MKUTANO BAINA YA SIKIKA NA BARAZA LA MADIWANI
MKUTANO BAINA YA SIKIKA NA BARAZA LA MADIWANI Wilaya ya Kilolo Julai 30, 2016
YALIYOMO • • Sikika ni nani Maeneo ya shughuli za Sikika Malengo na Idara za Sikika Ngazi za utendaji Matarajio ya sikika toka kwa wadau Wadau wakuu wa SAM ni kina nani? Nini kila mdau afanye kuleta uwajibikaji Hitimisho
SIKIKA NI. . . • Asasi ya kiraia inayofanya kazi ya uchechemuzi na kuhimiza utawala bora kwa kufuatilia uwajibikaji katika Sekta ya Afya nchini. • Sikika ilianza mwaka 2009, kabla ilikuwa ikijulikana kama Youth Action Volunteers (YAV). Lengo la Sikika kufikia usawa katika upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote
MAENEO YA KAZI Sikika kwa mwaka (2010 -2015) ilikuwa ikifanya kazi katika wilaya 10, kwa sasa (20162020) inafanya kazi katika Wilaya 20: - • Mara: Musoma Mjini & Serengeti • Lindi: Lindi Mjini & Kilwa • Kigoma: Kigoma Mjini & Kasuru • Dar-es-Salaam: Kinondoni & Temeke • Dodoma: Mpwapwa & Kondoa • Singida: Ikungi & Singida rural • Manyara: Babati & Simanjiro • Kilimanjaro: Moshi rural & Siha • Iringa: Iringa Mjini & Kilolo • Mbeya: Mbeya Mjini & Chunya
MALENGO YA SIKIKA • Kuboreshaa bajeti ya afya inayolenga kumlinda mwananchi wa hali ya chini pamoja usimamizi wa fedha za afya. • Kuboresha ikama na weledi kwa watoa huduma za afya. • Kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya (health commodities) nchini. • Kuboresha usimamizi wa rasilimali fedha za umma (PFM).
NGAZI ZA UTENDAJI Sikika inafanya kazi katika ngazi mbali za serikali ambazo ni: NGAZI YA TAIFA (Serikali Kuu) NGAZI YA WILAYA (Serikali za Mitaa) NGAZI YA JAMII • Wizara ya Afya, TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Utumishi & Utawala Bora, Bunge (SSC, PAC), na CAG • Watendaji (DC, DED, CHMTs, WEO, VEO), Madiwani, Vituo vya huduma za Afya, Bodi na Kamati za Usimamizi wa vituo vya huduma ya Afya • Wananchi na Asasi za kiraia
SAM NI NINI? . . • SAM ni dhana shirikikshi kati ya wananchi (wenye wajibu na haki) na watendaji (wenye wajibu na dhamana), kwa pamoja kuhakikisha upatikananji wa mahitaji muhimu ya jamii • SAM inasimamia usawa, haki, uwazi, uwajibikaji na uadilifu wa watoa huduma katika kuhakikisha mahitaji ya jamii yanageuzwa kuwa haki muhimu za kibinadamu (Afya) ili kuboresha maisha • SAM inalenga kuwawezesha wanchi kupata haki zao bila ya ubaguzi kutokana na kuboreshwa kwa huduma za msingi kwa kutumia ipasavyo rasilimali zilizopo nchini
MFUMO WA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI KWA JAMII Social Accountability Monitoring (SAM) Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali Usimamizi wa Uwajibikaji Afya Haki ya Msingi ya Binadamu Usimamizi wa Matumizi Usimamizi wa Uadilifu kwa Umma Usimamizi wa Utendaji 8
TAARIFA ZINAZO TUMIKA KUFANIKISHA SAM • Mpango Mkakati wa Halmashauri • Mpango Kabambe wa Afya kwa Halmashauri (CCHP) • Ripoti za Utekelezaji wa Mpango wa Afya • Ripoti za Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI • Mihutasari ya Vikao vya Baraza la Madiwani • Ripoti za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG & Internal Audit) • Mpango wa Kati wa Matumizi ya Halmashauri (MTEF)
