CHAKULA NA VINYWAJI HALALI NA HARAMU Soma uelewe

  • Slides: 46
Download presentation
CHAKULA NA VINYWAJI HALALI NA HARAMU. Soma uelewe!

CHAKULA NA VINYWAJI HALALI NA HARAMU. Soma uelewe!

UTANGULIZI. “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote

UTANGULIZI. “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na chakula” 1 Kotintho 6: 13.

VYAKULA ALIVYOPEWA ADAMU. Mwanzo 1: 29 -30. I. III. IV. V. VI. Kila mche

VYAKULA ALIVYOPEWA ADAMU. Mwanzo 1: 29 -30. I. III. IV. V. VI. Kila mche utoao mbegu Kila mti ambao matunda yake yana mbegu Chakula cha kila mnyama wa nchi. Kila ndege wa angani Kila kitambaacho chenye uhai Majani yote ya miche. Kabla ya gharika Adamu na vizazi vyake walikuwa wakiishi pamoja na hayawani wote[hawakuwa na uadui] wala hawakuwatumia kama chakula, walitumia mimea tu japo waliruhusiwa kuwatumia!

VYAKULA ALIVYOPEWA NUHU; BAADA YA GHARIKA. v Wanyama waliliwa kama chakula kwa binadamu, wanyama

VYAKULA ALIVYOPEWA NUHU; BAADA YA GHARIKA. v Wanyama waliliwa kama chakula kwa binadamu, wanyama wakawa maadui kwa binadamu, mwanzo wa wanyama pori!(Kut 23: 29) v Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu. v Kama nilivyowapa mboga za majani kadhalika nawapeni hivi vyote! v Damu ya wanyama wasiile, (maana ni uhai) v Nimrod alikuwa mtu hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA!, ndiye mwanzilishi wa ufalme na utawala wa enzi za kale hasa babeli, ereku, akadi na ninawi.

VYAKULA VISIVYORUHUSIWA KWA WANA WA ISRAELI JANGWANI. JAMII YA NDEGE VITAMBAAVYO WANYAMA SAMAKI Tai,

VYAKULA VISIVYORUHUSIWA KWA WANA WA ISRAELI JANGWANI. JAMII YA NDEGE VITAMBAAVYO WANYAMA SAMAKI Tai, mwewe Kicheche Sungura Wasiona mapezi wala magamba! Mumbi, mwari, mderi Panya Nguruwe kambale Furukombe, korongo Mjombakaka Ngamia Kipungu, koikoi Guruguru Wibari Kozi na aina zake Kenge Kunguru na aina zake; hudi Mjusi Mbuni, bata Goromoe Kirukanjia, dudumizi Lumbwi Kipanga na aina zake Nyoka Bundi, popo, mnandi Jongoo, mamba

KWA NINI WANA WA ISRAELI WALIKATAZWA KULA WANYAMA HAO? Ø Ø Walikuwa ni najisi!;

KWA NINI WANA WA ISRAELI WALIKATAZWA KULA WANYAMA HAO? Ø Ø Walikuwa ni najisi!; walikuwa si safi kwao! Asili ya wanyama hao ni wale waishio mazingira magumu, kama vile ya jangwani, miili yao imeubwa kwa namna ngumu ili kukabiliana na mazingira wanayoishi mfano ngamia. Wote hawana hali ya usafi bali ni wachafu, mfano nguruwe, kunguru, kicheche, bata, kambale na panya! Wenyeji wa nchi zile waliwatumia kama chakula na sadaka kwa miungu yao! Mfano wakaanani.

AINA ZA NAJISI. § § § Mwanamke akiwa katika siku zake alikuwa najisi siku

AINA ZA NAJISI. § § § Mwanamke akiwa katika siku zake alikuwa najisi siku 7, ikiwa mtu atamgusa, kugusa kitu alichokishika au alipokaa apapata unajisi Mwanamke alipojifungua alikuwa najisi kwa siku 7, akiwa ni mtoto wa kiume na siku 14 kwa mtoto wa kike! Mtu yeyote aliyetokwa na damu kwa mfunulizo atakuwa najisi. Mtu akishika maiti au mzoga atakuwa najisi hadi jioni ndipo aoge na kufua nguo zake Wenye magonjwa kama ukoma walikuwa najisi Kula chakula meza moja na watu wasio wayahudi ilikuwa najisi.

