Mradi wa Kubadili Sekta ya Mkaa Tanzania Michael
Mradi wa Kubadili Sekta ya Mkaa Tanzania Michael Nilongo TTCS Project Officer TFCG 24/02/2016
Baadhi ya dondoo za nishati ya mkaa na kuni hapa Tanzania Takribani 90% ya nishati itumikayo Tanzania inatokana na tungamotaka (mkaa na kuni) (NBS, 2013) Zaidi ya tani milioni 2. 3 za mkaa zinatumika kwa mwaka hapa nchini Tanzania (MEM, 2014) Mchango kwenye uchumi wa nchi: takribani trilioni 2. 2 (Camco, 2013) Kiwango cha misitu kinachopotea kwa mwaka ni zaidi ya hekta 370, 000 kutokana na ufyekaji kwa ajili ya kilimo na matumizi yasiyo endelevu ya mbao, mkaa na kuni (NAFORMA, 2015)
Utangulizi Unatekelezwa na TFCG kwa ubia na MJUMITA, Ta. TEDO pamoja na wadau wengine Unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) Eneo la mradi: • Vijiji 10 katika Wilaya ya Kilosa (Awamu ya kwanza) • Vijiji vingine 10 (Kilosa), vijiji 5 (Morogoro vijijini) na vijiji 5 (Mvomero) – Awamu ya pili Muda wa Mradi: • Awamu ya kwanza: 01/03/12 – 31/08/14 • Kipindi cha mwaka 1 cha nyongeza: 01/09/14 – 30/11/15 • Awamu ya pili: 01/12/2015 – 30/11/2019
Mkaa Endelevu ni nini? • Kwa mujibu wa Mradi huu, Mkaa Endelevu ni mkaa unaozalishwa kwenye Misitu ya Hifadhi ya Vijiji ambayo iko katika Usimamizi wa Misitu uliojikita katika Jamii (CBFM) kwa kufuata taratibu zote za Usimamizi Shirikishi wa Misitu ikiwamo kutenga maeneo ya Misitu ya Hifadhi ya Vijiji katika kanda mbali ikiwa ni pamoja na kanda ya kuzalisha mkaa kwa njia endelevu. • Ni mkaa ambao namna ya ukataji wa miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu unazingatia kanuni zote za uvunaji endelevu ili kuongeza ukuaji wa miti ya asili baada ya kuvunwa • Mkaa huu huzalishwa kwa ufanisi mkubwa kutumia teknolojia ya matanuri yaliyoboreshwa.
Lengo la Mradi Kuanzisha mnyororo wa thamani wa biashara ya mkaa na mazao mengine ya misitu wenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza faida za kiuchumi zitokanazo na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na kuboresha utawala bora
Baadhi ya mafanikio makubwa katika awamu ya kwanza Kuanzishwa kwa mfumo wa mkaa endelevu ambao: • Umeongeza motisha zaidi kwa jamii kusimamia misitu yao kwa ufanisi zaidi • Umeongeza umilikaji wa rasilimali za misitu kwa jamii • Umewezesha jamii kujipatia mapato kwa mkaa unaovunwa kihalali na kiundelevu zaidi
Hekta 6, 040 za misitu ya miombo zimetengwa kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu ~ 10% ya Misitu ya Hifadhi za Vijiji
Wachom a mkaa: Milioni 138 Wilaya: Milioni 20 Vijiji: Milioni 239 Mapato katika vijiji
Mapato kutoka ushuru uliolipwa yanasaidia usimamizi wa misitu pamoja na miradi ya maendeleo ya vijiji. Ujenzi wa nyumba ya Mganga katika kijiji cha Ihombwe Miradi ya maendeleo ya vijiji inapitishwa na wanakijiji wote katika mikutano ya vijiji Ununuzi wa mfumo wa Sola kwa ajili Pikipiki kwa ajili ya timu ya doria na kamati ya zahanati ya Ihombwe ya maliasili
Ujenzi wa ofisi za vijiji Bima ya Afya kwa wanakijiji wote
Kilimo hifadhi na ufugaji wa kisasa wa nyuki
Kilimo Hifadhi kupitia mashamba darasa ya kilimo Mashamba darasa 13; zaidi ya wakulima 700 Wakulima wakufunzi 26 wamepewa mafunzo
Kuwezesha vikundi vya kuweka na kukopa (VICOBA) Vikundi 56 vikiwa na wanachama zadi ya 1, 228 wakiwemo wakufunzi 31 Wanajamii wanapata mikopo kwa ajili ya ufagaji kuku, kulima mboga, biashara ndogoetc
Biashara ya Mkaa Endelevu • Mradi umewezesha kuundwa kwa umoja wa wazalisha mkaa endelevu katika vijiji 10 vya mradi. • Mradi umewezesha uazishwaji wa vituo vya uuzaji wa mkaa endelevu katika kijiji cha Msimba • Uanzishwaji wa umoja wa wafanya biashara wa mkaa endelevu (UWAMAMAKI)
Biashara ya Mkaa Endelevu Taratibu za kisheria q. Mfanyabiashara anafanya usajili (TFS Wilaya) q. Mfanyabiashara anapeleka maombi ya kuvuna katika kijiji husika q. Mfanyabiashara anakata leseni ya kuvuna kijijini q. Mfanyabiashara analipia kibali cha kusafirishia (TFS) q. Mfanyabiashara analipia ushuru wa wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imewezeshwa kuwa na Mpango wa Uvunaji wa Wilaya. . . na mengine mengi!
Awamu ya pili inalenga nini? • Kuendeleza shughuli za usimamizi wa misitu ya jamii, uzalishaji mkaa na mbao kiundelevu, matumizi bora ya ardhi za vijiji pamoja na shughuli za kujikimu kimaisha kwa jamii katika vijiji 10 vya awali Kilosa • Kutanua wigo wa utekelezaji wa shughuli katika vijiji vingine 10 katika wilaya ya Kilosa, 5 Morogoro Vijijini na 5 Mvomero
Changamoto na Vikwazo Karibu mkaa wote nchini unatengenezwa bila kuangalia kiwango cha miti kilichopo; na bila kuwekeza na kuhakikisha kwamba kuna uchipuaji utakaoendelea baada ya kuvunwa. Hali ya “bure kwa wote” inazidi kudhorotesha uendelevu wa mkaa. Kutokuwepo kwa sera mahususi au mikakati ya nishati inayotokana na tungamotaka ya mkaa na aina nyingine ya nishati. Juhudi zaidi zinahitajika kusimamia uzalishaji wa mkaa na kufuatilia vyanzo vya mkaa unaofanyiwa biashara sokoni.
Ahsanteni kwa kunisikiliza!
Asanteni kwa kunisikiliza; Tanuri la Asili Kichuguu udongo
- Slides: 21