Mafunzo ya Biashara Ujasiriamali MALENGO YA KUNGAMANOWARSHA Kuhamasisha
Mafunzo ya Biashara Ujasiriamali
MALENGO YA KUNGAMANO/WARSHA ◊ Kuhamasisha mawazo ya kibiashara ili kuonyesha umuhimu wa kutofautisha biashara na mtu mwenye kuiendesha. ◊ Kuchambua mazingira yanayoizunguka biashara. ◊ Kutoa mwangaza kwa mfanyabiashara katika kufahamu uwezo na udhaifu alionao katika mazingira ya kibiashara yanayomzunguka na yanayohusiana na biashara yake. Mfano, vizuizi vinavyoweza kuzuia ukuaji wa biashara ◊ Kumwezesha mfanyabiashara kubuni na kutekeleza suluhisho la matatizo hayo ◊ Kuwaelimisha washiriki kuhusu nafasi za biashara (Business opportunities) zilizo katika eneo na kuzichambua ◊ Kumwezesha mfanyabiashara kufikia hatua ya kubadilisha aina ya biashara au kuanzisha biashara mpya kabisa kulingana na uwezo alionao, rasilimali au malighafi zilizopo, soko, ujuzi na ushindani uliopo ◊ Kuwezesha washiriki kutambua mchango wa jinsia katika maendeleo ya biashara na athari za ukimwi ◊ Kuwezesha washiriki kutambua mbinu mbali za masoko, soko na utafiti wa soko ◊ Kuelimisha na kuhamasisha wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia njia mbali za kupata mtaji, kujiwekea akiba kwa ajili ya matumizi ya binafsi, na kama njia mojawapo ya kupata kianzio/kuimarisha biashara
BIASHARA NI NINI? • Ni shughuli yoyote ile halali ya kuuza na kununua bidhaa au huduma kwa ajili ya kupata FAIDA
MFANYABIASHARA NI NANI? • Ni mtu yoyote aliyejiari kufanya shughuli yoyote halali ya kuuza na kununua bidhaa au huduma kwa ajili ya kuapata FAIDA
• Ujuzi/Elimu • Tekinolojiaa • Muda muafaka
MAMBO MUHIMU KABLA YA KUANZA BIASHARA • • Watu Kipato Uwezo Mahitaji Mahali Washindani Malighafi
(a) Maana ya Ujasiriamali na Mjasiriamali Ujasiriamali ni ubunifu au ugunduzi au uundaji wa wazo na kuliweka katika matendo ya kiuzalishaji mali au utoaji wa huduma. Jasiriamali au mjasiriamali ni mtu ambaye anajishughulisha na biashara kwa njia ya kumwezesha kumudu maisha yake kiuchumi na kijamii Mbunifu ni mtu anayefikiria na kugundua biashara mpya, kuinzisha, kuikuza, kuvumilia matatizo yake na anafaidikanna biashara hiyo.
(b) Sifa za Mjasiriamali mwenye mafanikio Kwa ujumla mjasiriamali mwenye mafanikio huwa na sifa zifuatazo: -
1. Kila mara anatafuta nafasi za kibiashara 2. Mvumilivu 3. Huheshimu mikataba ya kazi. 4. Hutaka ufanisi na kazi iliyo bora 5. Hujitosa (bila kuogopa) 6. Hujiwekea malengo 7. Hupenda kutafuta taarifa mbali 8. Huwa na mipango thabiti na hufuatilia utendaji wa kazi 9. Ana uwezo mkubwa wa kushawishi na hutumia mtandao wa wafanyabiashara 10. Hujiamini
TABIA • Kujiamini, uhuru na mwenye malengo • Mhitaji mafanikio kama vile faida • Utayari wa kubeba hasara/matatizo ya wastani kama vile changamoto • Mwenye uwezo wa kuongoza, mwenye Kufanyia kazi ushauri na vikwazo • Mvumbuzi, mwenye mawazo safi/Mwanana na mwenye busara.