HISTORIA YA WANYAMA WA ISRAELI. o o o Yakobo na kizazi chake wakikwenda Misri

HISTORIA YA WANYAMA WA ISRAELI. o o o Yakobo na kizazi chake wakikwenda Misri na wanyama wao na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya kaanani; ila kwa wamisri kila mchunga wanyama kwao ni chukizo ndio maana wakapewa nchi ya Gosheni waishi huko. Walopotoka Misri walitoka na wanyama wao wengi sana; kwa sababu ya njia ndefu ya jangwani, wanyama wao wengi walikufa kwa kukosa malisho na maji na wengine waliliwa kama nyama. na wengine wachache walihifadhiwa kama mbegu na kwa sadaka! BWANA Mungu kuwaonea huruma akawapa MANA asubuni na Jioni akawapa KWARE sikuzote hadi walipofika kaanani. Kwa sababu wanyama wote wa jangwani hawana sifa ya kuliwa[najisi] na Mungu ameshawapa MANA na akawapa tena na KWARE hawana haja tena nakutafuta kula vyakula visivyo safi! Mkazo wa TORATI YA MUSA ilikuwa juu ya matendo ya sheria kama vile usafi wa mwili, matendo ya mwili, hivyo kumkaribia MUNGU walipaswa wafue nguo zao na kutoa dhabihu ya dhambi.

TAMADUNI ZA NCHI ZILE! ü ü ü Mkaanani, Mhiti, Mwamori, Mperizi, Mhivi na Myebusi

TAMADUNI ZA NCHI ZILE! ü ü ü Mkaanani, Mhiti, Mwamori, Mperizi, Mhivi na Myebusi waliwatumia wanyama hawa kama chakula na wakaviambatanisha na ibada ya sanamu(tambiko)[Danieli 1: 16] Nguruwe[kitimoto], wakaanani walimtumia kama dhabihu katika madhabahu zao kwa mungu wao wa rutuba(baali). . Isaya 66: 3 Mbali na wanyama, binadamu pia walitolewa dhabihu kama sadaka, kwa kupitishwa motoni ili miungu yao ifurahi. [Kumb 18: 912, 2 Wafalme 17: 17] Wenyeji wa nchi hizi kwa sababu ya maovu yao hasa wakaanani walipaswa wafutwe wote juu ya nchi ili Wana wa Israeli wasije wakaiga tamaduni zao na ibada zao za sabamu. Wana wa Israeli walikatazwa kuyala mafuta ya wanyama[fats]bali wayatumie kwa matumizi mengine kwani yalitumika kwa Dhabihu Kukatazwa kunywa damu za wanyama kwa sababu uhai wa mnyama uko katika damu yake. 1

NYAMA.

NYAMA.

VYAKULA KATIKA AGANO JIPYA. Ukweli kuhusu najisi. [Mathayo 15: 10 -20] �Wana wa israeli

VYAKULA KATIKA AGANO JIPYA. Ukweli kuhusu najisi. [Mathayo 15: 10 -20] �Wana wa israeli walikuwa hawali nyama za wanyama wale kwa sababu ni najisi[wachafu] �Kile kimtokacho mtu baada ya kula au kunywa ndicho kimtiacho unajisi; mfano mtu baada ya kunywa pombe atatoa, mawazo mabaya, matukano, ugomvi, uongo, matendo ya aibu hivi ndivyo vitiavyo najisi[ahesabiwe hatia, makosa] �Kula CHAKULA kabla ya kunawa hakumtii mtu unajisi �Agano Jipya mkazo umewakwa mambo ya kiroho; kama moya safi , imani, haki, rehema na neema �Chanzo [moyo]hutoka uuaji, uzinzi, uasherati, wivi, upendo, haki na tabia njema au mbaya! �Najisi katika Agano Jipya ni kuhesabiwa hatia, dhambi; tofauti na Torati ilikuwa ikimaanisha hali ya uchafu!

UNAJISI WA VYAKULA. • 1 korintho 10: 23 -31. , 6: 12 vitu vyote

UNAJISI WA VYAKULA. • 1 korintho 10: 23 -31. , 6: 12 vitu vyote ni halali, lakini sio vyote vifaavyo! Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni…. …. . Kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza. . Matendo 10: 12 -15 Petro aliwahesabu watu wa mataifa kuwa ni najisi nakula nao ni najisi pia aina zote za wanyama(mataifa yote) Ruhusa kuhubiriwa injili, Vilivyotakaswa na Mungu usiviite najisi.

