KUELEZEA HABARI ZA YESU Somo la 11 k
KUELEZEA HABARI ZA YESU Somo la 11 k wa ajili Septe mba 12, 202 0
“These things I have written to you who believe in the name of the Son of God, that you may know that you have eternal life, and that you may continue to believe in the name of the Son of God” (1 John 5: 13 NKJV )
Tunao ujumbe wa ajabu wa kuushiriki na wengine: Neema ya Mungu ipo kwa kila mmoja, sio tu kwa watu fulani walioteuliwa. Injili ni kwa kila mmoja. Msamaha, Rehema, huruma, na Neema vipo kwa kila mmoja. Yesu hubadilisha maisha yetu kwa kutumia upendo wake, na anatuhimiza kushiriki uzoefu huu na wengine ili waweze kubadilishwa. Kabla na Baada ya Yesu Wale waliomshiriki Yesu Kukataa hasira na kugawa upendo Kukataa uovu na kumshiriki Yesu na wengine Kuelezea habari za Yesu: Uhakikisho wa Wokovu Kumuelezea Yesu
KABLA NA BAADA YA YESU “hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. ” (Waefeso 2: 5) Kabla ya Yesu Waefeso 2: 1 -3 Baada ya Yesu Waefeso 2: 4 -10 Kifo katika dhambi zetu Hai katika Kristo Kufuatisha kawaida ya Ulimwengu Kuketi katika sehemu za mbinguni Chini ya utawala wa Shetani Kuokolewa kwa Imani Ukaidi Kufurahia utajiri wa utukufu wake Kufanya mapenzi yetu wenyewe Kufanya matendo mema Wana wa hasira Watoto wa Mungu (Aliowaumbwa)
KUKATAA HASIRA NA KUGAWA UPENDO “Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. ” (1 Yohana 4: 11) Watu wa kijiji cha Samaria walikataa kumpatia Yesu na mitume wake malala pa kulala. Yakobo na Yohana walijazwa na hasira, wakaomba ruhusa ili wakiangamize kijiji kwa moto wa Mbinguni kam alivyofanya Eliya (2 Wafalme 1: 9 -15). Hata hivyo, uhusiano wao na Yesu ulibadilisha hisia zao. Yakobo alipoteza maisha yake sababu ya kumshiriki Yesu kwa wengine (Matendo 12: 1 -2). Injili na waraka wa Yohana vimejaa upendo kwa Mungu na kwa majirani (Yn. 13: 35; 1 Yn. 4: 8; 2 Yn. 1: 6; 3 Yn. 1: 6 -7). Hii ni nguvu ya Yesu ibadilishayo inayotenda kazi ndani yetu.
KUKATAA UOVU NA KUMSHIRIKI YESU NA WENGINE “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile[…]” (Mathayo 8: 28) Hakuna ambaye angeweza kupita katika eneo la Gadara bila kushambuliwa na hawa watu waliopagawana pepo hatari. Yesu na wanafunzi wake walitia nanga hapo. Hata hivyo, maisha ya hao wenye pepo, yalibadilika kabisa baada ya kukutana na Yesu. Waliponywa kimwili, kiakili, kihisia na kiroho. kisha, Yesu aliwataka wakaeleza habari zao kwa watu wote katika eneo hilo. Walikuwa na kisa cha kusimulia kwa sababu nguvu ya Kristo ilikuwa imebadilisha maisha yao. Wengeeleza ushuhuda wao binafsi na kuwatia moyo wengine ili wamruhusu Yesu abadilishe maisha yao.
“Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. ” (1 Yohana 5: 13) Ujumbe wa Biblia uko wazi: wale wanaomwamini Yesu wataokolewa (Yn. 3: 15, 36; 6: 40, 47; Matendo 16: 31; 1 Yn. 5: 13). Hatupaswi kusubiri tuwe wema vya kutosha ili tuokolewe. Wokovu unaweza kupotea (Kut. 32: 33; Mt. 10: 28; 2 P. 2: 20 -21; Ufu. 3: 5, 11), Lakini hili linaweza kutokea kama tu tutamkataa Mungu kwa makusudi. Uhakikisho wa wokovu huimarisha ushuhuda wetu. Ni rahisi kushiriki/kueleza jambo unalolifahamu kwa uhakika. Daima tafuta fursa ya kuwatia moyo wengine ili wapokee zawadi ya uzima wa milele.
KUMUELEZEA YESU “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. ” (Warumi 12: 1) Alitufanya kuwa watoto wa Mungu Alitupatia uzima Alitupatia amani Alitupatia Hekima Alitufanya wenye haki Aitutakasa Alitukomboa Tunapogundua kila kitu Yesu alichofanya kwa ajili yetu, mwitikio wetu wa asili ni kutoa kila kitu kwake kwa kujikana bila kujali gharama yake na kuwaelezea wengine maajabu aliyotendea kwetu na kwa ajili yetu. Yesu anatuomba tumpatia kila kitu (Lk. 9: 23). Lakini yeye ametupatia nini? (see Yn. 1: 12; 10: 10; 14: 27; 1 kor. 1: 30)
“Tunapaswa kuwa mashahidi wa Kristo; na hivi tutakuwa pale tu tunapokua kila siku kufikia ukamilifu wa kimo cha wanaume na wanawake katika Kristo. Ni upendeleo wetu kukua zaidi na kuwa kama yeye kila siku. Kisha tutapata nguvu ya kuelezea upendo wetu kwake kwa sauti ya juu na safi, mawazo yetu yatapanuka na kuwa ya kina, na hukumu zetu zitakuwa zenye maana na za kweli, wakati huo shuhuda zetu zitakuwa zenye uhai zaidi na za uhakika E. G. W. (Sons and Daughters of God, March 6)
- Slides: 9