• Aiangalie biashara yake kwa baadaye • Mwenye mtizamo wa mbele katika kupanga • Anatunza na kuheshimu makubaliano.
JAMII SOK O WAGAVI BIASHARA NDOGO WAFANYAKA ZI BENKI SERIKALI
KANUNI SABA ZA MFANYABIASHARA 1. Angalia ukweli wa mambo 2. Fanya biashara kwa majaribio lakini punguza uwezekano wa kupata hasara 3. Lenga shabaha kwa mteja wako 4. Kuwa mbunifu 5. Kuwa jasiri na mwenye kuipenda biashara yako 6. Jenga uhusiano mzuri 7. Fahamu vizuri wakati uliopo na wakati ujao
SOKO/ MASOKO
SOKO NI NINI? • Mteja au mahali MASOKO NI NINI? • Jumla ya shughuli zote tangu mwazo wa biashara hadi kukidhi mahitaji ya mteja
NJIA 4 ZA KUTAMBUA SOKO LA BIDHAA YAKO 1. 2. 3. 4. Shida/uhitaji Mapenzi ya kuwa na kitu fulani Uwezo wa kununua Mapungufu ya bidhaa nyingine
PEMBE TATU ZA SOKO WATEJA BIDHAA BEI BANDA BANGO BIDHAA/HUDU MA WASHINDA NI
B 4 1. BIDHAA Inahusu uasili (nature), mtindo wake (design), jina la kibiashara (Brand name) na ufungashaji (packaging). 2. BEI Hii inahusu hasa bei ambayo bidhaa inauzwa. Bei ni thamani ya kifedha ambayo huwekwa katika kulinganisha umbo, thamani ya matumizi na mafao kwa mtumiaji. 3. BANDA Ni mahali ambapo bidhaa huhifadhiwa na kuuzwa. Mahali panaweza kuwa kwenye nyumba yako au kwenye nyumba ya kukodisha au sehemu maalum kwa ajili ya soko (gulio) 4. BANGO Hii ni namna na ujanja ambao bidhaa hutangazwa. Ni muhimu kutangaza bidhaa au huduma ambayo unauza kwa wateja wako.
NJIA 7 ZA UTANGAZAJI KWA GHARAMA NAFUU 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. Motisha Matangazo Kuonyesha kwa vitendo Zungumza kuhusu bidhaa au huduma yako Fadhili timu (Hisani) Fadhili mashindano Andika makala
Kutoa Huduma Bora Kwa Mteja Wako
MTEJA NI NANI? v Mteja ni mtu au tasisi yoyote ambaye tuna uhusiano naye katika biashara. Si lazima mteja awe ni yule anayenunua bidhaa au huduma kutoka katika biashara yako leo. v Hata yule mtu anayekuja kuulizia au kutembelea biashara yako ni mteja vile.
Vidokezo vya kujenga uhusiano mwema na wateja. Kila mara msalimie mteja na kisha muulize “ Naweza kukusaidia”? • Kwanza jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Sikiliza na kuelewa. • Kama hujaelewa, uliza ili kukidhi haja ya mteja. • Kuwa mkarimu kwa wateja wote. Wahudumie kwa tabasamu. Watimzie wanachotaka kwa utaratibu ulio wazi. • Wahudumie wateja kwa makini. • Ruhusu wateja wazijaribu bidhaa zako (inapobidi). • Kubali malalamiko na ujibu kwa uangalifu. • Zungumza kidogo, onyesha zaidi. • Uza manufaa, siyo bidhaa pekee. • Kila mara jaribu kuwa na subira, kwasababu wateja wengine ni wazito kuamua.
MAMBO YASIYOFAA a) b) c) d) Usibishane na mteja Usimchanganye mteja kwa maelezo mengi mno. Usimuuzie mteja zaidi ya kile anachoweza kutumia Usikate tamaa mteja anaposema kwamba bei ni kubwa mno. Badala yake mweleze manufaa atakayopata e) Usimlazimishe mteja kununua, bali mshawishi. f) Usimkatize mteja anapozungumza, yeye ndiye mfalme. g) Usunywe, usivute, wala usile unapokuwa unauza, hivi ni vitendo vinavyoweza kumkera mteja.
