MACHO YA BWANA MTAZAMO WA KIBIBLIA WA ULIMWENGU
“MACHO YA BWANA”: MTAZAMO WA KIBIBLIA WA ULIMWENGU Somo la 4 kwa ajili ya Oktoba 24, 2020
“Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema” (Mithali 15: 3)
Mtazamo wa kiulimwengu ni njia ya kuuelezea na kuufahamu ulimwengu unaotuzunguka. Mtazamo wetu wa kiulimwengu unaathiri namna tunavyotenda na kuwafanyia wengine, ikiwemo na maamuzi yetu. Mtazamo wa Kibiblia wa ulimwengu umejengwa katika uwepo wa Mungu, na kwamba ni Mungu pekee anayechangamana na Uumbaji Wake Uwepo wa Mungu Uumbaji Mafundisho ya Kibiblia Mpango wa Ukombozi Sheria ya Mungu
UWEPO WA MUNGU “Mpumbavu amesema moyoni mwake, ‘Hakuna Mungu. ’” (Zaburi 53: 1) Kuna aina mbili kuu za mitazamo ya ulimwengu: MTAZAMO WA WANAOAMINI MTAZAMO WA WASIOAMINI • Ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake vilitokea tu • Hakuna miungu wala uwepo wa nguvu nyingine za asili • Maisha hayana lengo wa maana, ni usitawi tu • Ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake viliumbwa na Mungu • Mungu yupo na anajali Uumbaji Wake • Tuliumbwa kwa lengo: tuishi na Mungu milele Biblia hueleza kwamba Mungu ni Mungu pekee anayetupenda na kuchangamana na Uumbaji Wake. Ni Mungu mwenye nguvu, Anayejua kila kitu, na Aliyeko kila mahali. Lakini pia Hutujali kila mmoja wetu na huvumilia kuwa nasi.
“Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru. ” (Isaya 45: 12) Biblia inaangazia kweli kuu mbili zilizowekwa tangu aya za kwanza kabisa: Mungu yupo, na Aliuumba Ulimwengu (Mwanzo 1: 1). Sehemu iliyobaki ya ukweli wa kibiblia umejengwa katika kanuni hizo mbili: Sheria, ukombozi, ufufuo… Mafundisho ya kibiblia hayatakuwa na maana yo yote ikiwa tutakana kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa muda wa siku sita. Biblia haiwezi kuwa kweli kwenye sehemu fulani tu. Kwa kweli, Uumbaji ni moja ya dhima zilizojierudia kwenye Biblia (Mwz. 14: 9; Kut. 20: 8 -11; Mhu. 12: 1; Mal. 2: 10; Yoh. 1: 1 -4; Ru. 1: 25; Kol. 1: 6; 1 Pt. 4: 19; Uf. 5: 13; 14: 6 -7…). Ikiwa tutalikubali wazo la mageuzi lililotokea miaka mamilioni yaliyopita–liwe limefanywa na Mungu au la–, tunakuwa tunakana kwamba Mungu aliivuvia Biblia.
MAFUNDISHO YA KIBIBLIA Namna tunavyoyafasiri mazingira yetu inategemea na mtazamo wetu wa ulimwengu “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. ” (Waefeso 4: 14) Kwa mfano, kwa wasioamini upinde wa mvua ni tukio zuri tu linaloonekana. Kwa wanaoamini, ni zaidi ya hilo; ni ukumbusho wa ahadi ya Mungu, kwamba hataiharibu Dunia kwa gharika tena (Mwanzo 9: 9 -17). Mtazamo wa kibiblia wa kiulimwengu unajumuisha mtiririko wa mafundisho yanayotufundisha… Namna ya kuishi Namna ya kufanya maamuzi ya kimaadili Namna ya kuwatendea majirani zetu Namna ya kufasiri ulimwengu unaotuzunguka Nini cha kutegemea baadaye Kwahiyo, elimu ya Kikristo lazima ijikite katika Biblia.
MPANGO WA UKOMBOZI “Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. ” (Warumi 3: 24) Mungu hakuuacha Uumbaji Wake pale wanadamu walipoasi. Alikuwa Ameshapanga mpango wa ukombozi; Muumbaji alipaswa afe kuwakomboa viumbe Wake (Yohana 1: 114; Marko 10: 45). Tumeitwa kushirikisha “injili ya milele” kwa wengine. Injili ina uhusiano wa karibu sana na Uumbaji (Ufunuo 14: 6 -7). Mpango wa Mungu wa Ukombozi uliwekwa kabla ya Uumbaji. Inajumuisha kifo na ufufuo wa Yesu, na tumaini jema la Kurudi Kwake kwa Mara ya Pili (1 Petro 1: 18 -20; Tito 2: 13).
SHERIA YA MUNGU “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. ” (Ufunuo 14: 12) Hakuna maadili kabisa kwa mtazamo wa kiulimwengu wa wasioamini. Kwahiyo, maamuzi ya kimaadili ya uhusiano. Hivyo inaleta maana kwa nchi tofauti kuwa na sheria tofauti juu ya tabia za kimaadili za raia wao. Hata hivyo, Biblia inatoa sheria njema ya kimaadili, isiyo badilika, ya milele, na ya lazima inayofanya kazi kwa wanadamu wote: Sheria ya Mungu (Kutoka 20: 317; Zaburi 119: 142). Adhabu ya kuivunja ni mauti (Warumi 3: 20). Hii ndiyo ilifanya mpango wa ukombozi uwepo (Warumi 6: 23). Sheria hii imejengwa juu ya kumpenda na kumheshimu Mungu pamoja na majirani zetu (Marko 12: 29 -31). Ni mpangilio wa maadili unaotuonyesha lipi jema mbele ya macho ya Mungu.
“Ni katika neno la Mungu pekee ndipo tunapata kumbu halisi ya uumbaji […] Katika neno la Mungu akili hupata somo kwa ajili ya fikra za kina, mawazo ya kina zaidi […] Hapa tunauona Utukufu wa mbinguni kama alivyojinyenyekesha mwenyewe ili kuwa mbadala wetu na kuhakikisha amesimama dhidi ya nguvu za giza na kupata ushindi kwa niaba yetu. Heshima ya juu namna ile haiwezi kushindwa kulainisha, kusafisha, na kuvutia mioyo, na, kwa wakati mmoja, kuhamasisha akili kwa nguvu mpya. ” E. G. W. (Testimonies for the Church, vol. 5, cp. 2, p. 25)
- Slides: 9