HATUA ZA UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA SAM 10 Ufuatiliaji Uwajibikaji Mikutano ya Jamii Mkutano na Baraza la Madiwani Mkutano wa Wadau - I Mafunzo na Uchambuzi Uhakiki Vituoni Kikao cha Ndani (CHMT/CMT) Mkutano wa Mrejesho (Wadau)
WADAU WAKUU WA SAM NI KINA NANI? Wadau wakuu wa SAM Muundo wa Timu ya SAM Wananchi 4 Madiwani PLHIV 1 Wakuu wa Wilaya Viongozi wa Dini 1 Watu wenye Ulemavu 1 Madiwani 2 WEOs 1 HFGCs 1 CHMT/CMT 1 CMAC 1 Bodi ya Afya 1 Taasisi za Ukaguzi - CAG Asasi za Kiraia 1 Asasi za Kiraia Jumla 15 Wakurugenzi (H) Wajumbe CHMT Watumishi wa Afya Bodi na Kamati za Vituo vya Afya Timu za SAM Wabunge
NINI WADAU WAFANYE KULETA UWAJIBIKAJI Wananchi • Waelewe vema mchakato wa mipango na bajeti • Washiriki na kufuatilia utekelezwaji wa bajeti • Kuhoji uwajibikaji juu ya mipango na maamuzi mbali ya watendaji, yenye maslahi kwa wananchi • Kudai taarifa za wazi kwa Umma na kutumia mfumo wa utoaji malalamiko
NINI WADAU WAFANYE KULETA UWAJIBIKAJI. . Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi • Wahamasishe umuhimu wa SAM • Kusisitiza malengo na ushiriki wa wananchi • Kusimamia uwajibikaji wa watendaji kulingana na mahitaji ya wananchi kupitia utekelezaji wa mipango • Kusaidia upatikanaji wa taarifa muhimu zinazowezesha utekelezajia wa SAM
NINI WADAU WAFANYE KULETA UWAJIBIKAJI. . CHMT na Wafanyakazi wa Afya • Kutengeneza bajeti na mipango inayogusa mahitaji ya wananchi • Kushirikiana na kamati za afya katika kuboresha huduma vituoni • Kusimamia maadili na ufanisi wa watoa huduma vituoni • Kuhakikisha upatikanaji wa watoa huduma vituoni • Kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vituoni • Kushirikisha jamii, asasi za kiraia katika kutoa huduma • Kusimamia uwazi wa taarifa za afya kwa wananchi
NINI WADAU WAFANYE KULETA UWAJIBIKAJI? . . Timu ya SAM ya Wilaya • Kuelewa mfumo mzima wa SAM • Kutekeleza SAM katika sekta ya afya na sekta zingine • Ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii • Muendelezo wa ujuzi wa SAM kwa wadau wengine • Kuhitaji maelezo na ufafanuzi juu ya maamuzi yanayofanywa na wawajibikaji kuhusu utoaji wa huduma za afya • Kutoa taarifa/mrejesho kuhusu matokeo ya SAM • Kusimamia uwazi wa taarifa za afya kwa wananchi
NINI WADAU WAFANYE KULETA UWAJIBIKAJI? . . . Madiwani/Wabunge • Kuielewa vema dhana ya SAM • Kuchambua na kuhoji taarifa mbali zinazowasilishwa kwa Baraza/Bunge • Kutumia taaluma ya SAM kushawishi mgawanyo sawa wa bajeti za Halmashauri hususani katika sekta ya Afya • Kusimamia uwajibikajiwa wa watendaji wa halmashauri • Kusimamia uwazi wa taarifa na upatikanaji wa nyaraka kwa umma hususani timu ya SAM
HITIMISHO • Kila mdau ana nafasi kubwa ya kusimamia utekelezaji wa uwajibikiaji kwa jamii • Na kila mdau ana umuhimu wa pekee katika kutekeleza uwajibikaji • SAM ni njia muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa haki ya kupata huduma za msingi za binadamu (human right and capabilities)
ASANTENI KWA KUSIKILIZA
- Slides: 18