Mambo Ambayo Huweza Kuharibu Uhusiano Na Wateja……. . • • • Uso wenye hasira Uso unaoonyeha kusononeka au kuchoka. Kutojali mteja anapokuja Kutoa huduma kwa upendeleo Kuonyesha kutokuwa na ujuzi katika utoaji huduma • Kutoa huduma pole sana • Lugha isiyofaa
• Kukejeli wateja • Kumdai mteja kitu kilicho nje ya utaratibu ndipo huduma itolewe • Kutotekeleza ahadi
………Mambo Ambayo Huweza Kuharibu Uhusiano Na Wateja • Kupokea zawadi kutoka kwa wateja (zenye nia ya kutoa upendeleo) • Kujenga mahusiano ya kimapenzi na wateja • Kutowatimizia wateja mahitaji yao • Kupiga soga wakati wateja wanasubiri • Kutoa huduma huku umelewa. • Kushindwa kutoa faraja kwa wateja wakati inapobidi wasubiri huduma.
• Kuweka vibaya, kuharibu au kupoteza vitu vya wateja. • Kuwazungusha wateja badala ya kutoa huduma moja kwa moja
Huduma/kujali wateja • • • Kujali wateja ni kuwa na mwelekeo wa kumwona mteja kuwa ndiye damu ya shughuli/huduma. Kwani bila mteja hakuna mauzo yatakayofanyika, Hivyo kutokuwepo “biashara asilani”. Hivyo ni kusema kuwa biashara/huduma iuzwayo lazima imuweke mbele mteja na wala siyo fedha!. Kujali wateja ni kuhakikisha kuwa mteja anaridhika na kufurahia huduma aipatayo.
Maana Ya Kumridhisha Mteja ‘Mteja Anakuwa Ameridhika Ikiwa Mahitaji, Matakwa Na Matarajio Yake Yamekidhiwa’.
MATARAJIO YA MTEJA • Kupata hitaji • Unategemea mazingira safi, mapokezi mazuri,
NINI UMUHIMU WA MTEJA? Mteja ni mtu/ taasisi muhimu sana kwa mfanyabiashara yeyote. Hii inatokana na ukweli kuwa mteja. • Ndiyo chimbuko la biashara yoyote, na bila yeye hakuna biashara itakayofanyika. • Ndiyo damu ya biashara. (je, mwili ukikosa damu-nini matokeo). • Ndiyo malipo ya mishahara (fedha tunazowatoza ndizo hutupa mishahara).
Aina za Wateja…… • • • Wabishi Wenye duku Wanaopenda Sitaha Wasioamua upesi Wenye haraka Wenye bugdha
……. . Aina za Wateja • • • Wanaopenda kusifiwa Wagumu kuelewa Wenye hasira Wateja wakimya Wateja wacheshi.
Hasara Za Kutomridhisha Mteja (Husasani Wanafunzi) • • • Picha mbaya ya Ofisi yako ktk jamii Migomo Maandamano Ugomvi Matusi Kupoteza Ajira Ari ya wafanyakazi kwenda chini Kutengeneza uadui N. k
Faida za kuridhisha wateja • Wateja wanaporidhika inakuwa rahisi hata kulipa bei ya juu zaidi na hivyo kuleta faida zaidi. • Wateja walioridhika husambaza sifa nzuri za biashara na hivyo kuleta wateja wapya. • Wateja wa zamani hurudi tena.
• Kuongezeka kwa wateja huongeza mauzo na faida pia. • Wateja wakiridhika huongeza hata ari ya mfanya biashara na wafanyakazi, na hivyo kuboresha zaidi utendaji kazi wao.
