumia makanisa, misikiti ambapo ni rahisi katika kupata wateja.

Inaendelea…… Mgagao Ugweno Usangi Kisangara Gonja Bangalala Same Ibwe ijewa Ndenga Rombo Marangu-kyala Makanya Nadururu Mwembe. Toloha kigoni

Maeneo makuu tunayofanya kazi kwa milima ya pare Vudee Kirangare Makasa Same Kisiwani Bombo Lwami Jipe Hedaru kilomeni.

Changamoto za mradi. Kutolewa kwa ruzuku Uhudumu wa mtambo-kunakuwa na uangalizi mdogo katika ngazi ya katika kuuhudumia mtambo. Malipo kwa mafundi/kampuni. Usambazaji wa taarifa sahihi kuhusu mradi Uelewa mdogo wa wananchi juu ya biogas Uchumi kwa mwanchi mmoja.

Je Tumefanikiwa? FIDE tumefanikiwa kwa asilimia kubwa katika kueneza teknolojia na kupunguza uharibifu wa mazingira kwani wakazi wengi wanafurahia matumizi ya biogas na bio slurry/tope chujio katika kilimo na kukuzia mimea

BOQ VIFAA VINAVYOHITAJIKA KATIKA UJENZI WA MTAMBO WA SSD(6 M 3) 1. Kuchimbashimo……(Maelewanonamchimbaji) 2. Matofali. Madogo (23 cm/11 cm/7 cm) …. . 1200 3. Kokoto ……………. . …………………. . Debe 40 4. Mchanga ………………. …Debe 130 au nusu. Lory 5. Mawe……………. . . Meta 3 au Lori moja 6. Saruji ……………………. ……Mifuko 20 7. Chokaa………………………Mifuko 4 8. Water Proof Cement…………………. . . Mifuko 4 9. Wire-Mesh ………………. . ………. . Kipande (Kipandekimojawanatumiawatejawawili) 10. Chicken wire …………………meta 25 (Rolamoja la futisitawanatumiawatejawawili) 11. Bomba la PVC …………… Moja 12. Nondoya mm. 10 ……………. Moja 13. Kipande cha bomba la chuma/IPS. . . Metamoja 14. “T”-Joint + Plug…………………. . Mojamoja 15. Misumari. Nch 2 ………………. . ………Kilo Moja

VIFAA VINAVYOHITAJIKA KATIKA UJENZI WA MTAMBO WA MCD(6 M 3) VIFAA VINAVYOHITAJIKA KATIKA UJENZI WA MTAMBO WA MCD(6 M 3) 1. Kuchimbashimo… (Maelewanonamchimbaji) 2. Matofali. Madogo (23 cm/11 cm/7 cm)…. . 1000 3. Kokoto ……………. . ………………. Debe 35. 4. Mchanga …………………Debe 130 au Lorymoja. 5. Mawe……………. . Meta 3 au Lorimoja. 6. Saruji …………………. . ……Mifuko 15 7. Chokaa……………………Mifuko 3 8. Water Proof Cement…………. Mifuko 4 9. Wire-Mesh ………………. . . ……. Kipande 1. (Kipandekimojawanatumiawatejawawili) 10. Chicken wire …………………Meta 35. (Rolamoja la futisitawanatumiawatejawawili) 11. Bomba la PVC…………………Moja. 12. Nondoya mm. 10 ……………… Moja

Asanteni Na Karibu katika. Teknolojia Ya Biogesi BIOGESI KWA MAISHA

Imeandaliwa na; ADRIAN FOUNDATION CO. Ltd ‘for the quality community initiative’ P. o. Box 131, SAME, Tanzania adrianmnzava@gmail. com Adrian. mnzava@yahoo. com www. adrianfoundation. blogspot. com +255 692754026 +255 745699561
- Slides: 38