JE WANYAMA HAWA[NAJISI] MUNGU ALIKOSEA KUVIUMBA? • “najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu,

JE WANYAMA HAWA[NAJISI] MUNGU ALIKOSEA KUVIUMBA? • “najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. • Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. • Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa. [Warumi 14: 14 -23] v. Waebrania 13: 9 Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo waliokwenda navyo hawakupata faida.

Vilivyotakaswa na Mungu usiviite najisi. “…. . wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na

Vilivyotakaswa na Mungu usiviite najisi. “…. . wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokelewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokelewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa na neno la Mungu na kwa kuomba”. [1 Timotheo 4: 1 -4]

 • Warumi 14: 1 -23 Mtu mmoja anayo imani anakula vyote! Lakini yeye

• Warumi 14: 1 -23 Mtu mmoja anayo imani anakula vyote! Lakini yeye liye dhaifu hula mboga!. “usihukumu wala kudharau”ili tusitie kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha, kumwaribu ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. Wakolosai 2: 16, 17 “Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato. mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. ”

VIYWAJI AGANO LA KALE � Kisha BWANA akanena na Haruni na kumwambia, usinywe divai

VIYWAJI AGANO LA KALE � Kisha BWANA akanena na Haruni na kumwambia, usinywe divai wala kileo chochote, wewe wala wanao pamoja nawe hapo uingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba usife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu. [Walawi 10: 8 -9] � Ikiwa mtu amemwekea Mungu nadhiri kubwa[kujiweka wakfu]; “. . atajitenga na divai na kileo, hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yeyote ya zabibu, wala asile zabibu mbichi wala zilizokauka”. § Basi sasa[jitahidi], jihadhari, nakuomba usinywe divai wala kileo, wala usile kitu chochote najisi. (Waamuzi 13: 4); kwa sababu Samsoni alikuwa mnadhiri wa MUNGU tangu tumboni, mama yake wala Yeye atakapozaliwa hawakuruhusiwa kutumia divai wala kileo. § Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za BWANA, hatakunywa divai wala kileo, naye atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye![Luka 1: 15]

KWA NINI TUSITUMIE KILEO AU MVINYO? • Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomwi, naakosaye kwa

KWA NINI TUSITUMIE KILEO AU MVINYO? • Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomwi, naakosaye kwa vitu hivyo hana hekima![Mithali 20: 1] • “Ni nani apigaye, Yowe? ni nani aliaye Ole? Ni nani mwenye ugomwi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; waendao kutafuta divai iliyochanganyika! • Macho yako yataona mambo mageni; na moyo wako utatoa yaliyopotoka. [Mithali 23: 29 -35] • Ee Lemueli kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, wala haifai wakuu kusema ki wapi kileo? [Mithali 31: 4]

Madhara ya mvinyo/kileo. �Wala kuhani awaye yote hatakunywa mvinyo, aingiapo katika ua wa ndani[Ezekieli

Madhara ya mvinyo/kileo. �Wala kuhani awaye yote hatakunywa mvinyo, aingiapo katika ua wa ndani[Ezekieli 44: 21] �Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu. [Isaya 28: 7] �Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; miongoni mwao walao nyama kwa pupa; kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. [mithali 23: 20 -21] �Msinywe divai, ninyi wala wana wenu hata milele[mausia kwa wana wa Rekabi](Yeremia 35: 6 -7) �Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu[Hosea 4: 11]

Madhara ya mvinyo/kileo. �Nuhu alipokuwa amekunywa mvinyo na kulewa alikaa uchi ndani ya hema

Madhara ya mvinyo/kileo. �Nuhu alipokuwa amekunywa mvinyo na kulewa alikaa uchi ndani ya hema yake na matokeo yake mwana wake[Kaanani] akamdhikaki kwa kukaa uchi, akapelekea kumtoea laana!{Mwanzo 9: 24} �Binti wawili wa Lutu walimnyesha baba yao mvinyo na baada ya kulewa wakalala nae na wakazaa wamoabu na waamoni maadui wa Israeli. {Mwanzo 19: 32} �Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao![Habakuki 2: 15]

Mlevi mmoja alisema hivi!.

Mlevi mmoja alisema hivi!.