Namna Ya Kufanya Mara Mteja Anapofika Kwenye Biashara Yako • Msikilize vizuri ili ujue mahitaji yake. Kama hujaelewa, uliza. • Onyesha ukarimu na mhudumie mteja kwa tabasamu. • Mhudumie mteja kwa makini. • Kubali malalamiko na ujibu kwa uangalifu • Zungumza kidogo, Sikiliza zaidi. • Kila mara jaribu kuwa na subira, kwa sababu wateja wengine ni wazito kuamua.
Mambo Ya Ziada Ya Kumtendea Mteja • Ubadilishe salamu/kufuatana na vile mteja aelekeavyo. • Kuwa na tabia sahihi/adilifu. • Kujiamini. • Fikiria kwa makini. • Onyesha hisia kuwa unapenda kumsaidia mteja. • Jaribu kugundua mambo anayopendelea mteja hata bila yeye kuyasema. • Weka mazingira yatakayojenga uhusiano na mteja hata kwa baadaye.
Kushughulikia Malalamiko Ya Wateja • Hakikisha umefahamu vizuri malalamiko yaliyoletwa kwako. • Omba radhi hata kama makosa ni ya mwenzio. • Kama mteja ana malalamiko mengi, shughulikia moja huku ukimhakikishia kwamba malalamiko yake yote yatashughulikiwa. • Kama unadhani uwezo wako wa kutatua tatizo la mteja umefika mwisho, usiendelee kumchelewesha bure, mhusishe mtu mwingine ambaye unadhani ataweza kuleta utatuzi.
• Wafuatilie wateja wako ili uone kama wameridhika kwa kuongea nao, kuwapigia simu au kwa mawasiliano mengine yo yote
Sifa Za Mtoaji Huduma Anayefaa…. • Anatambua kwamba mteja ndiye uti wa mgongo wa Kazi yake. • Anakuwa nadhifu na mtanashati. • Husalimia wateja na kuwapokea vizuri • Daima huwa na uso wenye tabasamu. Haonyeshi kuchoka, hasira, kusononeka au uso wenye kukunjamana. • Anamjali kila mteja anayekuja na kutoa huduma bila upendeleo.
• Anakuwa na ujuzi katika kazi yake na anawapa imani wateja kwamba huduma yake ni ya uhakika • Anatoa huduma kwa kasi inayotakiwa bila kuwachelewesha wateja.
…. . Sifa Za Mtoaji Huduma Anayefaa • Ni mcheshi, anatumia lugha nzuri na anaonyesha upendo kwa kila mteja. • Anasikiliza na kutatua matatizo ya wateja bila kudai au kupokea zawadi au malipo ya ziada. • Anatoa ahadi za kweli na ambazo anazitekeleza. • Haonyeshi tamaa mbaya kama vile kutaka uhusiano wa kimapenzi na wateja. • Anaepuka tabia zinazoweza kuleta kero kwa wateja kama vile kulewa akiwa kazini.
• Hamkatishi mteja anapoongea. Anakuwa na subira na uvumilivu kwa wateja. • Hamng’anizi mteja kununua kitu, bali humshawishi.
Kujipima Mwenyewe 1 = Hata kidogo; 2 = Mara chache; 3 = Mara nyingi; 4 = Wakati wote • Huchoshwa na wateja wenye maswali mengi. • Hutoa huduma kwa upendeleo • Ninapoudhika huonyesha wazi kwa wateja . . . . • Huwaomba radhi wateja hata kwa makosa ya wenzangu . . • Hujibu kiungwana hata penye kauli zinazokera . . • Huwafukuza wateja wenye kauli za kipuuzi . . • Sifichi hisia zangu hata kama zitawaudhi wateja . .
• Huwafurahia wateja wote, hata wale wakorofi . . . • Hutoa ushauri na maelekezo pale ninapohitajika . . . • Hushughulikia malalamiko ya wateja mara tu inapoletewa ………. .
