BIMA YA AFYA KATI YA SHARIAH NA HALI
ﺑﻴﻦ ﺍﻟﺸﺮﻳﻌﺔ ﻭ ﺍﻟﻮﺍﻗﻊ : ﺍﻟﺘﺄﻤﻴﻦ ﺍﻟﺼﻴﺤﻲ BIMA YA AFYA: KATI YA SHARIAH NA HALI ILIVYO Sh Muhammad Issa Naibu Katibu Mkuu BASUTA
1. 0 UTANGULIZI Afya au Siha ni neema kubwa ambayo wengi wa wanadamu wameghafilika nayo; ( ﺍﻟﺼﺤﺔ ﻭ ﺍﻟﻔﺮﺍﻏﺔ )ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ : ﻧﻌﻤﺘﺎﻥ ﻣﻐﺒﻮﻥ ﻓﻴﻬﻤﺎ ﻛﺜﻴﺮ ﻣﻦ ﺍﻟﻨﺎﺱ “Neema mbili watu wengi wanazipunja: afya na faragha” (Bukhari). Kutoa huduma za afya na matibabu ni moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za nchi mbali duniani na ni moja ya mahitaji ya msingi ya mwanadamu Inaaminika kwamba, takriban Dola za Marekani Trilioni zaidi ya 2 hutumika kila mwaka kwa ajili ya kutoa hudma za afya na matibabu kwa wanadamu duninai kote
INTRODUCTION Kwa hiyo, kuitegemea Wizara ya Afya katika nchi pekee kutoa huduma za afya kwa wananchi wake husababisha kuweko kwa nakisi kati ya mahitaji na huduma zinazotolewa Hivyo basi, kutokana na hali hii, huwa ni jambo la lazima kwa serikali kutafuta njia mbadala za kufidia nakisi za bajeti za afya Hata kwa upande wa mtu binafsi, kupata huduma za afya na matibabu kwa ajili yake na wategemezi wake huwa changamoto kubwa ikisingatiwa kupanda kwa gharama za afya na matibabu siku hadi siku
INTRODUCTION Ni kutokana na mazingira haya ya uhitaji mkubwa wa kifedha kati ya serikali na watu binafsi ndiyo pakazalika fikra ya Bima ya Afya/Matibabu au kwa Kiarabu ﺗﺄﻤﻴﻦ ﺍﻟﺼﻴﺤﻲ kama sehemu ya mfumo wa bima usio wa Kiislamu Bima ya Afya/Matibabu iliibuka kama mbadala kwa; � Serikali kuwezesha kupata fedha za kuhudumia wananchi wake � Watu binafsi kuweza kumuda gharama za huduma za afya/matibabu hasa huduma za afya/matibabu za bure zinapokosekana na kuhitajika kulipa pesa ili kupata huduma hizo
2. 0 DHANA YA BIMA YA AFYA Bima ya Afya/matibabu ni mfumo ambao pesa hukusanywa kutoka kwa watu katika mikupuo iliyokubalika kati ya Shirika la Bima ya Afya la serikali au la binafsi na wanachama kwa lengo la shirika hilo kumpatia mchangiaji au wategemezi wake huduma za afya/matibabu Ni huduma ambayo mpata huduma hulipia kiasi fulani cha pesa katika mkataba kati ya pande zifuatazo; � Shirika au Wakala( ﺍﻟﻤﺆ ) � Mnufaikaji wa Hudumaza Afya/Matibabu ( ﺍﻟﻤ � Mtoa Huduma za Afya/matibabu ( ﺍﻟﻤﻘ ﻡ ﺍﻟﺨﺪﻣﺔ ﺍﻟﺼﻴﺤﻴﺔ ) )
DHANA YA BIMA YA AFYA Bima ya Afya ni moja ya aina nyingi za bima zilizoshamiri katika jamii ya wanadamu duniani kote ambapo watu hulazimishwa wakate bima hizo hat abila ya ridhaa zao Bima za Afya imekuwa jambo la lazima katika nchi nyingi hivi sasa na dunia nzim ainaelekea kwenye kufanya bima hii kuwa ni jambo la lazima kwa wanadamu wote Miongoni mwa sababu zinazofanya Bima ya Afya kufanywa na serikali kuwa lazima kwa kila mwananchi ni; Kutumika kwa kiwango cha idadi ya wananchi wanaopata huduma za afya kam akiwango cha kupima kiwango cha maendeleo ya nchi � Kuongezeka kwa gharama za afya na matibabu kiasi cha kuzielemea serikali � Wananchi kukosa uwezo wa kumud agharam akubwa za matibabu �
DHANA YA BIMA YA AFYA Manufaa ya Bima za Afya huelezwa kama ifuatavyo; � Kuziwezesha serikali kupat afedha za kutosha kugharimia huduma za afya/matibabu kwa wananchi wao � Kuwezesha amani na utulivu kwa wananchi kupitia Bima ya Afya kwa kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya na matibabu � Kuwezesha kuboreshwa kwa huduma za afy ana matibabu kwa kutumia fedha za Bima ya Afya � Kuwezesha usawa kati ya wananchi kwa kuwawezesha wanancho wote kupata fursa sawa ya kupata huduma za afya na matibabu