SABABU ZA KUTOKUNYWA MVINYO AU KILEO. 1) Husababisha kufanya dhambi nyingine kwa kushidwa kufikiri,

SABABU ZA KUTOKUNYWA MVINYO AU KILEO. 1) Husababisha kufanya dhambi nyingine kwa kushidwa kufikiri, kupambanua na kufanya maamuzi sahihi. 2) Huleta hali ya kufanya mambo ya aibu na upumbavu, pasipo kuona aibu. 3) Humpa mtu ujasiri wa kufanya kwa hasira, kwa tamaa, kwa kiburi bila woga mambo mabaya. [ugomvi] 4) Ikimzoelea mtu, husababisha kushindwa kuiacha, kudumaza akili, ufahamu na kumletea umasikini na ufukara. 5) Huleta madhara ya kiafya mwilini. mfano ini, kongosho 6) Kupotoka, kupotosha hukumu.

 • Kuna maneno 2 ya kiebrania yanayotafsiriwa kama “DIVAI” kwenye Biblia A. @neno

• Kuna maneno 2 ya kiebrania yanayotafsiriwa kama “DIVAI” kwenye Biblia A. @neno la kwanza lililozoeleka ni “YAYIN”likijumuisha aina zote za divai; lilitumiwa mara 141 katika Agano la kale. pia huonesha aina mbali ya divai iliyotiwa chachu. ; kwa upande mwingine, yayin linatumika kwa maji matamu ya zabibu yasiyochachuka! B. Neno lingine la kiebrania linalotafsiriwa “DIVAI” ni “TIROSH”likimaanisha divai mpya, au divai iliyovunwa; limetumiwa mara 38 ktk Agano la Kale. kamwe haizungumzii kinywaji kilichotiwa chachu. kanuni ya kiebrania na kiingereza ya agano la kale inasema kwamba “Tirosh” inamaanisha maji ya zabibu yaliyokamuliwa sasa hivi au divai mpya! C. Neno lingine la kiebrania linalomaanisha kinywaji kilichotiwa chachu ni “shekar” linajitokeza mara 23 kwenye A. K hutafsiriwa kama bia[1 Samw 1: 15]

AGANO JIPYA NA VINYWAJI. • Neno la kiyunani “OINOS” limetumika katika Agano Jipya kumaanisha

AGANO JIPYA NA VINYWAJI. • Neno la kiyunani “OINOS” limetumika katika Agano Jipya kumaanisha divai ya aina mbili; 1)Maji ya zabibu yasiochacha 2)Maji ya zabibu yaliochachwa[yenye kulevya] § Je Yesu ktk meza ya Bwana alitumia divai ipi? I. Yesu alitumia maji ya zabibu yasiochachwa!; waandishi 3[Mathayo, Marko na Luka] wa kwanza wa Injili walitumia “tunda la zabibu” kwa habari ya meza ya Bwana, wakimaanisha divai isiyochachwa yenye takriban 20% ya sukari bila kileo II. Walikula meza ya Bwana wakati wa Pasaka; sheria ya pasaka tangu A. Kale chachu yeyote[seor]isitumike katika mikate wala vinywaji[Kutoka 12: 14 -20] III. Katika A. Kale kinywaji chenye chachu hakikutakiwa kwenye nyumba ya Mungu wala wakati wa kutoa sadaka ya kinywaji(divai) wala wahudumu wasitumie kabisa. [Lawi 10: 9]

JE YESU KTK HARUSI YA KANA ALITENGENEZA DIVAI GANI? � � i. iii. iv.

JE YESU KTK HARUSI YA KANA ALITENGENEZA DIVAI GANI? � � i. iii. iv. � Ilikuwa divai njema Mila na desturi za kuyahudi ktk makusanyiko[karamu] maandalizi ya divai na aina zake yalikuwa kama ifuatavyo; Divai iliyochachuka[iliyotiwa chachu] Divai isiyochachuka[divai njema] Divai iliyochanganywa[sehemu 20 za maji kwa sehemu 1 ya divai] Divai kali[ni najisi kwa mnywaji, haiwezi kubarikiwa] Aina zingine ni; maji ya zabibu zilizokaushwa, divai ya zabibu iliyotengenezwa kutokana na asali ya zabibu; kutokana na kuchemsha zabibu.