Mtaji ni nini? 1. Kiasi cha fedha ambacho mfanyabiashara amewekeza kwenye biashara yake kwa ajili ya kupata faida. (Equity)
• Fedha taslim + Rasimali - Majengo - Vifaa/zana - Malighafi - Mkopo - Utashi/nguvu kazi/ afya njema NOTE; - CAPITAL = Liability (MADENI) + Equity
Aina za Mitaji ya Biashara • Mitaji ya Kudumu 1. Vitendea kazi 2. Majengo 3. Magari
• Mtaji Unaozunguka 1. Bidhaa 2. Pesa 3. Mauzo kwa mkopo (wadaiwa)
Gharama au matumizi ya uendeshaji biashara Gharama zinazobadilika Gharama funge (zisizobadilika) Biadhaa kwa ajili ya kuuza Kodi ya pango, maji, nishati n. k Usafiri Leseni Ujira Mishahara
Mtiririko wa Mtaji Pesa taslimu na Benki Makusanyo kwa wadaiwa Bidhaa kwa ajili ya kuuzwa Mauzo kwa pesa taslimu na mkopo
Kumbuka • Kadri mzunguko unavyo kimbia haraka ndivyo biashara inakuwa ya faida
AINA ZA MITAJI NA VYANZO VYA MITAJI • Mtaji kutokana na Hisa • • • Zinazotokana na umiliki wa, Ardhi Majengo Vifaa Mali ghafi Fedha taslim
NJIA AMBAZO UNAWEZA KUJIJENGEA MTAJI WAKO BINAFSI • • • Kufanyakazi na kujiwekea sehemu ya ujira akiba Kulima na kujiwekea sehemu ya mazao kama akiba Kufuga mifigo na kujiwekea mifugo ya ziada kama akiba. Kufungua na kuendesha akaunti ya akiba ya muda maalumu. Msaada kutoka kwa wazazi au ndugu. Viingilio na hisa lama ni ushirika Upatu ama mchezo ama kuweka na kukopeshana katika kikundi. Amana zinazotoka kwa wanakikundi. Bahati nasibu (Ingawa hii si ya kutegemea). Kujiwekea vito vya thamani.
VYANZO VYA MTAJI KUTOKA NJE YA BIASHARA. • Taasisi za fedha, mfano mabenki • Wafanyabiashara, kwa kutoa mikopo ya bidhaa, fedha au vyote viwili. • Idara za serekali mfano Mikopo maalum kwa ajili ya wanawake, vijana, mfuko wa Rais wa nguvukazi na kadhalika. • Mashirika yasiyo ya kiserekali mfano: PRIDE Tanzania, Oxfam, Poverty Africa, SEDA, ADF kwa vikundi, mfuko maalum wa vijana na kadhalika. • Jamaa, ndugu na marafiki, hiki ndicho chanzo kinachotumika sana nchini Tanzania.
UNATAKIWA KUZINGITIA NINI ILI UWEZE KUJIJENGEA MTAJI WAKO BINAFSI? • Kukubali kuwa unayo shida ya mtaji. • Chagua chanzo cha mtaji. • Fanya hesabu ili ufahamu biashara inahitaji kiasi gani cha mtaji. • Amini kuwa vyanzo hivyo ulivyochagua ndivyo hasa vitakupatia mtaji. • Dhamiria kujijenga mtaji wako binafsi. • Tekeleza nia yako kwa kujijenga mtaji kiasi cha kutosha mahitaji ya biashara yako. • Anza biashara.