3. 0 UISLAMU NA BIMA YA AFYA Dhana ya Bima ya Afya ni jambo ambalo halikuweko enzi za Mtume na Maswahaba na wema walotangulia Katika Uislamu, nadharia iliyotawala ni ya undugu na kusaidiana (Ta’wun) ambapo watu walikusanya nguvu zao kwa lengo la kusaidiana tu na siyo kujipatia faida Wakati huo moyo uliotawala ulikuwa ule wa kanuni ya Maslahi ya Wote au Maswaalih Al-Mursal na ulipoondoka moyo huo pakaibuka Maslahi Binafsi au Maswaalih Alfard (individual matters)
UISLAMU NA BIMA YA AFYA Mfumo wa Bima ya Afya una shubha ya kufananishwa na Mfumo wa Takaful katika Uislamu lakini hauwezi kukidhi vigezo vya kuwa Takaful Kama mfumo wa Bima ya Afya ungekuwa ni Ta’wun Al. Ijtimaaiyyah ambapo watu hukusanya nguvu zao kwa lengo la kusaidiana wakati wa dhiki, hapo ungekubalika moja kwa moja Lakini mfumo huu ulivyo ni kama bima ya aina nyingine ambapo ndanimo mna Al-Jahallah, Kamari, Al-gharar, Riba na kula mali za watu kwa Batili
4. 0 AINA ZA BIMA YA AFYA ZILIZOPO Kwa Mujibu wa Dkt. Muhamamd Jibr Al-Ulfi, bima za afya zilizopo duniani zinaweza kugawanywa katika mafungu matano; � Ta’miin Swiihiyyi Al-Ijtimaaiyyi � Ta’iinn Swiihiyyi At-Tijaariyyi � Ta’miin Swiihiyyi At’ta’wuniyyi � Ta’miin Swiihiyyi At-tabaaduliyyi � Ta’miin Swiihiyyi Al-Mubaashara Huduma hizi ndizo zinazotumika duniani kote katika kutoa huduma ya Bima ya Afya na pengine katika nchi moja, zaidi ya huduma moja hutumika
4. 2 TA’MIIN SWIIHIYYI AT-TIJAARIYYI Ni mkataba kati ya mtu binafsi au taaisi na shirika linaloendesha huduma za bima ambapo shirika la mtu au taasisi hulazimika kulipa malipo fulani kwa mkupuo au kwa awamu ili kulipiwa gharama za matibabu au huduma za afya kwa muda maalumu Maulamaa wameafikiana kuhusu aina hii ya bima ya afya kwamba ni HARAMU 4. 3 TA’MIIN SWIIHIYYI AT’TA’WUNIYYI � Ni mkataba kati ya mtu au taasisi na Shirika la bima ya Ta’awuni kwa mkata bima kulipa kiasi cha pesa kwa mkupuoau kwa awamu ili kulipiwa na shirika hilo la bima gharama ya huduma za afya au matibabu zot eau sehemu yake pindi akiugua kwa muda maalumu � Maulamaa wamekubaliana kwamba bima hii ya afy ani HALALI
4. 4 TA’MIIN SWIIHIYYI AT-TABAADULIYYI Ni kukubaliana kwa kikundi cha watu kuchangia sawa kwa viwango sawa au tofauti kwa hiari kwa lengo la kumtibia mmoja wao pindia kipata maradhi au akihitaji huduma ya afya Mara nyingi husimamiwa na na taasisi ya kijamii yenye lengo la kuwahudumia wanachama wake wanapohitajia huduma ya afya au maradhi Maulamaa wamekubaliana kwamba aina hii ya bima za afya ni HALALI 4. 5 TA’MIIN SWIIHIYYI AL-MUBAASHARA Ni mkataba kati ya pande mbili ambapo upande mmoja (hospitali, kituo cha afya, zahanati) hulazimika kutoa matibabu na upande wa pili (mtu binafsi au kiundi cha watu) unapohitaji huduma za afya/matibabu kwa gharama maalum Maulamaa wametofautiana kuhusu je ni halali au haramu
Baada ya Uislamu kuweka kanuni hii ya jumla – Mwenye kuwafanyia watu wepesi- Uislamu unawaruhusu kuamua jinsi ya kuitekeleza kanuni hii ya kijamii kwa mujibu wa zama, mazingira na hali walizo nazo Mwongozo waliopewa ni kwamba katika kufanya hivyo wangalie walihalalishe lile ambalo Allah kaliharamisha wala wasiharamishe lile ambalo Allah kalihalalisha Panapotokea majanga, shida au madhara katik amali na maisha ya wanadamu, njia sahihi ya kupunguza madhara ya mambo hayo ni kuyagawa madhara hayo ili watu wachangie (Risk sharing) ﺗﺒﺮ ﻋﻠﻰ ﺳﺒﻴﻞ ﺗﻮﺯﻳﻊ ﺍﻟﻤﺨﺎﻃﺮ ﻭﺍﻟﺘﻌﺎﻭﻥ ﻋﻠﻰ ﺣﻤﻞ ﺍﻟﻤﺒﺘﻠﻰ