Utibitisho wa kitabibu na desturi za kale • Wanawake wa kirumi hawakuruhusiwa kutumia kileo[divai

Utibitisho wa kitabibu na desturi za kale • Wanawake wa kirumi hawakuruhusiwa kutumia kileo[divai iliyochachuka]…plybius* • Wamegundua kuwa mtumiaji wa kileo kwa mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa unaharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke; kuaribika mimba, akili ya mtoto, udhaifu wa mwili nk. • Mkuu wa meza alitoa maneno yenye kutibitisha ni divai njema[isiyo na kileo]

MAANDIKO AGANO JIPYA. • Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za BWANA, hatakunywa divai wala

MAANDIKO AGANO JIPYA. • Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za BWANA, hatakunywa divai wala kileo, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye!Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. [Luka 1: 15] • Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye, hivyo kwa mtu anaye hitaji ujazo wa Roho Mtakatifu hapaswi kutumia kileo chochote! • Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo kuna ufisadi bali mjazwe Roho Mtakatifu[Efeso 5: 18] • Vitu vyote ni halali; bali vitu vyote vifaavyo!, vitu vyote ni halali bali si vyote vijengavyo. [1 Kor 10: 23]

Pombe na Unywaji. AGANO LA KALE; AGANO JIPYA; Walawi 10: 8 -9. Luka 1:

Pombe na Unywaji. AGANO LA KALE; AGANO JIPYA; Walawi 10: 8 -9. Luka 1: 15 Mithali 20: 1 Efeso 5: 18 Hesabu 6: 3. 1 Koritho 10: 23, 31, 33 Ezekieli 44: 21 1 Timotheo 3: 3 Isaya 28: 7, 56: 12 Tito 1: 7 Mithali 23: 29 -35, 31: 4 Yeremia 35: 6 -7 msilewe kwa mvinyo! Hosea 4: 11 Waamuzi 13: 4

Je Biblia toleo la Roman Catholic linasemaje? • Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji

Je Biblia toleo la Roman Catholic linasemaje? • Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji ya uzima, ukinywa kiasi. Je anao uzima gani mtu asiye na mvinyo? Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu. • Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho, ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha. lakini kunywa mno ni uchungu wa roho, na fedheha na ugomvi. [Yoshua bin Sira 31: 27 -29] • Andiko hili huwatia moyo walevi, wapenda pombe kunywa pombe lakini kitabu hiki si Neno la Mungu, hivyo huwapotosha wakisomapo!

Je Biblia toleo la Roman Catholic linasemaje? • “usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa kileo,

Je Biblia toleo la Roman Catholic linasemaje? • “usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa kileo, yaani mvinyo imewaangamiza wengi. ”tanuru hujaribu kazi ya mhunzi, na mvinyo mioyo ya watu katika ugomwi wa wenye kiburi. [Yoshua bin Sira 31: 2526] • Kileo humzidishia mpumbavu mitego ya kumletea hasara; hupunguza nguvu, na zaidi huleta jeraha. [Yoshua bin Sira 31: 30] • Japo kinawatia moyo kunywa pombe, wasomaji wake huona kuwa wameruhusiwa kunywa lakini bado kuwaonya nacho kimewaonya!

Maandiko tata: �Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; kampe divai yeye na uchungu

Maandiko tata: �Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; kampe divai yeye na uchungu nafsini. anywe akausahau umaskini wake; asiikumbuke tena taabu yake[Mithali 31: 6 -7] �Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara[1 Timotheo 5: 23]

NINI MAANA YA MAANDIKO HAYA? � Tamaduni za kale zinatuambia, wafugwa walikuwa wakihukumiwa adhabu

NINI MAANA YA MAANDIKO HAYA? � Tamaduni za kale zinatuambia, wafugwa walikuwa wakihukumiwa adhabu kali kama vile kuchapwa na mijeledi viboko 40, kama vile Paulo alivyofanyiwa au kusulibiwa[kutundikwa msalabani] kwa wayahudi 200 walioteta uasi dhidi ya Herode. hivyo walipewa mvinyo ili wasiyasikie maumivu ya mapigo wanayopigwa! � Marko 15: 23[Yesu alikataa mvinyo alipopewa pale msalabani]. Luka 10: 34 ‘akakaribia, akamfunga jeraha zake, akazitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake. � Hivyo maandiko haya humaanisha, kumpa kileo maskini au mgonjwa kwa namna ya kumpatia tiba wala hamaanishi kumpa burudani. � Kuna usemi wa kiswahili unaosema “mtoto akililia wembe mpe” kama maskini anataka kunywa mvinyo ili asahau shida zake je ni kweli shida zitapungua au zitaongezeka? Mwandishi wa Mithali anatumia lugha ya mafumbo[kupima ufahamu] wa wale wanaodhani wakinywa pombe watasahau shida zao lakini bado ziko pale na zinazidi kuongezeka!

