MIHURI SABA Somo la 5 kwa ajili ya
MIHURI SABA Somo la 5 kwa ajili ya Februari 2, 2019
FUNGU KIONGOZI “‘Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. ”’ (Ufunuo 5: 9, 10, SUV)
Ujumbe wa Mihuri Saba ni Muhtasari wa historia ya Kanisa tangu mwanzo hadi kurudi kwa Yesu mara ya pili. Mihuri inafuata mfano ule wa kihistoria alioutumia Yesu katika Mathayo 24. MATHAYO 24 Dalili za mapema (4 -14) Dhiki (21 -22) Ishara juu ya anga (29) Mwana wa Adamu aonekana (30) Ufunuo 6 Vita, matetesi ya Vita, njaa, Tauni, Injili kuhubiriwa, Upanga, Njaa, Tauni. Wapanda Farasi wanne (6: 1 -8) Dhiki Kuu Roho chini ya madhabahu wakilalamikia dhiki zao Muhuri ya tano (6: 9 -11) Jua, Mwezi, Nyota na nguvu za Mbingu Ishara katika Jua, Mwezi, Nyota na Mbingu Ishara juu ya mbingu, dunia kuomboleza Watu wanajificha kutoa kwenye hasira ya Mwanakondoo Muhuri ya sita (6: 12 -17)
Mwenye uhai Farasi Mpanda farasi Alipewa wa kwanza Mweupe ana uta Taji wa pili Mwekundu Mweusi 5 -6 wa tatu 7 -8 wa nne Kipindi (BK) 31 -100 3 -4 1 -2 aya Wa kijivu Alipewa kuiondoa amani katika nchi Alikuwa na mizani mkononi mwake Jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye Upanga mkubwa 100 -313 Maelekezo juu ya gharama ya chakula Mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, kwa njaa, kwa tauni na kwa hayawani wa nchi. 313 -538 538 -1517
“Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda. ” (Ufunuo 6: 2) Muhuri ya kwanza ilifunguliwa, na Yohana aliona farasi mweupe. Naye aliyempanda alipepea kwa silaha (uta) na kushinda (taji). Farasi huyu ni ishara ya kanisa la Awali. Kanisa la Awali lilipokea nguvu siku ya Pentekoste na “wakaenda wakiwa washindi na kushinda” Ni miaka 30 tu baada ya kifo cha Yesu, Paulo alisema kwamba Injili “ilihubiriwa katika viumbe vyote chini ya mbingu. ” (Colossians 1: 23)
MUHURI YA PILI “Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa. ”(Ufunuo 6: 4) Yesu alikuwa ametabiri kuwa Injili itakumbana na Upinzani kutoka kwa nguvu za Mwovu (Mathayo 10: 34). Himaya ya Kirumi iliua Wakristo wengi na kumwaga damu nyingi ya mashahidi tangu karne ya pili. Mauaji yalikuwa makali wakati wa utawala wa Diocletian, Maximian, Galerius na Constantius. Kipindi hicho kiliisha pale Constantius alipositisha mauaji.
MUHURI YA TATU “Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti kati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai. ’” (Ufunuo 6: 5 -6) Nyeusi ni kinyume cha Nyeupe. Usafi wa Injili ya farasi mweupe ulipotoshwa wakati wa kipindi kati ya mwaka 313 BK na 538 BK. Njaa na umasikini vingeteketeza wafanyakazi kama kibaba cha ngano kilivyogharimu mshahara wa kazi ya siku nzima. Biblia ilitelekezwa, na watu wakaathirika kwa njaa ya Neno la Mungu (ngano na shayiri). Hata hivyo, bado Mungu alitoa wokovu kupitia Roho Mtakatifu (mafuta) na damu ya Yesu (divai).
MUHURI YA NNE “Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivu, na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”(Ufunuo 6: 8) Rangi ya huyu farasi ni rangi ya mpauko wa maiti anayeoza. Ni ishara ya kufa kiroho kama madhara ya kuitelekeza Biblia na kanuni za Injili. Hii ni sawa na wakati wa kipindi cha ujumbe kwa kanisa la Thiatira, kanisa lililokufa kiroho. Adhabu mpya (mauti na hayawani) zimeongezwa kwa zilizotangulia (upanga na njaa). Labda hili ni jaribio la Kiungu la kuliamsha Kanisa na kulifanya litoke katika uasi (Walawi 26: 21 -41).
MUHURI YA TANO “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. ” (Ufunuo 6: 9) Katika Hekalu, damu ya waathirika ilimwagwa kwenye madhabahu ya kuteketeza (Walawi 4: 25). Hapo ndipo Yohana—Kiishara—aliona watu (roho, angalia 1 Wafalme. 15: 29) waliouawa na Kanisa la Rumi kwa sababu ya Imani zao. Wale waaminifu walitazamwa kwa wamestahili (angalia Ufu. 3: 4) na walihakikishiwa kuwa Mungu hajawasahau. Wasubiri muda mchache hadili pale kila kesi itakapoamuriwa na ndipo Kristo arudi tenan “ kumlipa kila mmoja kadri ya kazi yake. ” (uf. U. 22: 12) Kwa wakati huo, watafufuliwa na kuungana na “wajoli wao na ndugu zao. ”
MUHURI YA SITA “Nami nikaona, alipoifunga muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeus kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu. ” (Ufunuo 6: 12) Dalili ambazo aya hii inatabiri zilitimia vile kama zilivyopangiliwa: 11/1/1755 Tetemeko la Lisbon 19/5/1780 Giza nene kuanzia saa 4 asubuhi 19/5/1780 Mwezi kuonekana kutiwa damu 13/11/1833 Kuanguka kwa kimondo kikubwa Tunaishi katika kipindi cha wakati wa Muhuri ya sita, hadi hapo kila mtu atakapoijua kweli ya Injili. Wale wanaoikataa kweli watataka kukimbia kutoka mbele ya uwepo wa Mwana-kondoo. “Na ni nani atakaeweza kusimama? ” Tutapata jibu la swali hili katika Sura ya 7.
“Ulimwengu unapotea kwa kukosa Injili. Kuna njaa ya neno la Mungu. Wapo wachache wanaolihubiri neno ambalo halijachanganywa kwa tamaduni za kibinadamu. Japo wanadamu wana Biblia mikononi mwao, hawapokei mibaraka ambayo Mungu ameiweka ndani yake. Mungu anawaita watumishi wake wabebe ujembe na kuupeleka kwa watu. Neno la uzima wa milele ni lazima litolewe kwao wanaoangamia dhambini. ” E. G. W. (Christ’s Object Lessons, cp. 18, p. 228)
- Slides: 11