Mtaji wa kukopa • • • Fedha iliyokopwa + riba Mkopo kutoka kwa wagavi Ndugu Marafiki Asasi za fedha Mikopo ya biashara
Kupata pesa taslimu kwa ajili ya biashara nje ya biashara Weka Akiba katika biashara Pata mkopo kutoka kwenye taasisi za fedha au kutoka kwa familia na marafiki Omba mkopo wa bidhaa Ahirisha ulipaji wa kutoka kwa wagavi malipo yoyote mpaka muda unapowadia, likini angalia usiharibu mahusiano mema na wagavi
Kupata Pesa taslimu kwa ajili ya biashara kutokea ndani ya biashara Kudhibiti uchukuaji pesa na biddaa kwa matumizi binafsi Punguza bidhaa ambazo “zinasinzia” (Bidhaa zisizonunuliwa haraka) Kudhibiti kiwango cha ukopeshaji wa bidhaa kwa wateja na kukusanya madeni kutoka kwao mara muda unapowadia Punguza matumizi ya pesa yasiyo ya lazima
MATUMIZI YA MTAJI Ø Mtaji wa kudumu Ø Ardhi, Majengo, Vifaa Ø Mtaji wa kuendeshea matumizi ya kila siku ya kibiashara. Ø Kununua malighafi/bidhaa, kodi, uvumishaji, matengenezo, usafirishaji
MKOPO NI NINI? Mkopo ni utaratibu ambapo mjasiriamali/mfanyabiashara anaweza kupata mali/fedha kwa makubaliano kuwa mali/fedha anazokopeshwa zitarejeshwa na riba baadaye/kwa utaratibu Fulani uliokubaliwa kati mkopeshaji na mkopaji.
FEDHA/MALI Mkopo ni fedha au mali ambayo inaweza kuuzwa na kupatikana fedha. Mali ama fedha anazokopeshwa mteja zinategemewa kuleta mabadiliko kiuchumi kwa mkopaji, hivyo ni lazima mkopaji aonyeshe ulazima/umuhimu wa yeye kukopeshwa kuelekeza/kuonyesha matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na riba inayozalishwa na mkopo huo.
MAKUBALIANO • Makubaliano ni maridhiano yaliyofikiwa kati ya pande mbili, yaani mkopaji na mkopeshaji. • Makubaliano hayo hujengwa na uaminifu unaotarajiwa kutoka pande zote mbili. Hivyo uaminifu ni msingi wa wa maridhiano yanayozaa mkopo.
MAREJESHO • Marejesho ni kiasi cha fedha/mali kilichokubalika kati ya mkopeshaji na mkopaji ambacho chatakiwa kurejesha kwa mkopeshaji kikiwa na kiasi cha riba kilichokubalika kwa kipindi maalum. • Marejesho ni lazima yaambatane na riba. Hivyo ni muhimu kwa mkopaji aelewe na kuzingatia muda muafaka wa kurejesha ili kuepuaka madhara yatokanayo na ucheleweshaji wa kurejesha.
SABABU ZA KUSHINDWA KULIPA MIKOPO i) Kutoweka akiba mara kwa mara. Ili kuweza kumudu maisha na kulipa deni, akiba ndio pekee ya kukabili mkopo. ii) Mpango madhubuti wa kulipa. Ieleweke kwamba ni rahisi kuweka fedha za kulipa iwapo mapato yanazidi matumizi. Hivyo ni muhimu kuongeza mapato na kupunguza matumizi wakati wa kulipa mkopo. iii) Miradi mbadala Biashara inaweza kufanikiwa au kutoifanikiwa kutokana na matakwa ya wateja na ushindani. Hivyo ni muhimu kuwa na uwezo wa kubadili biashara au kuanzisha biashara mbali, kupunguza uwezekano wa kukosa fedha ya kulipia mkopo.
FAIDA ZA KULIPA KWA WAKATI v Riba inapungua v Unakwepa usumbufu v Uwezekano wa kupata mwingine
ATHARI ZA KUTOLIPA KWA WAKATI • Riba inaongezeka • Hisia ya hatia • Mkopaji asiyelipa anakuwa na wasi kila mara kuwa atakamatwa na kuabishwa • Hatua za kisheria • Mkopaji asiyelipa yupo katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kikuika mkataba • Inakuwa vigumu kupata mkopo mwingine • Ikiwa mkopaji hajalipa mkopo wa mwanzo, haiwezekani kumwongezea mzigo wa mkopo mwingine.
UTUNZAJI WA KUMBU Utunzaji wa kumbu nini? Utunzaji wa kumbu ni utaratibu wa uwekaji wa kumbu za biashara; kuonyesha jinsi fedha inavyoingia na kutoka.