Maandiko tata: “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe

Maandiko tata: “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema. ” [Tito 2: 3] “si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu, bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha[1 Timotheo 3: 3] Ø Tamaduni za kiyahudi zinatuambia kuwa zabibu zilitengeneza bidhaa nyingi ; mfano juisi ya zabibu[divai] walipoiwekea chachu[ikawa mvinyo]; watu wa tamaduni hizi walipompa Yesu maisha yao , Paulo alikuwa akiwatofautishia aina ya bidhaa wasizopaswa kutumia tena!

IKIWA UMEKUWA MPINGAJI HATA SASA, HITIMISHO NI NINI? � Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu

IKIWA UMEKUWA MPINGAJI HATA SASA, HITIMISHO NI NINI? � Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. [1 The 2: 11] � Naye ndie aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa Agano Jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali Roho huuisha[2 Kor 3: 6] � Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu…[2 Petro 1: 20]

 • Malta na jamii zake; mf. grandmalt, vita malta; Alvaro na azam malta!

• Malta na jamii zake; mf. grandmalt, vita malta; Alvaro na azam malta! • Bavaria, redbull • Shampeni, burn

KANUNI YA KUTUMIKA KWA BWANA! � Kisha BWANA akanena na Haruni na kumwambia, usinywe

KANUNI YA KUTUMIKA KWA BWANA! � Kisha BWANA akanena na Haruni na kumwambia, usinywe divai wala kileo chochote, wewe wala wanao pamoja nawe hapo uingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba usife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu. [Walawi 10: 8 -9] � Ikiwa mtu amemwekea Mungu nadhiri kubwa[kujiweka wakfu]; “. . atajitenga na divai na kileo, hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yeyote ya zabibu, wala asile zabibu mbichi wala zilizokauka”. § Basi sasa[jitahidi], jihadhari, nakuomba usinywe divai wala kileo, wala usile kitu chochote najisi. (Waamuzi 13: 4); kwa sababu Samsoni alikuwa mnadhiri wa MUNGU tangu tumboni, mama yake wala Yeye atakapozaliwa hawakuruhusiwa kutumia divai wala kileo. § Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za BWANA, hatakunywa divai wala kileo, naye atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye![Luka 1: 15]

WALA MSIMPE SHETANI NAFASI. � � Ili makuhani wasijekufika mahali wakajikuta kwa bahati mbaya

WALA MSIMPE SHETANI NAFASI. � � Ili makuhani wasijekufika mahali wakajikuta kwa bahati mbaya wamelewa kunywa mvinyo kwa kudhani walikuwa wanakunywa divai, walinyimwa kunywa hata divai; ikiwa Mungu anapenda wanaomtumikia wawe makini sana; kunywa vinywaji hivi hatarishi vinavyotengenezwa katika kiwanda cha bia na kuondolewa kilevi tu, ili wanywao wasilewe je ikitokea wakajisahau kwa bahati mbaya wakaweka kilevi itakuwaje Kwa wanaotumika madhabahuni? waliozoea kuvinywa? Ili Roho Mtakatifu aendelee kukaa ndani ya mtu; hapaswi kulewa wala kutumia vinywaji hatarishi kama vile Yohana Mbatizaji alivyoambiwa!

MAADILI YA WOKOVU. �Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu

MAADILI YA WOKOVU. �Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. �Mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa, ili iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa. �Kama walio huru, wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu[1 Petro 2: 9, 12, 16]

MAADILI YA MAKUHANI. �Ikiwa waliokoka ni makuhani wa Bwana, wanapaswa kuwa na maadili ya

MAADILI YA MAKUHANI. �Ikiwa waliokoka ni makuhani wa Bwana, wanapaswa kuwa na maadili ya kikuhani. na Kama mtu atamwona kuhani wa Bwana anaingia baa kununua malta, wakimsingizia kuwa wamemwona akinunua bia wanakosa gani? �Ikiwa tuko huru kufanya lolote, je uhuru huo ni katika vitu venye kutiliwa mashaka? mara nyingi bidhaa feki ikishatiliwa shaka hainunuliwi tena. lakini ikiwa inazidi kununuliwa kwa wingi kuna HILA ndani yake!