5. 0 MJADALA JUU YA BIMA YA AFYA Kama kuna bima iliyoibua mjadala mpana ni suala la bima ya afya kutokana na kuweko katika fungu la kile kinachoitwa “Bima” au ﺗﺄﻤﻴﻦ Dhana nzima ya bima ilipoanza kwa mtindo wa sasa ilipata upinzani mkubwa huku ikidaiwa kwamba haikuweko zama za Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) Lakini uko ushahidi kwamba dhana ya bima ilikuweko zama za Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) na aliikubali dhana hii ya ﺗﺄﻤﻴﻦ ingawa ni tofauti na ilivyo leo
MJADALA JUU YA BIMA YA FYA Iko hadithi sahihi ya Mtume katika Bukhari na Muslim kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash’ari (Allah amridhie) Mtume alisema; “Watu wa Ash’ari wanapokuwa safarini na kujikuta wamepungukiwa na chakula au chakula kwa watu wao mjini Madina kinapopungua, hukusanya kila kitu walichonacho pamoja na kugawa sasa sawa baina yao. Wao ni wangu na mimi ni wa kwao”. Huu ni mpango wa bima ambao lengo lake ni kupunguza madhara ya shida au janga linapotokea. Msingi huu ndio uliojengea kukubalika kwa dhana ya bima katika Uislamu kama vile Takaful na hata bima ya afya
Bima za kibiashara zisizo za Kiislamu, ziwe za afya au vinginevyo, ni haramu kwa ujumla kama tulivyoona kutokana na kuweko ndani yake Gharar, Kamari, Kula mali za watu kwa batili n. k Pamoja na hayo, Maulamaa wanasema Musilamu anaruhusiwa kuzitumia bima hizo kwa masharti yafuatayo; Pale mtu anapolazimishwa – Bima za magari au wafanyakazi wanapolazimishwa na mwajiri kujiunga na bima au mifuko y akijamii inayojishughulisha na bima mbali ikiwemo bima ya afya Katika hali hii, Waislamu wanaruhusiwa kutumia bima hizi na dhambi itakuwa juu ya yule anayewalazimisha
Pale mtu anapolazimika kuhitaji bima ya afya kutokana na kuwa masikini sana kiasi kwamba hawezi kumudu gharama za matibabu kwa ajili yake na familia yake Inapokuwa hakuna bima ya afya ya Kiislamu na bima zilizopo hazina RIBA ndani yake, Maulamaa wengi wanasema hapo ni ruhusa Muislamu kutumia bima hizo za afya KWA DHARURA kwa kuwa ina Shub-ha ndani yake Lakini inapokuwa bima hiyo ya fya ina RIBA ndani yake, kwa mfano Bima ya Maisha (Life Insurance) ambapo mtu hulipa mikupuo ya malipo kwa ajili ya kuja kupata kiasi fulani cha fedha zaidi ya alichokilipa na huku hajui atalipa mpaka lini, hapo hakuna ruhusa Musilamu kujiunga na bima hiyo Katika Maulamaa waliojuzish abima ya afya katika mazingira haya ni Dkt Fauzan, Dr. ‘Ali Muhiy al-Deen al-Qurrah Daaghi, Dr. ‘Abd al. Rahmaan ibn Saalih al-Atran, Dr. Yusuf al-Shubayli and Dr. Khaalid al-Du‘ayji. Dr.
6. 0 HITIMISHO Azimio la majmaul fiqhul Islami Na 149 kuhusu bima ya Afya BIMA YA AFYA ni jambo linalohitajika sana katika nchi masikini Kwa kuokoa maisha ni jambo la kwamba katika Maqaasi As-Shar’iyyah, bima ya afya kwa wahitaji ni jambo litakalosaidia kuwafanyia wepesi Pamoja na hayo, Waislamu tunapaswa kuendelea kufanya bidii mpaka bima za Kiislamu zipatikane lakini kwa hali ya sasa mlango wa dharura utumike ili waislamu wasiathirike kwa kukosa bima ya afya
- Slides: 21