Umuhimu wake; Umuhimu wake ni kumwezesha mfanyabiashara kufuatilia utekelezaji wa biashara yake kwa kujua mambo yafuatayo: - Mali iliyopo kwenye biashara Mzunguko wa fedha katika biashara Jumla ya mapato na matumizi Gharama za uendeshaji wa biashara Faida inayotokana na biashara Kujua kama biashara inaendelea vizuri au inarudi nyuma. - Ukadiriaji wa kodi ya mapato
Kumbuka; sheria za nchi, Income Tax Act 1973, ndiyo inayoelekeza hivyo.
MAELEZO YA DAFTARI YA TASLIMU - Fedha inayoingia/pokelewa inaongeza kiasi cha fedha kilichopo kwenye biashara. Fedha inayolipwa hupunguza fedha iliyoko kwenye biashara. Fedha inayopelekwa benki hupunguza fedha iliyoko mkononi lakini huongeza fedha yako iliyoko benki. Vivyo hivyo fedha inayochukuliwa toka benki hupunguza fedha yako iliyoko benki lakini huongeza fedha iliyoko mkononi. Kutokana na kutunza kumbu vizuri baki ya fedha itakayoonyeshwa na kitabu chako lazima ilingane na fedha taslimu mkononi wakati ule. Salio la mwisho: - Katika daftari ya taslimu yapo masalio ya mwisho mawili katika safu mbili tofauti. Kwanza kuna salio la mwisho taslimu pili salio la mwisho benki. Jinsi ya kupiga hesabu na kuelewa kiasi cha salio la mwisho taslimu. Unaweza kufanya hivi kwa kuangalia hesabu zako kila siku jioni na kuzilinganisha kiasi cha fedha kilicho kwenye kasha.
DAFTARI YA TASLIMU TAREHE MAELEZO TASLIM/MKONONI Fedha Ingia Fedha Toka Salio BENKI/KIKUNDI Fedha Ingia Fedha Toka Salio
KUMBU ZA MATENDO BIASHARA KWA MKOPO • Mauzo kwa mkopo maana yake ni: • Tendo la kuuza bidhaa bila ya kupokea malipo yoyote wakati ule. • Manunuzi kwa mkopo maana yake ni: • Ni tendo la kununua bidhaa bila ya kulipia fedha taslimu au hundi wakati ule.
Kumbuka: • • • Mauzo au manunuzi yanayofanywa kwa mkopo, huwa hayaandikwi katika daftari ya mauzo taslimu isipokuwa katika daftari zilizotajwa hapo juu. Jumla ya mauzo kwa mkopo kwa mwezi unaohusika kutoka safu ya kiasi INGIA cha daftari ya mauzo kwa mkopo ukijumlisha na manunuzi taslimu kwa mwezi unaohusika kutoka daftari ya taslimu hukupatia jumla ya manunuzi kwa mwezi unaohusika. Jumla ya wanaodaiwa kwa mwezi unaohusika ukijumlisha na mauzo kwa fedha taslimu kwa mwezi unaohusika hukupatia jumla ya mauzo kwa mwezi unaohusika. Salio la deni unalodaiwa au unalodai linaonyeshwa katika safu ya mwisho katika daftari linalohusika. Kiasi kilicholipwa kwa wadai katika kipindi cha mwezi unaohusika huonekana katika daftari ya taslimu safu ya kiasi toka hivyo kupunguza kiasi cha fedha mkononi au benki kutegemea na njia ya malipo. Kiasi kilichopokelewa kutoka kwa wadaiwa katika kipindi cha mwezi unaohusika kuonekana katika daftari ya taslimu safu ya kiasi Ingia hivyo kuongeza kiasi cha fedha mkononi.
DAFTARI LA MAUZO KWA MKOPO JINA LA NINAYEMDAI -------------TAREHE MAELEZO NAMDAI Tshs AMELIPA Tshs SALIO Tshs SAHIHI
DAFTARI LA MANUNUZI KWA MKOPO JINA LA ANAYENIDAI ……………… TAREHE MAELEZO ANANIDAI Tshs NIMEMLIPA Tshs SALIO Tshs SAHIHI
- Slides: 85