KUHARIBU IMANI YA WAAMINI WACHANGA! Basi tusizidi kuhukumiana, bali mtu asitie kitu cha kumkwaza

KUHARIBU IMANI YA WAAMINI WACHANGA! Basi tusizidi kuhukumiana, bali mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. � Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula/kinywaji chako, umeacha kwenda katika upendo. kwa kinywaji chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. � Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe![Warumi 14: 13, 15 15: 2] � Ikiwa watu wanaokoka wanaacha pombe kali walizozoea kuzinywa, leo wanatamanishwa kurudi huo kwa kuoneshwa pombe zisizo na kilevi je ni kweli wanatendewa haki? �

1 WAKORITHO 8: 8 -13 inasemaje? � � � 8 Lakini chakula hakituleti karibu

1 WAKORITHO 8: 8 -13 inasemaje? � � � 8 Lakini chakula hakituleti karibu na Mungu wala hatupotezi chote tusipokula, wala hatuongezi chote kama tukila. 9 Lakini angalieni jinsi tunavyotumia uhuru wetu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu katika imani. 10 Kwa maana kama mtu ye yote mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi mkila katika hekalu la sanamu, [au mkinywa malta baa] je, si atatiwa moyo kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu? 11 Kwa njia hiyo, huyo ndugu mwenye dhamiri dhaifu, ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, ataangamia kwa sababu ya ujuzi wenu. 12 Mnapotenda dhambi dhidi ya ndugu zenu kwa njia hii na kujeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnamkosea Kristo. 13 Kwa hiyo, kama kile ninachokula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe nchi idumupo, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.

KUSHINDA KWA HALALI! � 25 Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao

KUSHINDA KWA HALALI! � 25 Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele. � 26 Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa. [1 Koritho 9: 25 -26] �Ikiwa wanariadha wanaogundulika wametumia dawa za kuongeza nguvu wananyanganywa ushindi wao kwa sababu ni batili; je mtu anapotumia vinywaji mbadala wa kileo ili ajisikie kama bado yupo duniani. je anastahili taji? �Wakristo wengine wameamua kuacha vyote ili wapige mbio kwa kasi. , kuna wengine wanatumia vitu vya kuwaongezea nguvu ili washinde kwa hila!Je Taji zao zitafanana?

TOFAUTI KATI YA VINYWAJI VIKALI NA VINYWAJI BARIDI. VINYWAJI VIKALI. � Huleta hali ya

TOFAUTI KATI YA VINYWAJI VIKALI NA VINYWAJI BARIDI. VINYWAJI VIKALI. � Huleta hali ya kushindwa kuviacha mtu anapovizoea � Huleta hali ya kutosheka anapokunywa, ili ajisikie labda nusu au kreti zima. � Ni vya gharama kubwa � Vina leta madhara makubwa kuliko faida, mfano ugomvi, kisukari, presha, umasiki ni, ukichaa, ajali n. k � Wakikosea huweza kulewesha � Ili kuongeza wateja[non-alholic] wanatumia hila. � Humwaweka watu kwenye danger zone! VINYWAJI BARIDI. � Havina hali yoyote yakushindwa kuviacha unapovizoea � Vina hali ya kutosheka mapema. � Vina gharama ndogo � Havileti madhara makubwa; mfano sukari yake, kemikali zilizotumika ndio tatizo � Kuvinywa mahali popote havileti mashaka � Wakikosea haviwezi kulewesha

Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke! � Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana

Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke! � Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. � Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao. � Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu. � Mfanywe upya roho ya nia zenu, � mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu. [Waefeso 4: 17 -18, 22 -24] Ukombozi kamili wa Msalabani hauitaji kusaidiwa ni kamili kabisa; mtu amehamishwa moja kutoka mautini kwenda uzimani hakuna kati wala kituo.

AT THE END.

AT THE END.

Study the Bible with a telescope and after that study it with a microscope.

Study the Bible with a telescope and after that study it with a microscope. Be blessed much more! By ngowi. dennis 5@gmail. com 0655329653.